Noti za Plastiki Kuchukua Nafasi ya Noti za Karatasi


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,383
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,383 280

Noti za plastiki zinavyoonekana Monday, March 08, 2010 1:16 AM
Kidogo kidogo noti za karatasi zinaanza kutoweka duniani na nafasi yake inachukuliwa na noti za plastiki, Kanada imekuwa nchi ya nane duniani kubadilisha pesa zake na kuanza kutumia noti za plastiki. Noti za karatasi kidogo kidogo zinaelekea kuwa historia na nafasi yake inachukuliwa na noti za plastiki ambazo hazipitishi maji hivyo hata ukizisahau kwenye nguo zako wakati wa kuzifua hazitapata madhara yoyote tofauti na noti za noti za karatasi ambazo huchanika kirahisi zinapolowa maji.

Kanada inakuwa nchi ya nane duniani kubadilisha noti zake na kuanza kutumia noti za plastiki. Kanada itaanza kuziondoa noti za karatasi kidogo kidogo kuanzia mwishoni mwa mwaka ujao.

Noti za plastiki zinatumia plastiki aina ya polymer biaxially-oriented polypropylene (BOPP) na zimeambatanishwa na vionjo vingine vya ulinzi ili kuzifanya noti hizo ziwe si rahisi kufojiwa.

Noti za plastiki hazichaniki wala kuharibika kirahisi hivyo kuziokoa pesa za serikali zinazotumika kuchapisha noti mpya kila baada ya muda.

Faida nyingine ya noti za plastiki ni kwamba hazibebi uchafu mwingi na bakteria kama zilivyo noti za karatasi. Mfano mzuri ni noti za dola ya Kimarekani asilimia kubwa ya noti hizo zina uchafu wa madawa ya kulevya kutokana na kutumiwa zaidi na wauzaji wa madawa ya kulevya.

Australia ndio iliyokuwa nchi ya kwanza kutumia noti za plastiki. Ilianza kutumia noti hizo tangia mwaka 1992.

Nchi zingine zinazotumia noti za plastiki ni Bermuda, Brunei, New Zealand, Papua New Guinea, Romania na Vietnam.
 

Forum statistics

Threads 1,251,889
Members 481,937
Posts 29,789,360