kaka why mnanunua windows phone halafu mnatafuta support kwenye website zenye watu wanaotumia android? lazima utaichoka sababu imetengenezwa kufanya vitu ambavyo android haiwezi kufanya sasa wewe kama unataka windows phone iwe android utakesha. sababu before kuomba msaada tayari ushaconclude hivyo ulivyovitaja havipo.
1. kueka 3g only.
android yenyewe imepata juzi tu hii option android zote za nyuma zilikua hamna sishangai os mpya ikawa haina. lakini kuonyesha kwamba hujatafuta solution kwenye site za windows phone ni kwamba hichi kitu ni common na kina solution kueka 3g only
nakushauri nenda wpcentral utapata solution ya kila namna. na solution yako ya kueka 3g only hii hapa.
Lumia 1020 ##3282 field test menu - Windows Phone Central Forums
2. swali la internet sharing kukataa solution yake ni hao hapo juu yaani field test kama umefanikiwa kueka 3g only ujue pia hapa itakubali. na pia kuna case watu wananunua simu za atnt au verizon au vodaphone mitandao ya majuu wanalock tethering ikija huku inakataa hadi uifanyie tweak.
3.kaka ukisema internet haipo stable ujue simu yako ndo ina matatizo sababu ni hii. lumia 1020 inatumia snapdragon s4 chip hii chip inatumika kote kote kwenye android na wp. adapter ya network ya lumia 1020 ni sawa na ya moto x, sawa na ya hizi xperia zote sawa na za samsung na wengine. huenda eneo lako huna network fanya research moja change line tigo, voda na airtel ujue tatizo ni simu au mtandao.
4. kaka ukidownload file ambalo halitambuliki kwenye windows phone linapotea ila bado lipo kwenye simu, unapoconect kwenye computer simu yako inakuwa mass storage utaona mafile yote. ukitaka kudownload mafile yaresume na mafile makubwa tumia uc browser halafu ukiconect simu na pc utaona mafolder yanatokea
nenda hapa kuona mass storage
WP8 Drag & Drop File Storage Detailed : My Nokia Blog