Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu Siku Ndani ya Jeneza-24-

WIKI ILIYOPITA:
"Ndiyo kijana wangu, umekaa nusu siku ndani ya jeneza, hebu nieleze ulikuwa wapi?," aliniuliza yule mzee na kunifanya nishtuke kwani sikutegemea kama angeniuliza swali kama lile.
ENDELEA

"Nilikokuwa siwezi kusema, naogopa ila cha msingi naomba niletewe mchungaji aniongoze sala ya toba ili niokoke. Hivi kweli nimerudi duniani? Niliuliza.
"Umerudi duniani, mimi pia ni mchungaji na ndiye niliyekuwa naendesha sala ya kuuaga mwili wako kabla ya kupelekwa makaburini kuzikwa.
"Sasa kama upo tayari toka ili nikutubishe," alisema mchungaji huku akiinama ili kunitoa kwenye jeneza. Nilijitahidi nikasimama, nikatoka huku nikipepesuka.
Nilipiga magoti, sala ya toba ilipoanza tu, watu walirudi na kuingia ndani huku wakinishuhudia.
Niliongozwa sala ya toba, nikaokoka rasmi siku hiyo. Watu walishangaa sana, wengi walipenda kujua nilikokuwa kulikuwa kunafananaje, lakini sikusema na hata mchungaji aliwaambia nilikataa kusema.
Nilichoamua, ni kuwa mtumishi wa kanisa la mchungaji yuleyule pale Kilosa aliyeniongoza sala ya toba ambapo natumikia mpaka sasa. Dar nimekuwa nikija kama hivi na kurudi kule. Namshukuru sana Yesu wangu, aliniokoa kwa jina lake. Amina."

MWISHO.
 
Aisee hii somo mkuu nakupa saluti


Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Aseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…