Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 88,375
- 154,702
Mtoto wa Gorbachev alituzingua sana.So ndio mkaunga tela sio
Mara kakaa kidogo kamtumia Mama yake Benz. Mara katutumia CD kama 1,000 hivi anatuzingua.Ilimradi wadogo zake tukaona tunataka kwenda huko duniani. Hizi biasharabiashara kawasaidia sana ndugu, wengine kawavuta wakaenda kukaa naye Europe.
Ila yeye alijikita Greece na Italy mimi nikaanza Unyamwezini.
Kuna wakati tulikuwa tume park gari yake moja Migomigo, watoto wa Magomeni mabaharia kuiona tu, wakatufuata.
Wakatuuliza, nyie wadogo zake Mtoto wa Gorbachev?
Tukawaambia ndiyo, kwani vipi?
Wakasema tunaijua hii gari alikuwa anaendesha akiwa hapa mjini, kaka yenu mtu mmoja roho safi sana alituokoa tulivyokuwa hatuna njia beach hapo Pereia kwa Wathesaloniki Ugiriki.
Watoto wa kihuni Migomigo walikuwa wanamfagilia sana kwa sababu kashawapiga tafu wengi sana hapo Greece na Italy miaka hiyo ya nyuma watu kabla hawajasafiri sana.
Kwa mtaji huo safari ilikuwa si kitu cha ajabu kwa sababu kuna watu walishatuonesha mfano kwamba maisha yako viwanjani.