NSSF, BOT, Bandari, TRA, Bunge, PSPF ajira zitenguliwe

NSSF, BOT, Bandari, TRA, Bunge, PSPF ajira zitenguliwe

Pagan Amum

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
1,930
Reaction score
4,409
Pamoja na mambo mengine kilichopelekea maboss wa NSSF kutenguliwa jana ni upendeleo katika ajira. Leo gazeti la Jamhuri limeonyesha jinsi Bunge linavyofanya upendeleo katika kutoa ajira.

Jana Bandari na BOT pia zililalamikiwa na taasisi ya SSRC, najua yatakuwa ni maamuzi magumu ila kwa manufaa ya taifa na kwa manufaa ya watoto wa masikini ambao hawana Godfathers katoka hizo taasisi ni sharti Rais pamoja na wizara ya utumishi itengue nafasi zote katika hizo taasisi ili ajira zitangazwe upya.

Najua kuna taratibu za kisheria ila katika hatua hii ya mpito kufata sheria sio muhimu sana la msingi ni kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa na katika hili vijana wote watoto wa masikini na matajiri wapate fursa sawa.

Kama nchi tuko katika kipindi cha mpito. Tunamshukuru Mungu kutupa Rais Magufuli ambaye anafanya vyema sana. Tunamuomba katika hili la ajira aliangalie pia, kwenye taasisi za umma ajira zinatolewa kwa upendeleo kama njugu.
 
Naunga mkono Uzi. Hizi ajira za upendeleo ktika taasisi za umma zitatipeleka pabaya sana.

Kabisa Mkuu.... Chiku aliyekuwa mkurugenzi wa Utawala jana katumbuliwa kwa kuingiza zaidi ya watu 87 wasio na sifa.... Na kati ya hao 23 ni ndugu zake...
 
watoto wa wakulima wanaajiriwa halmashauri tu sitimbi hukoooo..

ila watoto wa vigogo ni ma nssf, tpa, tra na huko huko tu

Kwa nia njema aliyonayo Rais Magufuli hiyo kitu inakoma muda si mrefu...

Saizi mtu atapata ajira kutokana na sifa zake. Tena napendekeza tume ya ajira ifanyiwe maboresho makubwa kabisa..
 
Pamoja na mambo mengine kilichopelekea maboss wa NSSF kutenguliwa jana ni upendeleo katika ajira. Leo gazeti la Jamhuri limeonyesha jinsi Bunge linavyofanya upendeleo katika kutoa ajira.

Jana Bandari na BOT pia zililalamikiwa na taasisi ya SSRC, najua yatakuwa ni maamuzi magumu ila kwa manufaa ya taifa na kwa manufaa ya watoto wa masikini ambao hawana Godfathers katoka hizo taasisi ni sharti Rais pamoja na wizara ya utumishi itengue nafasi zote katika hizo taasisi ili ajira zitangazwe upya.

Najua kuna taratibu za kisheria ila katika hatua hii ya mpito kufata sheria sio muhimu sana la msingi ni kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa na katika hili vijana wote watoto wa masikini na matajiri wapate fursa sawa.

Kama nchi tuko katika kipindi cha mpito. Tunamshukuru Mungu kutupa Rais Magufuli ambaye anafanya vyema sana. Tunamuomba katika hili la ajira aliangalie pia, kwenye taasisi za umma ajira zinatolewa kwa upendeleo kama njugu.
Usisahau TTB NA TANAPA
 
uko sahihi mleta mada, watu tuliacha kufanya interview kwenye baadhi yamashirika maana ilikua ni maiigizo watu tayari wameshaajiliwa tunapotezeana mida tu..
 
Na vyuo vikuu vya umma. UDSM, SUA na UDOM zimulikwe tena sana. Kubebana kikabila na kidini.
 
Nafasi zipi zitenguliwe sasa???
Ni mpya au zile ambazo ajira tayari???
Be objective dogo.
 
Fanyeni kazi za kilimo au jiajiri, acha kuwa mnalalamika tu kila siku.
Degree zenu zitakuwa PASS, GPA >3.5 hawanaga shida maana wanaanzia kazi za kujitolea kufundisha shule za PRIVATE na Vyuo vya Private, angalau wanapata posho ya nauri, huku wakiangalia kazi mpya za serikali.
Nyie PASS ndo mnashinda mitandaoni kulalamika maana hamna mvuto kokote.
 
Tanesco nalo ni jipu, piga chini wote ajira zitangazwe upya
 
Back
Top Bottom