Nobel Prize inamnyemelea Rais Samia

Kama hilo liko kwenye urefu wa kamba yake hamna kesi
 
Ndoto za mchana..

Hivi mnajua vigezo hadi upate hiyo nishani au mnafikiri inatolewa kisanii kama Ccm mlivyo wasanii??
 
Rais Mama Samia akiendelea hivihivi na juhudi za kujali hali za wananchi wa kawaida na kukuza demokrasia nchini lazima atapata mojawapo ya zawadi za amani za Nobel au Mo Ibrahim, Inshallah
Aje na katiba mbwembwe hatuhitaji
 
Kwakua mabeberu hawana shida naye basi ni jambo la muda tu.
 

Kwa kuahirisha katiba mpya hadi naye akwibe uchaguzi kwanza?
 
Hizo ni
Hizo ni ndoto za mchana, mtu asiyejielewa hawezi kuipata
 
Hata yeye anaweza kukataa kuandika katiba mpya kama walivyokataa waliomtangulia wote. Tusimchukulie poa
Suala ya katiba mpya siyo lake wala halimhusu bali ni la wenye nchi ambao ni wananchi.

Yeye Samia yupo chini ya wenye nchi ambao ni wananchi kwa hiyo hana nguvu wala uwezo wa kukataa maagizo ya maboss wake ambao ni wananchi.
 
Labda ya familia yako, not from Stockholm!
 
Sisi kazi kazi hiyo kwanza makundi ya uchaguzi ndani ya ccm yakae nae mbali ili afikikirie katiba mpya tu, uchaguzi wa kung'oana meno na kuminyana korodani hatutaki mama sasa ni 9yrs bila uchaguzi wa kitapeli
 
Namuombea kwa Mungu asilitie tembo maji nchi ielekee kule waliko watu wastaarabu.

Hujaona kuwa ameishaanza kulitia maji hilo TEMBO kwa kujibu utumbo kuhusu katiba alipohojiwa na Kikeke wa BBC?
 
Huo utumbo ndiyo kutumikia taifa
Kwahiyo kudai katiba mpya ndiyo muhimu kwenu kuliko kumpatia maji kila mtanzania?

Hivi leo hii tukienda kwa wananchi huko mikoani tuwaulize wachague mwaka huu 2022 wapatiwe kimojawapo kati ya maji safi na Katiba mpya unadhani watachagua nini?

Katiba iliyoko sio mbaya wabaya ni wanaotakiwa kuilinda na kuishi. Hata Marekani wana tume huru kwelikweli ya uchaguzi lakini umeona Trump aligoma kuyatambua matokeo na kugoma kuondoka Ikulu.

Tusidanganye watu wetu kuwa katiba yetu ndiyo chanzo cha hali mbaya walizokuwa nazo. Kenya, Zambia, Malawi, DRC wana katiba nzuri na tume huru kwelikweli za uchaguzi lakini hali zao ni heri ya sisi.

Tatizo letu ni uongozi sio katiba, na Rais Samia analifahamu hilo.

Unapodai vitu ambavyo sio tatizo kwa wananchi wala kipaumbele chao kunasababisha hata kiongozi wao huyo akikamatwa kama alivyo kamatwa Mh. Mbowe na kwenda jela wananchi wa kawaida wataendelea na shughuli zao zinazowahangaisha kila siku.

Huwezi kuwaona wanaandama wala kuchoma matairi barabarani kwakuwa hawaoni maana ya kile unachokidai hadi ukamatwe.
 
Wakati katiba ya 1977 inatengenezwa maji hayakupelekwa au 2014 maji haya kupelekwa?
 
Wapo marais wengi waliofanya zaidi ya anavyofanya Samia lakini hawamupata hizo tuzo.

Tuzo hizo zina vigezo specific ambavyo kuvifikia uwe umefanya mambo ya pekee hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…