Nunua gari kali, jenga ghorofa

Nunua gari kali, jenga ghorofa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Hayo ni maneno ya mwanangu, akitaka ninunue gari kali, means hajaridhika na nilililonalo. Matokeo ya kidato cha pili yametoka na amefaulu kidogo nikaona nimtembeze mjini kuangalia vitu mbali mbali.

Mtoto wangu akataka tuende Mlimani City, kama mnavyojua jana pale Mlimani kulikuwa na watu wazito wana sherehe. Basi nikazurura nae madukani, tulivyotoka nikasema twende upande wa sherehe (tupite karibu na ukumbi kwenda kwenye lile duka lingine la wachina kula upande wa pili). Basi nikapita na mwanangu pale, nje kulikuwa na askari kibao wakiona gari halihusiki wanakuelekeza kupita kwa haraka. Nikawaza kunanini hapa? Maana ukumbi ulipambwa hadi nje.

Mwanangu akaona magari makali yamepaki nje, akaniambia "enhee kama hili". Nikasema sawa mwanangu tutanunua. Oya yeyote aliyefanya sherehe jana pale Mlimani City hall ni tajiri haswa maana nje pale waliweka Fountains za kutosha kwa sample. Halafu ukumbi mzima ulininginizwa taa kwa nje. Wale walinzi as if ni mkutano wa kitaifa. Gari ya bei rahisi zilizopaki nje pale ni la milioni 100 nadhani.

Anyway, nimekuwa inspired na mimi kuwa na maisha ya vile, na nitafika kwa dua za mwanangu maana amesema anaendelea kupiga dua ili mashavu yafunguke nimiliki gari kali na ghorofa. Nikasema Amen!
 
Ni umaskini wa nchi zetu tu , ndio unasababisha watu Kuona kuwa na magari ndio mafanikio makubwa kiuchumi .
Yeah sure.

Nchi kama USA kuwa na gari ni basic need tu. Wala sio utajiri.

Wakati fulani hapa Tanzania 🇹🇿, miaka ile ya 70, 80 mpaka 90. Kwenu mkiwa na baiskeli zile za phoenix nyie wakishua hatari.

Au hata mkiwa na TV 📺 tu, nyie wakishua.

Umaskini sio poa. Kitu kidogo tu kinakufanya uone fulani wakishua. Kumbe ni kawaida sana.
 
🇺🇸 USA.
Kwa US, gari ni kipimo cha mafanikio, I have been there! Najua gari unaloendesha lina-determine heshima unayopewa. Na US ina consumerism kubwa than what you are told.

US ukitumia usafiri wa Umma wanajua kabisa unahitaji msaada unaingia kwenye kundi la "broke guys" ambapo hata kupata mapenzi ni lazima udeal na vibonge only.

So sio kweli kwamba US gari sio kipimo cha mafanikio, thus ni kawaida kusikia mtu kwanza akikutajia magari aliyonayo.
 
🚮
 
Kwanza USA 🇺🇸 hakuna mtu mwenye time na maisha ya mtu.

Hakuna wa kukupa heshima, eti kisa gari unalo endesha.

Usidanganye. It seems you haven't been there.

Gari ni kipimo cha mafanikio kwa maskini wengi Afrika. Sio USA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom