NSSF & PPF Tujengeeni nyumba sisi wanachama wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF & PPF Tujengeeni nyumba sisi wanachama wenu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ELNIN0, Jan 17, 2011.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Nimetoka NSSF kuchukua kadi mpya sasa hivi pia nikapata kucheki salio langu, yaani wakinipa hizo pesa leo nina uhakika wa kuwa na nyumba ya kisasa.

  Ombi langu kwa mifuko hii wangebuni miradi ili watuwezeshe na sisi wanachama wao tunufaike kwa mfano ujenzi wa nyumba za kisasa na kutukopesha sisi wanachama wake kwa riba nafuu wakitumia masalio yetu kama dhamana ya mikopo.

  Kama hawatoi mikopo hata mi naona hakuna haja ya mamilion yangu wakae nayo wakati mi nahangaika kukopa benki wa riba kubwa, na hii ndiyo inachangia watu wakibadili mwajiri wanazivuta pesa sababu hakuna faida unapata zikiwa huko.

  Kama kuna mtu humu anafanya katika mifuko hii ya jamii atupe ufafanuzi zaidi hasa hili la kuwekeza kwenye nyumba na kuwakopesha wanachama wake.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Wanasubiri kifo cha mwanachama watoe jeneza na sanda
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Majimbo, kama mwanachama ana akiba yake tuseme inazidi 20m kwa nini asitumie dhamana hii kukopeshwa vitu vya msingi kama nyumba, elimu? kwa nini wao wanatumia pesa zetu kuwekeza kwenye majengo na kuyakodisha ki biashara ali hali wanachama wanabakia wamechokaa chakari.

  Hizi benefits na riba wanazitoa ni ndogo sana ambazo haziwezi kumtoa mwanachama from point A to B.
   
 4. S

  Somi JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  watakujengea vipi hiyo nyumba wakati kulipa ela yenyewe kasheshe wakati hiyo ni ela yako sio yao uliwaazima mtaji wakazungushie .mimi nawadai ela nssf mpaka sasa urasimu mtupu sijalipwa ela yangu na muda wa miezi sita(toka nimeacha kazi) umeshapita wa kuchukua!! na sijui wanalipa ileile wanayokukata au wanalipa na riba, mwenye kujua anieleweshe.
   
Loading...