Nomba kujuzwa hivi bandari ipo ndani ya mashirika ya muungano?

Haipo ndio maana hao Wazanzibari wanataka kuuza baada ya kuona Watanganyika ni wapumbavu.
 
Je bandari ya Dar es Salaam ipo ndani ya mashirika ya Umma ya muuungano?

Kuuliza si ujinga
Bandari ya Dar es Salaam ipo chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Huko Zanzibar wana usimamizi chini ya Zanzibar Port Corporation (ZPC).

Hivyo, ijapokuwa bandari ni sehemu ya mambo ya Muungano lakini ni katika muktadha wa usafiri wa watu na vitu kadhaa.

Ndiyo maana ukinunua baadhi ya vitu Zanzibar ukifikisha tu Dar, unalimwa kodi.
 
Bandari ni jambo la muungano.
(Pamoja na usafiri wa anga, posta na mawasiliano ya simu).

Lakini Zanzibar walianzisha mamlaka yao ya bandari, sijui kwa utaratibu upi maana katiba inasema wazi ni jambo la muungano.

Muungano wetu umejaa uhuni uhuni mwingi, na siku zinavyozidi kwenda Zanzibar wanazidi kuanzisha taasisi zao kwa mambo yanayopaswa kuwa ya muungano, wakati huohuo vya Tanganyika wanavitaka pia.
 
Back
Top Bottom