Nukuu takatifu ya Mkuchika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nukuu takatifu ya Mkuchika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, May 15, 2009.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kutokana na umuhimu wake katika taifa letu, nimeamua kutundika hotuba iliyotolewa na Mheshimwa Mkuchika Huko Busanda kwenye kampeni za uchaguzi kwenye jimbo hilo. Ni hotuba inayohitaji tafakuri ya kina sana.hotuba hii nimeitoa kwenye gazeti la leo la Nipashe.

  Mapema jana asubuhi Mkuchika aliwacharukia waandishi wa habari wanaoripoti habari za vigogo wa CCM kuzomewa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Zakaria, Mkuchika alisema CCM ina nguvu na inakubalika ila waandishi ndio wanaifitini.

  “Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,”alifoka Mkuchika.
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Huyu jamaa ni kumn'goa ubunge tu.
   
 3. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180


  Hwana umeme, kwa nini? Magazet hayafiki, kwa nini? Hawana uwezo wa kununua magazeti, kwa nini? Nani kawaweka wananchi katika haya mazingira hata hawawezi kuwa na TV, Umeme wala kusoma gazeti? Kwani aliyesababisha haya yote hajulikani? Uwiiiiii
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Hivi huyu jamaa ni mbunge wa wapi???

  Tusuburi 2010, kila mmoja kivyakevyake, Hakuna kupeleka timu nzima kupigia kampeni mtu mmoja. Hakuna cha tingatinga wala baba yake tinga tinga. Hapo ndipo mchezo utakaponoga.
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mbunge wa Manyoni.
   
 6. N

  Nampula JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ama kweli watz tumeliwa hata mkuchika waziri?
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135  Jamani CCM ni la kuvunda.. yaani hata wanayo yasema hayaeleweki, sasa hiyo ni speech ya kumnadi mgombea mbele ya wapiga kura? yaani kuwadhalau hivo? mhh...
   
 8. H

  Hondo Member

  #8
  May 15, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba resume ya huyu Mkuchika pia kama kunamtu anajua uchapaji wake wakazi atutokezee, hawa ndio wanaopata vyeo kwa uchawi kwani hawana lolote ni mpuuzi.
   
 9. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Wangeandika Mkuchika kashangiliwa huku ukweli alizomewa angewapongeza hao waandishi? Hii si kauli ya kutamkwa na mtu ambaye ana dhamana ya uwaziri wa nchi, hata kama ni kada wa chama. Inawezekana kuwa waziri katika nchi hii si lazima uwe na akili timamu au siyo kigezo muhimu.
   
 10. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  Duu! anajikaanga mwenyewe kwa mafuta yake!! hivi aliyoyasema si kuwakebehi na kuwatukana watu wa Busanda? aliyesababisha haya ni nani si utawala wa CCM? soma - Chukua Chao(wananchi) Mapema. Na kama naibu katibu mkuu anakili kuwadhoofisha kiuchumi wana Busanda kuna haja tena kuwapa ubunge waendelee kudhoofisha? GOD FORBID!

  Tumefisadiwa kiasi cha kutosha
  Tumepuuzwa kiasi cha kutosha
  Tumenyonywa kiasi cha kitosha
  Utawala dhalimu wa ccm ndiyo uliotufikisha hapa
   
 11. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kazi kwelikweli. Tatizo tanzania kuchaguana kwenye hii serikali yetu. Hakuna kujali mtu huyu anauwezo gani,je yupo kwaajili ya maslai ya taifa/binafsi? Majibu yote 2010 wataita press tena tuone.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Hapo alikuwa na maana kwamba wananchi wakipata uwezo wa kununua Tv na kupata pesa ya kununua magazeti watajua mengi wasiyotakiwa kuyajua na hivo wanaweza kuipiga ccm chini,masikini wadanganyika,halafu wa huko vijiji wanatia huruma kwasababu ni wapole na wanyenyekevu wenye ukarimu. Wa Tarime ni tofauti kidogo,wa Busanda sijui,tusubiri tuone,lakini kama hayo aliyoyasema ni ukweli na wananchi hao wameyasikia na bado wakaichagua ccm,then hapo tutajua kuwa umasikini na ujinga ni utamaduni wetu na kwamba nothing else can be done in this generation if we are to preserve peace.
   
 13. A

  August JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kumbe CCM sera yao ni kudumaza watu wamaeneo fulani ili wasiwe na akili ya kujua mambo, na badala yake waipigie CCM, ndio maana nashanga miaka 48 ya uhuru Songea Umeme wa Kubabaisha, Lindi Mtwara Hivyo Hivyo, Shinyanga Tabora, Rukwa, Mwanza, Singida , Dodoma na Mlogolo ( Morogoro) Hivyo Hivyo, ili watu wasielemike usiwape umeme na barabara. Tosha, na hata Adam Lusekelo aliandika kwenye makala zake mojawapo, tafsiri ya kudumaza elimu tanzania
  Hii inaitwa weapons of Mass Destruction, huji cha afya wala cha nini ni kuwa Mtumwa wa mawakala wa Pamba kwa kwenda Mbele
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ina maana kuipigia kura CCM ni kuafiki na kukubali hiyo hali iendelee - wananchi wazidi kukaa gizani ili wezi waendelee kuiba. Nilijua tu kuwa hawana mkakati zaidi ya huo lakini na sisi wengine twasema - tutawamulika tu hata kwa vigenge vya moto !!
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145


  !!!!!! t.uc g..cuf a tahw
   
 16. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  CCM's weapons of mass Destruction kudumaza elimu tanzania
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Hwana umeme, kwa nini? Magazet hayafiki, kwa nini? Hawana uwezo wa kununua magazeti, kwa nini? Nani kawaweka wananchi katika haya mazingira hata hawawezi kuwa na TV, Umeme wala kusoma gazeti? Kwani aliyesababisha haya yote hajulikani? Uwiiiiii

  TAKATAKA MKUBWA HUYU TENA ANGETAKIWA ATUPWE SELO KWA KAULI ZA KASHFA VILE

  KAMA HAWANA UMEME,,MAGAZETI HAYAFIKI,HAWANA PESA YA KUNUNUA,HAWANA UWEZO WA KUSIMA MAGAZETI,CCM IMEKALIA JIMBO LILE MIAKA YOTE,

  THEN TAKATAKA ZA CCM ZINAENDA KUFANYA NINI...CI WAACHIE WENYE KULETA UMEME WENYE KULETA ELIMU....SHAME MKUCHIKA N FAMILY

  BUSANDANIAN
   
 18. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Iwapo tutaendelea kuwa na viongozi wenye dharau na maneno ya kashfa kama aliyotoa huyo waziri Mkuchika.....basi hatutakuwa na maendeleo.
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  HAYA NDIO MAISHA ANAYOFURAHIA WAZIRI MWENYE MAMLAKA KUWAHUDUMIA WATANZANIA ATI NI MWANAJESHI SIJUI ALIKUWA ANATUMIKIA JESHI LIPI .WANAJESHI WOTE WANA HURUMA YA MWENNYEZ MUNGU HUYU ANAFURAHIA WENZAKE MABAYA LOH

  Upungufu wa chakula watishia vijiji Dodoma

  Vijiji vya Chikola, Kigwe, Nholi, Mwitikira, Mchito na Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma vimetajwa kuwa na hali mbaya ya upungufu wa chakula. Upungufu wa chakula umevikumba vijiji hivyo tangu Aprili mwaka huu na kuwafanya baadhi ya wananchi kusaidiwa chakula na serikali ya kijiji.

  Akizungumza katika kikao cha ushauri cha wilaya hiyo kilichofanyika juzi wilayani hapa, Ofisa Kilimo wa Wilaya, Sylvester Kashaga alisema hali hiyo imesababishwa na maeneo hayo kukosa mvua kabisa katika kipindi cha msimu wa mvua uliopita.

  Kashaga alisema kwa mujibu wa tathmini ya hali ya mavuno shambani na upatikanaji wa chakula iliyofanywa katika vijiji, kata na tarafa zote za Wilaya ya Bahi kuanzia Machi 10 hadi 28, mwaka huu, ilibaini kuwapo kwa upungufu wa tani 51,093.46.

  Alisema mahitaji halisi ya chakula katika Wilaya ya Bahi kwa mwaka ni tani 61,172.77 kutokana na hali ya ukame ambapo mavuno tarajiwa ni tani 10,079.31 hivyo kusababisha upungufu wa tani 51,093.41. Ofisa Kilimo huyo alisema katika vijiji hivyo, tayari upungufu wa chakula umeshajitokeza tangu Aprili na katika vijiji vilivyobaki upungufu huo utajitokeza kuanzia Juni.

  Baadhi ya watendaji wa kata waliohudhuria kikao hicho, walimueleza Mkuu wa Wilaya hiyo, Betty Mkwasa kuwa hali ni mbaya sana katika maeneo yao na hivyo kuomba utaratibu ufanywe kuwanusuru. Watendaji walioomba kusaidiwa chakula haraka ni wa kata za Lamaiti, Bahi, Kigwe na Chipanga ambao walisema tayari serikali za vijiji zimekuwa zikisaidia baadhi ya familia ambazo hazina kabisa chakula.
   
 20. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Uhalisia wa viongozi wa CHICHIEMU ndio huo na wala hakuwa anatania bali ni kutoka moyoni mwake, akiwasemea na wenzie wana CCM "WACHACHE" narudia WACHACHE... wasiotaka kuuona ukweli, wasioamini kuwa kuna watu wengine wanaweza kuongoza vizuri kuliko wao, Mkuchika anakata tamaa lakini bado anaamini kuwa atashinda kwa mbinu anazojua yeye na si kwa kutumia media kwani nyenzo hizo hazifanyi kazi vijijini na ana mbadala wake moyoni ambao wengi tunahisi lakini 24/05/09 itatupa jibu
   
Loading...