Nombeni mnishauri nifanyeje

Nombeni mnishauri nifanyeje

nackyvona

Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
19
Reaction score
3
Habari wana JF, nimejiunga na hii Forums siku si nyingi, ila nimependa sana comment zenu , na ushauri mnaotoa kwa watu mbali mbali pale wanapoomba msaada wa mawazo, nami nikavutiwa nikaona bora nijiunge nanyi labda nitapata mawazo mazuri ambayo yatanifanya niendelee kuishi.

Mimi ni mtoto wa pili katika familia yetu, tulizaliwa wasichana wote 4, tulilelewa vizuri na kusomeshwa pia, bahati nzuri tulipata kazi na Mungu akabariki tuliolewa wote, ila katika maisha Mungu huwa na mipango yake, ndugu zangu wawili wakafariki dunia na kutuachia watoto ambao tunawalea mm na mdogo wangu.Katika kuishi huko mm ndoa ikanishinda ikabidi niachike, nikaenda kujenga kwenye kiwanja cha wazazi wangu, nashukuru Mungu maisha yakaanza kuwa mazuri, nikawa naweza kulea watoto wangu wawili pamoja na wandugu yangu wawili umla nilikuwa na watoto 4.
Katika kuishi huko nikaweza kuongeza nyumba ya pili ambayo nimepangisha napata pesa za kusomeshea watoto. Lakini linalonitatiza ni Mama yangu Mazazi simuelewi kabisa, kwamba anataka mm nitafute sehemu nihame pale kwa sababu anahitaji hizo nyumba kupangisha , anasema nimeshakaa sana inatosha, sasa nikamuuliza kuwa mm si ndiyo nimejibana nikajenga, ananiambia nitoe tofari zangu.
Imefikia steg ya kubagua hata wanangu, kwa kweli inaniuma sana, kwa sababu yeye ni mama yangu, anatakiwa aniunge mkono aslimia 100, lakini yeye ndiyo anakuwa kikwazo kwangu , sifahamu ni kwa nn, na kama nimemkosea kwa nn asiniambie?, najiuliza nimemchukiza nn, sipati jibu.Kama matumizi nampa, au anaona hazitoshi?

Sipendi kuandika hapa , ila imenibidi, naona sina faida ya kuendelea kuishi, maana mume kanishinda
na ninayemtegemea kunisupport kanigeuka, naona bora nife mm na wanangu nimuachie hizo nyumba.

naombeni ushauri nifanyeje?
 
pole sana mdada, ni kwa nini ulienda kujenga nyumbani kwenu? kama ulikuwa na uwezo wa kujenga nyumba dadaangu kwa nini hukununua kiwanja chako ujenge? naandika huku naumia sana utafikiri ni mm ndo nafanyiwa hivyo. kwa upeo wangu unaweza kujenga kwenye kiwanja cha nyumbani iwapo umepewa urithi au ukaamua kujengea wazazi as a gift. sijui mapatano yako na wazazi hadi kuanza kujenga nyumba ni kuita ya kwako kwenye kiwanja cha familia labda utwambie tujue pa kuanzia kutoa ushauri.
 
Mimi nilienda kuomba kujenga kwenye kiwanja hicho , ni baada ya kushindwa maisha na vituko vya mume wangu, nikaenda kuomba kujenga vyumba viwili ili nitafute kwangu, baba akaja kunisalimia , akaniambia nijenge nyumba kubwa nikae maana hamna mtu atakayekuja kukusumbua,basi nikaona kama mwenye kiwanja katoa go ahed kwa nn nisijenge nkajenga . Baadae nikapata pesa nikaamua kuweka kitega uchumi ili niweze kuishi vizuri nisije nikamanga manga na wanaume tena nikapata magonjwa nikawaacha wanangu. Sasa nilianza kusikia kwa ndugu watoto wa mama mkubwa kuwa mama anasema hayo nikawa siamini, juzi nimeyasikia kwa kaka mtoto wa baba mkubwa, kuwa anasema haoni faida ya mm kuendelea kukaa pale, ikabidi nimfuate ndiyo akanipa live kuwa kama ni nyumba basi nitoe tofari zangu. kwa kweli nimechoka hoiii, nashindwa la kufanya , sipati usingizi, naona dunia imenisonga, pa kushika sina nifanyeje?
 
Pole sana mamito. Mimi nina swali kabla hata sijatoa ushauri. Alietoa go ahead ni baba, je mama alishirikishwa kwenye hayo maamuzi? na je baba anasemaje sasa hivi kuhusu hilo suala. Na mama anavyosema utoe matofali manake ni ubomoe right! ukishabomoa atapangisha nini?
 
Inawezekana kuna laana juu yako au kwa Mama yako. Utafute kanisa wanalotoa huduma za maombezi ukaombewe.
 
dadaangu pamoja na kuambiwa na baba yako ulitakiwa uishie kwenye vile vyumba viwili ili utafuta maisha ukishapata utafute kwako ambako hakuna kelele, mm ninaeandika hapa nilikuwa na mume ila tumeachana yeye aliuza asset za familia viwanja pamoja na nyumba hakunihusisha katika maamuzi, any way mie sikwenda kwetu nilipanga chumba kimoja na sebule nikaanza kutafuta maisha yangu, namshukuru mungu sasa hivi nina viwanja viwili na nyumba nimeshamaliza chini natafuta hela ya kununua bati na watoto nawalea mimi. my dear think outside the box.
 
Pole sana mamito. Mimi nina swali kabla hata sijatoa ushauri. Alietoa go ahead ni baba, je mama alishirikishwa kwenye hayo maamuzi? na je baba anasemaje sasa hivi kuhusu hilo suala. Na mama anavyosema utoe matofali manake ni ubomoe right! ukishabomoa atapangisha nini?
Mama yeye ndiye aliyeniombe kujenga vyumba viwili kwa baba na kumpa mkasa mzima kuhusu ndoa yangu, kwa hiyo baba ndiyo akaja kwangu kuangalia jinsi ninavyoishi na watoto akanionea huruma na kuniambia jenga nyumba kubwa, uishi na wanao na usiogope kwamba kuna mtu atakusumbua. Sasa nashangaa mama ndiyo kikwazo.
Nimeongea na Dada yangu mtoto wa mama yangu mkubwa alitulea na mama alimsomesha, nimemueleza yote, alichonijibu kuwa ndivyo mama yako alivyo, hata mm alinifukuza pale home, sema nilikuwa sitaki kuwaambia mtanikatalia, hakuishia hapo , kanimbia kama huamini muulize kaka yako mtoto wa baba yako mkubwa ilikuwaje akaondoka pale home? kumbe naye alifukuzwa na mama, nimebaki nimeshikwa na butwaa.
Mimi nilikuwa najua waliondoka kwa uamuzi wao wenyewe.
 
Inawezekana kuna laana juu yako au kwa Mama yako. Utafute kanisa wanalotoa huduma za maombezi ukaombewe.
Asante sanaaaaaaaaa , Hata mm nimewaza hilo kuwa haiwezekani akawa na roho hiyo, ni lazima kuna roho ya kishetani ndani yake, nashukuru sana kwa ushauri. Nimepata faraja.
 
Au huyo siyo mama yako mzazi umuulize vizuri.
NI mama yangu kabisaaaaaa, na ni msomi mzuri na ana nyumba Tano hapa Dar, na kapangisha zote, Lakini sijui ni nn kwa kweli, niombeeni, maana nimeanza kufunga na kusali ili Mungu anionyeshe ni nn kipo ndani yake.
 
ukisikia nyoka anakula mkia wake ndo haya!mbona upendo umepoa hivi yaani hata kwa mama na mwana!!!!!!
 
Inawezekana kuna laana juu yako au kwa Mama yako. Utafute kanisa wanalotoa huduma za maombezi ukaombewe.

Hayo makanisa yenyewe laana tupu hata wachungaji wenyewe laana mshauri lingine.
 
Utulivu na busara zinaitajika hata kama mama anasema hayo bado atabaki kuwa mama kuna kitu ambacho kipo either mama ameambiwa ama amechukizwa nacho mpaka amehanua hayo zungumza nae kwa utaratibu ikishindikana ita ndugu wa familia muyamalize kuondoka au kubomoa hiyo nyumba siyo tatizo.
 
Dah, pole sana mamitho! Hii mada ni sensitive sana! Binafsi nitarudi baadae kidogo, kwasasa pole tu!
 
Pole sana. Piga goti umwombe Mungu amalize hili tatizo na muishi kwa amani na Mam. Funga na kuomba bila kuchoka mana kumjibisha mama nako c vema.
 
Dunia hii bana. Pole dadaa'angu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
bidii uliyokua nayo hadi kufika hapo ulipofikia naomba uiendeleze na ujipange upya utafute kiwanja kingine ujenge,maana huwezi kung'ang'ania kwenye kiwanja cha familia hususan mama kashakupa makavu live,cha msingi muombe akupe muda(ikiwezekana mkae kikao cha familia)ili utafute mwelekeo.Dah hata siamini kama huyo ni mama yako mzazi pole sana na jipe moyo kwani Mungu wetu ni mwema utafanikiwa tu.
 
Pole shosti,naelewa kua unawakati mgumu sana lakini Mama ni mama tuu piga moyo konde mpishe bila ushindani as long as unayo nyengine muachie hiyo kwani nyumba kubwa iko kwa mungu hapa tunapita tuu,najua kua sio rahisi lakini muombe mungu kwa sana na utazidi kufanikiwa na utapata nyengine bora kuliko hiyo,na vile vile muheshimu kama kawaida kilio chako chote mtupie mungu atakusaidia...
 
Mi naona tatizo lipo hapo kwa watoto wa marehemu ndipo bifu lilipoanzia kama vipi nifafanulie kauli ya mama yako anaposema unawatesa watoto kivipi? Unajua mamtu ya bongo inafikili ni wajibu wako kulea mtoto wa mwenzio tena kwa kuprovide kila kitu kutoka kwako as if alikuzalia yeye.Nakusifu kwa kuchukua jukumu la kutoa msaada wa kuwalea watoto wa marehemu ambao mara nyingi ndo chanzo cha kuonekana una roho mbaya dia.
 
Back
Top Bottom