Noandoka Tanzania

Kama kweli unataka kuondoka na kuishi vizuri usiende ulaya wala amerika tafuta nchi yeyote Africa yenye amani kasettle huko
 
Pole sana kwa kuchukua uamuzi huo, ni kweli kuna baadhi ya changamoto zipo hapa nchini ila naamini zinarekebishika, inawezekana kuna watu wameshindwa kufanya majukumu yao kutokana na uoga au unafiki wa kushauri vizuri maeneno fulani ila ninaamini kabisa jinsi siku zinavyoelekea tutakaa sawa, ukiondoka wewe ukawaacha ndugu zako, rafiki zako na taifa lako bado naona ni kujiweka katika shida nyingine kubwa, maana unapoishi nchi nyingine unakuwa mgeni, hutakuwa hata na haki ya kulaumu au kukosoa mambo yakienda kombo kwenye hizo nchi. Hakuna nchi ambayo haina changamoto, kila sehemu zipo shida zake na uzuri wake. Kinachotakiwa ni kupaza sauti kiungwana ili wahusika wajitathmini kiungwana na kurekebisha kasoro kiungwana ili tupige hatua.
 

Mkuu aliwahi kuandika NGULI WA MASHAIRI NA UANDISHI marehemu Mzee Shaaban Robert katika kitabu chake cha Maisha ya Shaaban Robert kwamba "huwezi toka kwa jirani ukaenda kwa jirani bali mtu hutoka nyumbani kwenda kwa jirani", rudisha mabegi nyumbani mkuu, tafadhali usiende huko watakudharau, watakutukana, watakudhalilisha na hutaweza kujitetea kwakua, wewe ni miongoni mwa watu wa hovyo katika dunia hii na ni kweli ukitafakari kwa kina, utagundua kweli ni wa hovyo...
 
Safari njema. Wasalimje kwenu Somalia.
 
Unapokimbilia wenzako walipita hapatulipo miaka makumi kadhaa yaliyopita. Usidhani huku ni salama kuliko tz. Watu weusi wanaishi kwa manyanyaso makubwa sana. Nikueleze tu Tanzania ninayoiota ilikuwa lazima tuanzie hapa tulipo kwa sasa. La sivyo tungeendelea kuwa wasindikizaji. Nenda tuachie nchi yetu. Tukishaitengeneza karibu tena uje kuivuruga
 
Nikiendelea kuka hapa nitakuja kuwa mtu mbaya sana zaidi ya gaidi
Nimekupata mkuu. All the best! Wengi waliondoka toka zamani kwasababu hizihizi. Unaweza kujikuta upo jela au umeuwawa na watu wasiojulikana na manazi wengine wa chama na sirkali.

Nchi imekuwa hovyo sana siwezi kukushauri tofauti mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…