C- series zinakuwa na specs kubwa zaidi hasa Ram na storage ila haitofautiani sawa na A series
A- series haitofautiani sana na C inakuwa na design nzuri na ina muonekano wake unavutia ila specs zake za kawaida
J- series zenyewe zimetengenezwa kuvutia watu wasio na hela kubwa ya kununulia simu zinauzwa bei rahisi zaidi, specs zake na muonekano sio mzuri kama hao hapo juu.
Note- series ni habari nyengine yenyewe ni flagship All around ni simu nzuri kuliko J, C na A.
sema inabidi uwe makini kuna vitu viwili muhimu vya kuangalia,
1. mwaka simu iliotoka
ni vyema ku consider hiki kitu, sababu Note series ni nzuri haimaanishi note ya mwaka 2013 itakuwa nzuri kuliko C au A ya 2017. inabidi uangalie ni latest kiasi gani.
2. zina michanganuo ya model,
kuna A3, A5, A7 etc, kuna C5, C7, C9 etc J3, J5, J7 etc
Hapa tunajua C au A ni nzuri kuliko J lakini si mara zote mfano J kubwa kama J7 inaweza kuwa nzuri kuliko A ndogo kama A3.