dada white
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 1,228
- 515
Teh teh tehUmenikumbusha yule mchungaji anaemtaka binti aliyekua kama family friend wao!!
yupi huyo ndugu?
Teh teh tehUmenikumbusha yule mchungaji anaemtaka binti aliyekua kama family friend wao!!
huyo ana roho ya kauzibe hapendi kuona wenzie wakifanikiwa ila ye kapitiliza anawafanyia ubinafsi hadi watoto wa kuzaa kweli duniani kuna mambo.Mama yeye ndiye aliyeniombe kujenga vyumba viwili kwa baba na kumpa mkasa mzima kuhusu ndoa yangu, kwa hiyo baba ndiyo akaja kwangu kuangalia jinsi ninavyoishi na watoto akanionea huruma na kuniambia jenga nyumba kubwa, uishi na wanao na usiogope kwamba kuna mtu atakusumbua. Sasa nashangaa mama ndiyo kikwazo.
Nimeongea na Dada yangu mtoto wa mama yangu mkubwa alitulea na mama alimsomesha, nimemueleza yote, alichonijibu kuwa ndivyo mama yako alivyo, hata mm alinifukuza pale home, sema nilikuwa sitaki kuwaambia mtanikatalia, hakuishia hapo , kanimbia kama huamini muulize kaka yako mtoto wa baba yako mkubwa ilikuwaje akaondoka pale home? kumbe naye alifukuzwa na mama, nimebaki nimeshikwa na butwaa.
Mimi nilikuwa najua waliondoka kwa uamuzi wao wenyewe.
kubomoa nyumba sitabomoa, wala sitashindana naye, nataka nikaongee naye anipe muda, ili nimalize chuo, maana nasoma kwa sasa nipo mwaka wa pili, nikimaliza nijenge hata vyumba viwili kwingine, nimuachie zile nyumba ale kodi yeye.kwa kuwa Mungu anajua lile ni jasho langu haliwezi potea.Utulivu na busara zinaitajika hata kama mama anasema hayo bado atabaki kuwa mama kuna kitu ambacho kipo either mama ameambiwa ama amechukizwa nacho mpaka amehanua hayo zungumza nae kwa utaratibu ikishindikana ita ndugu wa familia muyamalize kuondoka au kubomoa hiyo nyumba siyo tatizo.
Mimi nilienda kuomba kujenga kwenye kiwanja hicho , ni baada ya kushindwa maisha na vituko vya mume wangu, nikaenda kuomba kujenga vyumba viwili ili nitafute kwangu, baba akaja kunisalimia , akaniambia nijenge nyumba kubwa nikae maana hamna mtu atakayekuja kukusumbua,basi nikaona kama mwenye kiwanja katoa go ahed kwa nn nisijenge nkajenga . Baadae nikapata pesa nikaamua kuweka kitega uchumi ili niweze kuishi vizuri nisije nikamanga manga na wanaume tena nikapata magonjwa nikawaacha wanangu. Sasa nilianza kusikia kwa ndugu watoto wa mama mkubwa kuwa mama anasema hayo nikawa siamini, juzi nimeyasikia kwa kaka mtoto wa baba mkubwa, kuwa anasema haoni faida ya mm kuendelea kukaa pale, ikabidi nimfuate ndiyo akanipa live kuwa kama ni nyumba basi nitoe tofari zangu. kwa kweli nimechoka hoiii, nashindwa la kufanya , sipati usingizi, naona dunia imenisonga, pa kushika sina nifanyeje?
dadaangu pamoja na kuambiwa na baba yako ulitakiwa uishie kwenye vile vyumba viwili ili utafuta maisha ukishapata utafute kwako ambako hakuna kelele, mm ninaeandika hapa nilikuwa na mume ila tumeachana yeye aliuza asset za familia viwanja pamoja na nyumba hakunihusisha katika maamuzi, any way mie sikwenda kwetu nilipanga chumba kimoja na sebule nikaanza kutafuta maisha yangu, namshukuru mungu sasa hivi nina viwanja viwili na nyumba nimeshamaliza chini natafuta hela ya kununua bati na watoto nawalea mimi. my dear think outside the box.
Nenda kaongee na baba yako na ujue kiwanja kilikuwa ni cha nani maana kama bado baba yako yupo basi hakuna haja ya kulumbana na mama yako wala kuumia,usichukue uamuzi wa haraka katika hili kwani katika maisha tunayoishi kila siku mambo kama haya hutokea na wenzako wana makubwa kuliko ya kwako.Mimi nilienda kuomba kujenga kwenye kiwanja hicho , ni baada ya kushindwa maisha na vituko vya mume wangu, nikaenda kuomba kujenga vyumba viwili ili nitafute kwangu, baba akaja kunisalimia , akaniambia nijenge nyumba kubwa nikae maana hamna mtu atakayekuja kukusumbua,basi nikaona kama mwenye kiwanja katoa go ahed kwa nn nisijenge nkajenga . Baadae nikapata pesa nikaamua kuweka kitega uchumi ili niweze kuishi vizuri nisije nikamanga manga na wanaume tena nikapata magonjwa nikawaacha wanangu. Sasa nilianza kusikia kwa ndugu watoto wa mama mkubwa kuwa mama anasema hayo nikawa siamini, juzi nimeyasikia kwa kaka mtoto wa baba mkubwa, kuwa anasema haoni faida ya mm kuendelea kukaa pale, ikabidi nimfuate ndiyo akanipa live kuwa kama ni nyumba basi nitoe tofari zangu. kwa kweli nimechoka hoiii, nashindwa la kufanya , sipati usingizi, naona dunia imenisonga, pa kushika sina nifanyeje?
Naomba nikwambie kitu watalamu wa mambo wanasema kuwa tatizo halikimbiwa mpendwa hata siku moja kwa mtazamo wangu plan ya kujenga nyumba ni outcome ya mgogoro uliokuwepo sasa na tambua hata ukijenga nyumba nyingine pale utaondoka kana kwamba kumsusia hivyo basi usiwe na zana ukimwaga mboga basi na wewe umwage ugali chukulia hii ni kama changamoto endelea kuishi kwa amani lkn umeshajifunza kitu timiza malengo yako taratibu mpaka yatakapotimi mimi nina amini yatakwisha na mtakuwa kama awali mambo hayo yapo hapa Duniani na wewe si wakwanza.kubomoa nyumba sitabomoa, wala sitashindana naye, nataka nikaongee naye anipe muda, ili nimalize chuo, maana nasoma kwa sasa nipo mwaka wa pili, nikimaliza nijenge hata vyumba viwili kwingine, nimuachie zile nyumba ale kodi yeye.kwa kuwa Mungu anajua lile ni jasho langu haliwezi potea.
m
Baba hajajua kwa sasa, ndiyo nataka nikamwelezee nisikie atasemaje, lakini baba yngu ananipenda sana , najua akijua hilo panaweza pakachimbika pale home, na mm sitaki kuwa chanzo cha ugomvi wao.dada kwani kiwanja ni cha nani?kama cha baba yako basi mshirikishe yeye, na mueleze kwa uwaz mama yako anachotaka kufanya. na kama inawezekana baba yako athibitishe kabisa kwa maandishi kuwa amekupa hicho kiwanja. otherwise mkalishe mama na mzee na wanandugu wengine mjadili hili swala.
Ni kweli kabisa mama hajibishwi, unaweza pata laana, lakini linalonichanganya mm ni kuwa tuko wawili, na ndugu yangu ana mali kishenzi kiasi mm mwenyewe huwa ananisaidia pindi ninapoishiwa. sasa mama tatizo lake ni nn? kama maisha hana mabaya , ni mtu wa East Africa, kastaafu kapata milioni 130. sasa nn tatizo sielewei, au ndiyo mapepo yamwemwingia?Pole sana. Piga goti umwombe Mungu amalize hili tatizo na muishi kwa amani na Mam. Funga na kuomba bila kuchoka mana kumjibisha mama nako c vema.
Ingekuwa ni hivyo kaka ningekuwa sina shida, Tatizo ni kwamba nimejenga zote kwenye kiwanja kimoja. sasa zingekuwa zinabebeka ningebeba, lakini siwezi, niombeeni ili alegeze moyo.Hili kosa hufanywa na wengi sana hapa kwa dunia.... Kwa mujibu wa ufahamu wangu, MWENYE KIWANJA NDO MWENYE NYUMBA. Jipange upya, vinginevyo utapoteza muda na lasilimali nyingi katika hilo. We hamia kwenye nyumba uliyopangisha...
Ndugu yangu, watoto ni kwa mama, siku zote, baba wa watoto hao wapo kwa kweli wao wananisaidia kulipia ada, ila mambo mengine nafanya mm. na ndugu yangu yeye anauwezo mkubwa tu, so yeye haitaji kitu kutoka kwa hao mashemeji.Na baba wa hao watoto wameridhia kukaa nasi kwa sababu ya mama zao kufa.Pole dada ! Umesema dada zako wawili walifariki mkagawana watoto wao na mdogo wako! Kwani hao dada zako walizaa hao watoto na nani? Baba za hao watoto wako wapi? Nareserve comments zangu hadi utakaponijibu hayo maswali.
Asante , asante sana kwa kunitia moyo, nimeshapanga kwenda kumuona baba siku ya jumamosi, pale home, nitamwambia kila kitu ili anishauri, Baba yangu ni mpole sana na anajua ni jinsi gani nilivyoumia baada ya kupata matatizo na mume wangu, alinisapport kwa kila hali.Nenda kaongee na baba yako na ujue kiwanja kilikuwa ni cha nani maana kama bado baba yako yupo basi hakuna haja ya kulumbana na mama yako wala kuumia,usichukue uamuzi wa haraka katika hili kwani katika maisha tunayoishi kila siku mambo kama haya hutokea na wenzako wana makubwa kuliko ya kwako.
Tulia na mweke Mungu mbele maana ukiifanya hasira ikuongoze utaharibu kila kitu.
Pole sana.
Wewe dada white muogope Mungu kabisa tena usithubutu siku nyingine usihukumu usije ukahukumiwa mwnyw acha kabisa Mungu ndio anajua walio wake,amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa ukienda kumtafuta Mungu kanisani utamuona ukienda kanisani kwa mchungaji na ukaweka tegemeo lako lote kwake utayaona yaliyo ya kibinadamu,dada @nackvyona endelea kumtegemea Mungu yy ndo anaijua shida yako na msaada pekee utaupata kwake.Hayo makanisa yenyewe laana tupu hata wachungaji wenyewe laana mshauri lingine.