Nombeni mnishauri nifanyeje

Nombeni mnishauri nifanyeje

Mi naona tatizo lipo hapo kwa watoto wa marehemu ndipo bifu lilipoanzia kama vipi nifafanulie kauli ya mama yako anaposema unawatesa watoto kivipi? Unajua mamtu ya bongo inafikili ni wajibu wako kulea mtoto wa mwenzio tena kwa kuprovide kila kitu kutoka kwako as if alikuzalia yeye.Nakusifu kwa kuchukua jukumu la kutoa msaada wa kuwalea watoto wa marehemu ambao mara nyingi ndo chanzo cha kuonekana una roho mbaya dia.

Inaonyesa hujaelewa ndugu yangu, mama yangu hasemi ninawatesa watoto wa ndugu yangu, ila mimi nkienda Home wakati wa weekend kusalimia unaona mama anavyowatenga wanangu mm ,mmpk watoto wanasema kuwa bibi sisi hatupendi. Nina maana gani tukifika pale anawashangilia zaidi wale wa marehemu na kuwabeba lakini wangu mm hafanyi hivyo, kwa hiyo watoto wangu wameona hilo wakalalamika.
 
Daa.. Kweli dunia haiko fair! Pole sana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Dada Ameline kitabu hichi biblia kitabu cha Maombolezo 3:31-33, nitakipata wapi?Maana kwenye shida ya kumtafuta Mungu haijalishi dini, kinachotakiwa ni amani ndani ya moyo.
Pia Yasintha nashukuru kwa ushauri wako, Ila kusema kweli nampenda sana Mama yangu hata yeye anajua hilo, ndiyo maana nataka nikapate ushauri kwa Baba , nisikie anasemaje, halafu nitarudi tena kwake kuongea naye anieleze tatizo ni nn, au nimemchukiza nn, aniambie ili nimuombe msamaha.
Ndugu aliyepo ni huyo mdogo wangu na hana njaa, yeye na mumewe wana uwezo sana, kiasi hata nikikwama huwa wananisaidia. Pia nataka nikazungumze naye leo nimpe mkasa wote. kesho nitakupa feedback, kwamba tumeamua nn mm na ndugu yangu.
 
Aiseee pole sana mdada kwa kimbembe hicho kilichokukuta,mi kwa ushauri naona kama unaweza jitegemea na una namna ya kupata pesa ni jambo la busara kutoka hapo nyumbani na kuangalia mambo yako mengine,huku ukisubiri mwelekeo wa mama yako huyo.Ikiwa atakufata na huko ujue ana lake jambo,ila kwa sasa mhamie kwake ufanye mambo yako ila usinoyeshe kumchukia wala usiweke bifu naye kwani umama wake kwako bado upo palepale.
 
wazazi wengine jamani,wana tamaa tu.mama yako ana nyumba 5 na bado anataka kukutoa hapo unapoishi.hajui ipo siku hizo nguvu zake atakuwa hana,na hizo mali zitakuwa nothing kwake.atakaowahitaji ni nyijyi na sio mali.inasikitisha
 
Binafsi yangu huwa naona hasara ni roho tu pesa makaratasi...kama ulitoka kwenye matatizo ya ndoa na ukaamua kuanza moja, basi ongea na mungu wako kama alikupatia hicho ulichopata ukajenga atakupa kikubwa zaidi, inauma na inaumiza sana nguvu zako kupotea ila kuliko kuanza kuvutana na mama yako bora uwaite ndugu uwaambie kilichotokea na umwachie hizo nyumba ndugu wakiwa mashahidi....alafu utakuja kuniambia kama jasho la mtu linaliwa...
 
hakuna kuhama wala nini jenga ukuta.

Tafuta kiwanja sehemu nyingine ujenge hizo ndo changamoto za kujenga kwenu.......

Ila komaa hakuna kumuachia....
 
wazazi wengine jamani,wana tamaa tu.mama yako ana nyumba 5 na bado anataka kukutoa hapo unapoishi.hajui ipo siku hizo nguvu zake atakuwa hana,na hizo mali zitakuwa nothing kwake.atakaowahitaji ni nyijyi na sio mali.inasikitisha
Ni kweli ameanza kupoteza nguvu, ndiyo maana dada mtoto wa mama mkubwa kaniambia nimuachie, iko siku atanitafuta.naona uzee unamsumbua, Anyway i don't know!!!
 
Binafsi yangu huwa naona hasara ni roho tu pesa makaratasi...kama ulitoka kwenye matatizo ya ndoa na ukaamua kuanza moja, basi ongea na mungu wako kama alikupatia hicho ulichopata ukajenga atakupa kikubwa zaidi, inauma na inaumiza sana nguvu zako kupotea ila kuliko kuanza kuvutana na mama yako bora uwaite ndugu uwaambie kilichotokea na umwachie hizo nyumba ndugu wakiwa mashahidi....alafu utakuja kuniambia kama jasho la mtu linaliwa...
Kwanza mpk sasa siamini macho yangu kama kitu kama hicho kingeweza kunitokea kwenye maisha yangu, kwa sababu nilikuwa nina imani kuwa wazazi wangu wapo watanisupport , na ndiyo maana niliweza kuondoka kwa mume nikaanza moja kwa kujua wapo wa kunisaidia. Ila jumamosi naenda kuongea na Baba anipe ushauri nifanyeje, lakini pia nahofia naweza kuwa chanzo cha ugomvi wao.
 
Mdogo wangu/Dada yangu,kwanza anza kwa maombi,nenda kwa waombezi unaowaamini,komboa ardhi hapo unapoishi,TUBU NA WEWE MWENYEWE DHAMBI ZOTE UNAZOZIJUA UMEFANYA(MAOMBI YA TOBA)THEN BAADA YA HAPO ITAKUWA RAHISI KUSOLVE YOYOTE YATAKOYOKUJA,TEMBEA MWAMBIE MUNGU AKUFANYIE WEPESI,AKUONYESHE UFANYE NINI,WEWE MWENYEWE HUTAWEZA,MAANA HAPO UMEANDIKA KUHUSU MTOTO WA MAMA MKUBWA ,BABA MKUBWA,MMMMHH HAPANA ,KWANZA MAOMBI.UBARIKIWE,
 
Baba hajajua kwa sasa, ndiyo nataka nikamwelezee nisikie atasemaje, lakini baba yngu ananipenda sana , najua akijua hilo panaweza pakachimbika pale home, na mm sitaki kuwa chanzo cha ugomvi wao.

no talk to him au jitolee kuwa kondoo wa kafara, which i think its not good...
 
nakivona = nimekiona, ni sawa na kumwita mwanao shida, tabu
Nakijwa = nimefukuzwa, kama umemwita mwanao jina hilo ni kwamba atafukuzwa milele kwenye maisha yeke
Nakiete= nimekileta
Nanzia= Mtoto aliyezaliwa njiani,

Sasa dada yangu jina lako tu linajieleza kuwa wewe kwenye maisha yako ni shida kwenda mbele, nakuomba badilisha jina au likatae hilo jina siyo zuri kwako na kwa maisha yako. linamaanisha UTAKIONA.

Nikirudi kwenye mada naomba usimkasirikie mama yako, mpende kuliko ulivyokuwa unampenda, mjali, iko siku atakuja kukuita na kukukabidhi mali zako, kwa sababu nguvu zitamwisha na atakuwa hana wa kumsaidia isipokuwa wewe na huyo nduguyo. Na usiache kusali na kufunga Mungu atashusha Rehma zake mtaelewana kama mwanzo na hatobagua tena watoto wako.

INGAWA KUWA MWANGALIFU SANA NA MAMA YAKO SINA IMANI NAYE.
 
Kwanza mpk sasa siamini macho yangu kama kitu kama hicho kingeweza kunitokea kwenye maisha yangu, kwa sababu nilikuwa nina imani kuwa wazazi wangu wapo watanisupport , na ndiyo maana niliweza kuondoka kwa mume nikaanza moja kwa kujua wapo wa kunisaidia. Ila jumamosi naenda kuongea na Baba anipe ushauri nifanyeje, lakini pia nahofia naweza kuwa chanzo cha ugomvi wao.

wala hilo lisikutishe kwan wewe ni mtoto wafamilia si mtu baki...nenda kaongee naye umsikie anasemaje kwani yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho..
kila la kheri...
 
Pole sana dada,ila usimchukie mama yako tena ondoa hayo mawazo ya kujiua mana bado hujaongea nae ukajua tatizo ni nini pengine ni uzee tu au mastress mengine yanamfanya akili yake inashindwa kufilter mambo

Ushauri wangu mwite huyo mdogo wako,baba yako kama yupo halafu muongee kinagaubaga I hope mtapata suluhu
 
daa pole sana wangu ujue mi nilijua zile movie sometimes wana acts pasipo uhalisia,duu kumbe kweli yanatokea?sasa bi dada mi nadhani onana na mzee tena na muambie kilichotokea na umsikilize yeye kama mwenye kiwanja atakuambiaje,pia usichoke kumuomba mungu,
 
mweh mweh mweh!!!!!
Nilizani familia yangu tu matatizo. Kumbe tupo wengi jamani.

Ugombanishaji wa kifamilia ndio unaanzaga hivo, dada we.
Ulikuja kuambiwa na mtoto wa baba ako mkubwa.
Nawe ukaenda kuuliza kama ni kweli.
Na mama akajibu ni kweli.

Jiulize mazungumzo yao yalianzia na nini?
Na kwanini mama hakuja kukuambia wewe mwenyewe?

Mie nafikiri hao watoto wa baba ako mkubwa wanaona umependelewa, wewe kukaa hapo ikiwa wao walifukuzwa. Na wanataka na wewe pia ufukuzwe kama wao.

Nafikiri walienda kumlaumu au kulalamika ama kumuliza mama mbona wewe hakufukuzi? ikiwa wengine aliwafukuza!!!
Ndio hapo mama ako akajibu, "nitamtoa na yeye pia nipangishe", maana kakaa muda mrefu sasa.

Umeona picha?

Ushauri wangu, fanya kama my brother.
Mwambie mama yako "hapa sitoki", nitakaa hapa hapa.
Ukitaka nitoke njoo niue mimi na wanangu.

Na waambie jamaa zako wote utakaa hapo hapo, mali za baba ako na mama ako alie kuzaa.

Utaona mama ako wala hatokufukuza, atawaambia nyie si mumemsikia alivo jibu? hatoki, mimi nikamue mwanangu ili iweje? akae tu.

Mie naona hao ndugu zako, jamaa zako wanakuonea wivu umependwa kupewa kiwanja ujenge. Hizo mali za baba ako na mama ako mzazi, wao wanataka kujingiza kwa vile wamekulea au mama ako aliwalea? kha...

sema hautoki, fanya lolote lile mama
 
Wewe dada white muogope Mungu kabisa tena usithubutu siku nyingine usihukumu usije ukahukumiwa mwnyw acha kabisa Mungu ndio anajua walio wake,amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa ukienda kumtafuta Mungu kanisani utamuona ukienda kanisani kwa mchungaji na ukaweka tegemeo lako lote kwake utayaona yaliyo ya kibinadamu,dada @nackvyona endelea kumtegemea Mungu yy ndo anaijua shida yako na msaada pekee utaupata kwake.

nampenda Mungu ila siamini kila mchungaji sijui umenielewa mpendwa katika bwana?
 
Last edited by a moderator:
Habari wana JF, nimejiunga na hii Forums siku si nyingi, ila nimependa sana comment zenu , na ushauri mnaotoa kwa watu mbali mbali pale wanapoomba msaada wa mawazo, nami nikavutiwa nikaona bora nijiunge nanyi labda nitapata mawazo mazuri ambayo yatanifanya niendelee kuishi.

Mimi ni mtoto wa pili katika familia yetu, tulizaliwa wasichana wote 4, tulilelewa vizuri na kusomeshwa pia, bahati nzuri tulipata kazi na Mungu akabariki tuliolewa wote, ila katika maisha Mungu huwa na mipango yake, ndugu zangu wawili wakafariki dunia na kutuachia watoto ambao tunawalea mm na mdogo wangu.Katika kuishi huko mm ndoa ikanishinda ikabidi niachike, nikaenda kujenga kwenye kiwanja cha wazazi wangu, nashukuru Mungu maisha yakaanza kuwa mazuri, nikawa naweza kulea watoto wangu wawili pamoja na wandugu yangu wawili umla nilikuwa na watoto 4.
Katika kuishi huko nikaweza kuongeza nyumba ya pili ambayo nimepangisha napata pesa za kusomeshea watoto. Lakini linalonitatiza ni Mama yangu Mazazi simuelewi kabisa, kwamba anataka mm nitafute sehemu nihame pale kwa sababu anahitaji hizo nyumba kupangisha , anasema nimeshakaa sana inatosha, sasa nikamuuliza kuwa mm si ndiyo nimejibana nikajenga, ananiambia nitoe tofari zangu.
Imefikia steg ya kubagua hata wanangu, kwa kweli inaniuma sana, kwa sababu yeye ni mama yangu, anatakiwa aniunge mkono aslimia 100, lakini yeye ndiyo anakuwa kikwazo kwangu , sifahamu ni kwa nn, na kama nimemkosea kwa nn asiniambie?, najiuliza nimemchukiza nn, sipati jibu.Kama matumizi nampa, au anaona hazitoshi?

Sipendi kuandika hapa , ila imenibidi, naona sina faida ya kuendelea kuishi, maana mume kanishinda
na ninayemtegemea kunisupport kanigeuka, naona bora nife mm na wanangu nimuachie hizo nyumba.

naombeni ushauri nifanyeje?
Some mothers are controlling and have narcisstic personality disorder.she can't control you anachoamua kukutenda .kuna wamama wanaua watoto Wao sometimes.Ignore her
 
NI mama yangu kabisaaaaaa, na ni msomi mzuri na ana nyumba Tano hapa Dar, na kapangisha zote, Lakini sijui ni nn kwa kweli, niombeeni, maana nimeanza kufunga na kusali ili Mungu anionyeshe ni nn kipo ndani yake.

She wants to control you
 
Habari wana JF, nimejiunga na hii Forums siku si nyingi, ila nimependa sana comment zenu , na ushauri mnaotoa kwa watu mbali mbali pale wanapoomba msaada wa mawazo, nami nikavutiwa nikaona bora nijiunge nanyi labda nitapata mawazo mazuri ambayo yatanifanya niendelee kuishi.

Mimi ni mtoto wa pili katika familia yetu, tulizaliwa wasichana wote 4, tulilelewa vizuri na kusomeshwa pia, bahati nzuri tulipata kazi na Mungu akabariki tuliolewa wote, ila katika maisha Mungu huwa na mipango yake, ndugu zangu wawili wakafariki dunia na kutuachia watoto ambao tunawalea mm na mdogo wangu.Katika kuishi huko mm ndoa ikanishinda ikabidi niachike, nikaenda kujenga kwenye kiwanja cha wazazi wangu, nashukuru Mungu maisha yakaanza kuwa mazuri, nikawa naweza kulea watoto wangu wawili pamoja na wandugu yangu wawili umla nilikuwa na watoto 4.
Katika kuishi huko nikaweza kuongeza nyumba ya pili ambayo nimepangisha napata pesa za kusomeshea watoto. Lakini linalonitatiza ni Mama yangu Mazazi simuelewi kabisa, kwamba anataka mm nitafute sehemu nihame pale kwa sababu anahitaji hizo nyumba kupangisha , anasema nimeshakaa sana inatosha, sasa nikamuuliza kuwa mm si ndiyo nimejibana nikajenga, ananiambia nitoe tofari zangu.
Imefikia steg ya kubagua hata wanangu, kwa kweli inaniuma sana, kwa sababu yeye ni mama yangu, anatakiwa aniunge mkono aslimia 100, lakini yeye ndiyo anakuwa kikwazo kwangu , sifahamu ni kwa nn, na kama nimemkosea kwa nn asiniambie?, najiuliza nimemchukiza nn, sipati jibu.Kama matumizi nampa, au anaona hazitoshi?

Sipendi kuandika hapa , ila imenibidi, naona sina faida ya kuendelea kuishi, maana mume kanishinda
na ninayemtegemea kunisupport kanigeuka, naona bora nife mm na wanangu nimuachie hizo nyumba.

naombeni ushauri nifanyeje?

Si kwamba nakulaumu ila napenda niseme kwa faida ya wengine,
kujenga ktk kiwanja cha wazazi si kosa ila ifahamike nyumba hio lazma ni ya familia na si yako kwani kiwanja ni chafamilia vinginevyo uwe umezaliwa pekeyako ndani ya familia hiyo.Kuhusu mgongano wako na mama yako cha msingi mkumbuke Mungu kwani hayo ni mapito ktk maisha na siku moja yataisha, isitoshe mama ameshakua mzee cha msingi usimchukie kwani ni mama yako.
 
Back
Top Bottom