Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Leo Novemba 12, 2025 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo iliahirishwa Jumatatu ya Novemba 10, 2025 baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Thawabu Issa kuieleza mahakama kuwa mshtakiwa hatoweza kufika mahakama kutokana na hali ya usalama katika jiji la Dar Es Salaam kutokuwa nzuri.
Wakili huyo aliieleza mahakama kuwa taarifa hizo walipokea kutoka kwa Mkuu wa Magereza baada ya kumuuliza kwa nini mshtakiwa hajafikishwa mahakamani.
Siku hiyo pia jamhuri iliomba kesi kuahirishwa kwa siku 14 kutokana na mashahidi waliopaswa kutoka mikoa ya Ruvuma na Mbeya kushindwa kusafiri kuja Dar es Salaam kwa sababu za kiusalama.
Hata hivyo timu ya Majaji watatu wanaosikiliza kesi hii wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru uliiagiza wito kutolewa kwa magereza ili Lissu afikishwe mahakamani leo na pia mashahidi waletwe ili kesi iweze kuendelea.
Ikumbukwe Lissu ambae anatimiza miezi saba gerezani toka April mwaka huu alipokamatwa, katika kesi hii anajitetea mwenyewe baada ya kuomba katika Mahakama ya ukabidhi (Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu) ajitetee huku jopo la mawakili zaidi ya 30 lililokuwa lilikimtetea wakibaki kama washauri.
Leo kuna kila dalili kesi itaendelea. Kwasababu Lissu ameshafikishwa asubuhi ya leo na maandalizi yanavyoonekana hapa Ukumbi namba 1 wa Mahakama kuu, shauri litaendelea.
Maandalizi yapo kama ambavyo huwa yanafanyika siku kesi inasikilizwa. Wafuatiliaji mbalimbali wanaendelea kufika mmoja mmoja na pia amefika Naibu Katibu Mkuu wa Chama, Amani Golugwa, yupo pia Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" na Godbless Lema pia wamefika hapa Mahakamani.
Muda wowote kuanzia sasa shauri linaweza kuanza kusikilizwa.
Sehemu ya 146
Mheshimiwa Lissu ameingia Mahakamani kama kawaida akiwa na vibe amekoroga "amezungusha ngumi" akiwa na morali ya kutosha.
Kama kawaida ameambatana na maaskari magereza wakutosha ambao huwa wanamlinda.
Siku za karibuni tulisema sehemu ya askari hawa wamekuwa ni wapya sio tunaowafahamu wa siku zote.
Inapigwa High Courttttttttt kubwa sana na kali.
Watu wote wamesimama hapa na Majaji wanaingia.
Sauti ya Askari imeendelea hadi Majaji wamefika kwenye viti vyao na kukaa ndio ameacha huyu askari.
Mawakili wa Serikali wamejitambulisha na kusema leo wana shahidi na wako tayari kuendelea na kesi.
Shahidi waliyenae leo ni shahidi wa siri ambae ni P11 kwahiyo wako tayari kuendelea Jamhuri.
Anaulizwa Mh. Lissu kama na yeye yuko tayari.
Mhe. Lissu anasema:
Niko tayari waheshimiwa lakini naomba niseme neno dogo tu sio la kuweka kwenye rekodi.
Jaji anashangaa sio la kuweka kwenye rekodi ni jambo gani hilo na lina umuhimu gani sasa?
Mhe. Lissu anajibu ndio waheshimiwa majaji sio la kuweka kwenye rekodi na neno langu sio lingine bali ni kwamba,
Nimefurahi kuwaona maana huko nilikokuwa hizi wiki mbili hakukuwa kwa kawaida.
Watu wote wameangua kicheko mahakamani hadi Majaji wamecheka.😂😂😂
Anaendelea Mh. Lissu
Mh. Jaji hapa Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameiambia Mahakama kuwa kuna mashahidi wengine wa Siri na hivyo leo tutakuwa na Shahidi P11.
Huyo Shahidi wa siri ameingia na Mahakama haijamuona.
Sasa nina pingamizi, waheshimiwa majaji huyo shahidi wa siri anatakiwa asimame kwenye kizimba na sio huko ambako haonekani.
Napenda kuwafahamisha kwamba hili suala la ulinzi wa mashahidi, nimelitafakari kwa zaidi ya miezi 6 sasa na nimeliangalia kwa makini sana.
Naomba kutoa hoja kwamba, hakuna shahidi yoyote kwa amri iliyotolewa na mahakama hakuna shahidi hata mmoja ambaye anatakiwa kutoa Ushahidi akiwa hapo kwenye kificho, anatakiwa akae hapo kizimbani.
Naomba nianze na sheria kwamba inasema nini? hapa Lissu ameandaa nondo za kutosha naona yuko imara kuanza pambano hili la kisheria.
Mahakama imejaa utulivu na kamvua kameanza kunyesha kwa mbali.
Watu wametulia utafikiri wanasubiri kuchomwa sindano au wanasubiri kupewa utaratibu wa kuanza kumuaga marehemu. Utulivu ni mkubwa sana.
Naomba nianze na sheria sasa kwamba inasema nini kuhusu hawa wanaoitwa Mashahidi wa siri?
Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025, zimeeleza hicho kiboksi hapo ni kitu gani kisheria?
Sasa kisheria kinaitwa kizimba maalum cha shahidi na kwa kanuni hizi kizimba kimetafsiriwa kwenye kanuni ya 3 kuwa ni sehemu ya kusimama au kukaa wakati wa kutoa Ushahidi iliyoandaliwa mahususi ili kutoa Ushahidi bila kuonekana isipokuwa na Jaji au Hakimu.
Nasisitiza isipokuwa kwa Jaji au Hakimu. Sasa swali Je hapo alipokaa shahidi waheshimiwa Majaji mnaweza kumuona huyo shahidi?
Majaji wanashangaa na kila mtu anashangaa, Waheshimiwa majaji kwa macho yangu shahidi hapo haonekani kwa majaji, wala mimi simuoni. Watu pekee wanamjua ni hawa mawakili wa serikali waliomleta akina Katuga.
Mhe. Lissu anaendelea kuweka ngumu kuwa huyo shahidi asiyeonekana kwa majaji, kwa mshtakiwa ni shahidi wa namna gani?
Kwa misingi gani ya haki katika dunia hii? Mhe. Lissu anahoji huyu shahidi anapaswa kusikilizwa.
Labda nichomekee kidogo ili mpate picha. Hicho kibox anachosadikika shahidi kipo sehemu ya juu pembeni kidogo na mlango wanaoingilia majaji.
Ni kibox kimetengenezwa kama kasanduku hakuna mtu unaweza kumuona ukiwa upande wowote maana kimezungushiwa pande zote nne so huwezi kumuona kabisa. Pia hakijawekwa hapa kwa sehemu ya mashahidi wanaposimama siku zote. Kiko kule juu kabisa. Hata majaji hawawezi kumuona aliyepo ndani ya hicho kibox chao. Kwa mbele kina kama kioo kidogo lakini pia huwezi kuona ndani kuna nini kupitia hicho kioo.
Sehemu ya 147
Anaendelea Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji,
Hoja yangu ya pili ni kwamba, huyo shahidi ni shahidi wa namna gani?
Kwa mujibu wa kanuni ya 3 lazima awe yuko chini ya amri ya ulinzi.
Sasa Mahakama hii inawezaje kujua shahidi kama yuko chini ya amri ya ulinzi?
Naomba kuwarejesha kwenye Kanuni ya 5(1) ambayo inasema mtu huyo lazima awe amebainishwa katika maombi.
Maana ya haya maneno ni nini?
Maana yake rahisi ni kwamba mtu ambaye jina lake lilipelekwa kwa jaji likaombewa ulinzi.
Jaji awe anamfahamu kwa jina na kuwa maisha yake yako hatarini.
Naomba niwarejeshe kwenye hati ya maombi ya tarehe 14 Julai 2025, hiyo application ina viapo viwili, ina kiapo cha SSA Mose Kaima na ACP Amini Mahamba.
Waheshimiwa majaji kwenye hiyo hati ya maombi, hivyo viapo viwili hakuna kiapo hata kimoja chenye jina la shahidi hata mmoja.
Katika orodha ya mashahidi wanaoitwa wamepewa ulinzi, hakuna hata jina moja la shahidi ambalo lilipelekwa kwa Jaji Mtembwa.
Hiyo amri ilitolewa on insufficient ground na ilitolewa kwa concealment (kwa kuficha Ushahidi kwa mahakama) na mawakili wa serikali.
Walipaswa kupeleka majina kwa jaji lakini hawakufanya hivyo, hivyo Jaji Mtembwa hawafahamu na nyie waheshimiwa majaji hamuwafahamu, wanajulikana tu na waliowaleta, hivyo sitaki kusema kuwa amri ya ulinzi ilipatikana kwa fraud but by concealment by the State Attorneys.
Waheshimiwa majaji kama hiyo ni haki then tunahitaji tafsiri mpya ya haki huku Duniani.
Waheshimiwa majaji sio tu kuwa hakuna majina ya mashahidi ila hakuna hata majina ya wanaowatishia ni maneno tu, maneno matupu kabisa.
Hata nature ya vitisho haijaelezwa kwamba wanatishiwaje, kivipi na nani anawatisha? Haipo kabisa.
Waheshimiwa majaji, sasa niende kwenye hoja yangu ya tatu ambayo ni kuhusu amri ya Mahakama Kuu;
Mahakama kuu ilitoa ulinzi upi? Ili kujibu hilo swali sawasawa naomba nitangulize kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi.
Kanuni inasema kwamba hatua za ulinzi wa shahidi zitadumu kwa kipindi cha usikilizwaji wa kesi isipokuwa kama amri husika itaashiria vinginevyo.
Kwenye uamuzi wa Jaji Mtembwa maombi ya Jamhuri yalikuwa kutokuonyesha utambulisho wa mashahidi wanaotarajiwa kwa kutokuweka wazi nyaraka zinazoweza kupelekea shahidi kujulikana, matumizi ya majina bandia, amri nyingine yoyote kwaajili ya usalama wa mashahidi wa Jamhuri wakati wa mwenendo wa ukabidhi au wakati wa kesi kusikilizwa.
Naomba waheshimiwa majaji pia muangalie kanuni ya 6(1) ili muone ni maombi gani mengine ambayo kama upande wa mashtaka wangetaka wangeyaomba.
Kanuni hii imetaja orodha ya amri zinazoweza kuombwa na kutolewa na mahakama. Zimeelezwa kwa uwazi kabisa kwenye kanuni husika hii itatusaidia kuelewa ninachotaka kukisema.
Waheshimiwa majaji, katika kanuni hiyo ya 6 kuna amri 16 ambazo zinaweza kuombwa na hiyo ya kutumia kizimba maalumu hawakuomba mawakili wa serikali.
Katika dunia hii waheshimiwa majaji, usipoomba hupewi, hili sio takwa la kisheria tu ni takwa pia la kibiblia kuwa ombeni nanyi mtapewa.
Jamhuri walipewa amri nne walizoomba lakini amri ya kutumia kizimba maalum hawakuomba, hivyo hawawezi kupewa kitu ambacho hawakuomba katika lugha ya kisheria, they are estopped.
Waheshimiwa majaji kwa maoni yangu kanuni hizi zilitungwa kuwafurahisha waendesha mashtaka na watu wao. They are totally one sided.
Waheshimiwa majaji kwa mujibu pia wa kanuni ya 8 kama Jamhuri wangeona amri za Jaji Mtembwa haikulinda mashahidi sawa sawa walikuwa na fursa ya kuleta maombi mbele yenu kwa mfano kuwa tunaomba kutumia kizimba maalum, hawajaleta maombi hayo.
Now it is late in the day to sneek in today kuleta hao mashahidi. Wameleta wakijua kanuni hizi hamtazisoma au mshtakiwa atanyamaza. Wamelalia haki yao, waachwe waendelee kuilalia.
Sehemu ya 148
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja yangu ya nne Waheshimiwa Majaji ipo kwenye kanuni ya 6(2) ambapo Mahakama inaweza kutoa amri bila kuathiri haki ya kusikilizwa kwa usawa.
Waheshimiwa majaji naomba hiyo kanuni isomwe pamoja na kanuni ya 5(2)(f) ambayo inasisitiza kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kwamba kuna effective cross examination.
Waheshimiwa Majaji naomba mtafakari hayo maneno ya mahitaji ya fair trial, kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kuna effective cross examination.
Waheshimiwa majaji kwenye kesi ambayo adhabu yake ni kifo, shahidi akatoa Ushahidi ambaye Mahakama haimfahamu, mshtakiwa hamfahamu isipokuwa tu mawakili wa serikali.
Shahidi akitoa Ushahidi bila mahakama kumuona, majaji hawamfahamu, mtuhumiwa atafanyaje effective cross examination? Shahidi asiyejulikana na Mahakama, haonekani kwa mtuhumiwa itatoaje uamuzi ambao hauhatarishi maslahi ya haki?
Waheshimiwa majaji kuruhusu Ushahidi wa namna hii itakuwa ni a mockery of justice and just adjudication of cases by the court, hakutakuwa na haki kabisa.
Waheshimiwa Majaji katika mazingira haya shahidi akiruhusiwa kutoa kinachoitwa Ushahidi wake:
Mahakama itajuaje demeanour of the witness?
Hii haitakuwa fair hearing, hakutakuwa na usawa mbele ya sheria, mtahakikishaje waheshimiwa majaji kuwa kutakuwa na usawa mbele ya sheria kama ambavyo Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya JMT inasema.
Tunapozungumzia usawa mbele ya Sheria hatuzungumzii kanuni zilizotungwa na Jaji Mkuu tu peke yake, tunazungumzia kanuni za kikatiba pamoja na Ibara ya 107A ambayo inaweka sharti kwamba Mahakama lazima itende haki sawa kwa wote.
Waheshimiwa majaji hili litawezaje kutekelezwa kama mtaruhusu mashahidi msiowajua na msiowaona kutoa Ushahidi? Waheshimiwa majaji nawaomba msije mkakubali kutumika kuharibu utendaji haki katika mahakama zetu, don’t ever allow.
Waheshimiwa majaji haya niliyoyasema ya misingi ya haki yamewekwa pia katika mikataba mbalimbali ambayo nchi yetu imeridhia.
Naomba niwape mifano, Ibara ya 2 , 7, 10 and 11 za Tangazo la Haki za Binadamu of UDHR 1948, Ibara ya 14(1) , 14(3) (e ) na 26 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kirai na Kisiasa wa Mwaka 1966 (ICCPR) zote zinazungumzia usawa mbele ya Sheria, ulinzi sawa mbele ya sheria.
Waheshimiwa majaji naomba kuwasomea Ibara ya 14(3)(e) of ICCPR inasisitiza kuhusu in full equality, mkiruhusu shahidi ambaye hamumjui, hamumfahamu, mimi simuoni na wala simfahamu, hiyo in full equality itatoka wapi?
Vilevile Ibara ya 3 na 7 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu, ibara ya 6(d) na 7(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rules of Procedure International Residual Criminal Procedure Mechanisms hizi zimeweka gold standard na best practices za umoja wa Mataifa hivyo mahakama zetu zinaweza zikazitumia hasa kanuni ya 75A, 75C, 86A na 86B.
Waheshimiwa Majaji hizi kanuni 4 ndio best standards za kulinda mashahidi, hivyo utaratibu huu upo sio kwamba umegunduliwa na mawakili wa serikali na hazina hii darkness tunayotaka kuletewa hapa (Lissu anaonyesha kizimba alipojificha shahidi wa leo)
Utaratibu huu hauwezi kuleta fair trial, mkiruhusu huu utaratibu unaotaka kuletwa hapa then we must forget about fair trial.
Sehemu ya 149
Waheshimiwa Majaji, naomba niende kwenye hoja ya tano;
Naomba kurejea kesi zifuatazo High hope international group Jiangsu native produce import and export cooporation limited vs JOC Textile (Tanzania Company Limited) Misc. Commercial Application No 48 of 2020, kesi ya Sheer Illusions Ltd vs Christina Ulawe Umiro Civil Appeal 114 of 2014.
Hizi kanuni zimechapishwa Julai 11, 2025 miezi mitatu kabla ya kesi hii. Swali ni je, kanuni hizi zinaweza kutumika katika kesi iliyoanza kabla hazijatungwa? Jibu ni Sheer Illusions kwenye ukurasa wa 11 wa hukumu hiyo kuwa haziwezi kutumika kwenye kesi yangu.
Waheshimiwa Majaji hoja yangu nyingine ni kwamba kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa Jinai ambacho ndio msingi wa Kanuni hizi.
Kifungu hiki kililetwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 07 ya 2018. Hii sheria inayoruhusu kuficha mashahidi haijawahi kuchapishwa kwenye gazeti la serikali.
Kifungu cha 14 cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria kinasema ili sheria ianze kutumika lazima iwe published kwenye gazeti.
Sheria yenyewe haisemi itaanza kutumika tarehe ngapi hivyo ilipaswa kuanza kutumika siku ilipotangazwa kwenye gazeti la serikali hadi muda huu niliposimama hapa sheria hii haijawahi kutangazwa kwenye gazeti la serikali.
Waheshimiwa majaji sheria ikitangazwa katika gazette la Serikali inachapishwa kwenye website ya Serikali, official website ya ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Rais Idara ya Utumishi, huku vilevile haipo.
Anaendelea Mhe. Lissu tena.
Waheshimiwa Majaji publication in the Government Gazette ni takwa la Sheria kuwa gazette lazima liwasilishwe Bungeni, halikuwa tabled Bungeni.
Sheria ikitangazwa katika Gazette la Serikali utakuta physical copies katika maktaba ya Mahakama kuu Dar es Salaam kwenye jengo hili, napo haipo.
Vilevile kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali vilevile haipo na huko.
Mahakama Kuu kitengo cha Biashara pia haipo kwenye Hansard za Bunge pia haipo, kwenye duka la Serikali Dodoma na Dar es Salaam pia haipo kwenye Sheria ya Huduma za Maktaba inasema Sheria ikiwa gazetted and published lazima kuwekwa Maktaba Kuu ya Taifa Dar es Salaam hapo Kisutu pia haipo, kuna Sheria nyingine inaitwa Publications (Compulsory Deposit) Act Cap. 294 ambayo inalazimishwa publication must be deposited central library Dar es Salaam.
Kwenye hiyo sheria kuna Publications (Compulsory Deposit) Order GN 61 of 1964 inayosema all publications must be deposited in the central library, haipo waheshimiwa majaji.
Waheshimiwa majaji nimezungumzia tabling bungeni naomba niwaelekeze kwenye kanuni ya 37(2) Kanuni za Kudumu za Bunge GN 56 of 15/01/2016. Kanuni ya 53(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge GN No. 626 of 2020 hivyo kuchapisha sheria kwenye gazette la serikali ni matakwa ya sheria na kusambaza kwenye hizo sehemu nilizozitaja ni takwa la kisheria, haijafanyika sasa katika kanuni hizi.
Uthibitisho wa kuwa sheria imechapishwa ni sheria yenyewe, mimi na Mawakili wangu wanaonisaidia wamelitafuta hilo gazeti nchi nzima halipo. Vijana wamezunguka kila kona ya nchi hii na kwenye hayo maofisi niliyosema hawajawahi kukutana na hiyo sheria. Haipo.
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja hapa ninayojaribu kusema ni kwamba kama hiyo sheria haijawa published kwenye gazeti and there is no proof anywhere na kama imetumika, imetumika kimakosa.
Sehemu ya 150
Anaendelea Mhe. Lissu
Hivyo naomba sheria hii kama Jaji Mtembwa aliitumia, naiomba Mahakama hii isiendelee kukosea, isiendelee kuitumia.
Waheshimiwa Majaji mkiangalia sheria namba 7 ya 2018 utaona imeandikwa kwenye header note kuwa sheria hii imetolewa kwenye gazeti maalum la Serikali la tarehe 15 Septemba 2018, waheshimiwa majaji huo ni uongo.
Uthibitisho kuwa ilichapishwa kwenye gazeti la serikali ni kulitoa gazeti lenyewe, proof sio what the law says, bali ni physical existence or electronic existence.
Nawaomba waheshimiwa majaji msiitumie hii sheria, msipoitumia maana yake mashahidi waje watoe Ushahidi hadharani, hii ya kufichaficha mashahidi gizani haitakuwepo kabisa na haitakiwi kabisa kuwepo.
Anasimama Wakili wa Serikali Nassoro Katuga yupo kama amechanganyikiwa au ametoka kubeba gunia la mchanga ni mdogo kama Pilton.
Amesimama akiwa amenywea sana na kusema,
Kwa hoja nyingi zilizoletwa tunaomba muda wa kujiandaa kujibu hoja nyingi sana ambazo mshtakiwa amezisema.
Tunaomba tarehe ambayo tutapangiwa kwaajili ya kuja kujibu.
Lissu hajapinga ila ameomba tarehe ya karibu zaidi wapewe.
Kesi imeahirishwa kwa muda usiojulikana hadi pale ambapo Mahakama itatoa Notisi ya siku ya kusikilizwa kwasababu notisi ya awali ilionyesha mwisho wa kusikiliza kesi hii ni leo Novemba 12, 2025.