GE2025 No reforms no election itatekelezwaje, raia tujiandaeje?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi; hata jwa bahati mbaya serikali isikae kimya pale ustawi wa wananchi kijamii, kiuchumi na kisiiasa unapotishiwa na mtu wala kikundi fulani
Unaandika Uzi Kisha unajijibu mwenyewe! Tz tunasafari ndefu sana!
 
Kila alfajiri lazima wanipigie simu kuulizia kama nimetekwa na mimi.

Bro wanaotekwa wanajijua orodha yao na kosa lao, Hizi kelele za utekaji ni njia yao ya kujihami wasitekwe. Acheni tabia ya kutembea na waumini wenu wake za watu la sivyo mtatekwa kweli. Kama wewe uko kwenye orodha ya waliokuwa wananataka Rais Samia asiwe Rais si utakuwa unadhani kuwa utatekwa? Utakuwa unaogopa kivuli chako mwenyewe.
Umeacha kujiheshimu mkuu au siyo?
 
Muundo wa tume ya uchaguzi uko kwenye katiba ya nchi. Kuibadilisha tume lazima uibadilishe vifungu vya katiba. katiba ni ya wananchi wote 65m sio ya viongozi wa siasa tu. Hivyo kuibadilisha katiba lazima tuhusishwe sisi wote hata tusiojuwa na vyama, Unaposema no reforms no election ni juhudi za kikundi kulazimisha kupora madaraka ya wananchi. Lazima tupate muda wa kurudi kwa wananchi wote waamue juu ya madaraka.

Huko nyuma wabunge wachache walikuwa wanachakachua katiba kwaajili yetu, hiyo hatuitaki sasa hivi.
Ndio ujue hakuna uchaguzi Hadi tukae tujadiliane.

NRNE 💪 🔥
 
Kwa akili kama yako, Tanzania itaendelea kuwa chaka la wapigaji na wezi wa kura, na rudi shule ujifunze kuandika tena
 
Kuna sehemu nilimsikia mtu ikibidi bendera ipepee nusu mlingoti.

Ni mchungaji mmoja hivi.

Sasa sijui kamba ya kuipandisha bendera imekuwa fupi au upepo wa kuipepea umeshuka chini kwa mujibu wa TMA, anyway iwe iwavyo itekelezwe.
Mungu hapendi kuombea mtu mabaya, yatakurudia, waulize watu wa ubaya ubwela watakwambia kilichowakuta.
 
k
kwani hiyo agenda nonsense ya mropokaji bado ipo? sio alienda nayo korokoroni?🐒
20250820_184603.jpg

Ipo siku wewe Tlaatlaah na hayawani wenzio mtakuja kuelewa tu though it could be too late.

Hata hivyo hatuchoki kukuelimisha. Hebu soma maneno ya huyu anayemwita "mropokaji" kisha jipime naye na utagundua kuwa kumbe wewe ni takataka tu usiye na lolote kichwani mwako...

Haya soma hapa👇

"......Hayo maneno yanayodaiwa kuwa nilisema. Sitaki tusumbuane huko mbele ya safari. Ninachokisema hapa ni kwamba NI KWELI NILISEMA MANENO HAYO na sijawahi kukataa maneno yangu....."

".....Ni maneno ambayo nimeyasema kwenye mikutano yangu ya hadhara mkoa wa Mbeya, mkoa wa Iringa, Songwe, Njombe, Rukwa na Mtwara....."

"....Msimamo wangu kuhusu kuzuia uchaguzi haujawahi kuwa wa kificho, ni WA wazi na usioyumba na ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa. Swali ni, Je Msimamo na maneno yangu ndiyo uhaini..."

"...Mh Hakimu, nataka hawa wanaonishitaki kwa uhaini, wajibu hilo swali la msingi. Je, huo ndio uhaini kwa mujibu wa sheria zetu za Tanzania...?"

".....Msihangaike kwa sababu sitabishina na hao mashahidi mchongo wa gizani au hawa mashahidi wa video. Hawa hawana lolote na sina shida nao..."

Tundu A. M. Lissu
Mahakama ya Kisutu - Dar eE Salaam
18/8/2025

----------------------------------------------
Godbless Lema naye anaandika katika X - Twitter page yake👇

"....Kuna watu ambao historia huwaita kwa jina la pekee, sio kwa mali walizokuwa nazo, sio kwa nguvu walizoshikilia, bali kwa msimamo usiotikisika mbele ya dhoruba.

Tundu Lissu ni mmoja wao....

Wakati fulani nilipodhani nimemjua, lakini nimegundua Sasa kuwa, kumbe nilikuwa bado sijamjua vya kutosha...

Tundu Lissu anasimama ktk kile anachokiamini. Na sababu na kiini cha msimamo wake hakiwezi kupimwa kwa macho ya kawaida. Huyu mtu haina shaka yoyote kuwa ni mtu wa haki, anaipenda HAKI....

Hakuna kitisho kinachoweza kumbadilisha Mwenyekiti wetu Tundu Lissu, natamani wangalijua hili mapema, ili waepuke adhabu kali ya Mungu iliyo mbele yao....

Mwenyekiti Tundu Lissu ni mtu anayesimama juu ya misingi ya haki. Hofu, kifungo, hata kifo havina uwezo wa kuondoa ukweli huu kwake.

Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini mateso haya si alama ya kushindwa, bali ni alama ya maana ya utu. Kwa upande mwingine, wenye mamlaka wanaoyatumia vibaya hujenga kaburi lao wenyewe....

Mshahara wa dhambi ni mauti, hakuna mamlaka itakayo dumu juu ya udhalimu. Mungu anaandaa jambo kuu, ambalo si kila mtu ataweza kuliona. Watesi na waonevu wa Nchi yetu wataangamia, kwa sababu wamevuka mipaka ya utu , haki na uadilifu kwa kiwango cha juu kabisa...."
 
Usalama kwanza

Tusilichukulie poa neno hili la no reforms no election. Watanzania tuna haki ya kujua kama siku hiyo tutarajie kuona, kusikia au kupatwa na kitu gani kutokana na harakati za kuzuia uchaguzi kama hizo reforms hazitatekelezwa ili tujiandae mapema.

Kuna wakati nilitaka kuamini kuwa no reforms no election itatekelezwa kwa kuhamasisha watu wabaki majumbani wasiende kupiga kula lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, hasa baada ya kumsikia Mh. Lissu akisema watakinukisha vibaya sana siku hiyo. Hapo ndiyo nikajua kuwa huwezi kukinukisha vibaya sana kwa kulala nyumbani siku ya uchaguzi usiende kupiga kura.

Kukinukisha vibaya sana nchi nzima siku ya uchaguzi ambayo watu wengi watakuwa kwenye misululu mirefu ya kusubiri kupiga kura mbele ya askali polisi wanaolinda usalama wa wapigakura, wasimamizi na masanduku ya kura bila shaka yoyote lazima kutasababisha mzozano mkubwa sana kati ya wanaotaka kupiga kura dhidi ya wasiotaka kupiga kura, vyombo vya usalama dhidi ya wanaozuia watu wasipige kura, na wanaotaka kupiga kura wakisaidiwa na walinzi wa uchaguzi dhidi ya wanaopinga uchaguzi. Kwavyovyote vile mzozano kama huu lazima utazalisha hasira, kugombana, majeraha na mauaji kwa raia na wanausalama. Hii inanitia hofu na sipendi mimi na familia yangu kuichukulia poa.

Kama mimi nimeogopa hivi bila shaka hata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na vyombo vyote vya ulinzi na usalama huenda navyo vimeogopa kama mimi au zaidi pengine kuliko mimi; maana hawa tumewapa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Naomba watu hawa watuhakikishie usalama wetu na watueleze mapema wajibu wetu siku hiyo ili tujiandae.
Kaa na kura yako nyumbani
 
View attachment 3447312

Lissu atulie kwakuwa swala liko mahakamani, katika nchi za utawala wa sheria mabishano kati ya makosa na haki vinaamuliwa mahakamani.

Hata hivyo kwenye Taifa la watu 65m haifai kuwa na mtu mwenye kura ya veto, akisema sitaki hiki na kile lazima vitejelezwe la sivyo kitanuka vibaya sana. Lissu na wenzake wana kazi ya kutengeneza akidi ya watanzania inayotosha kulazimisha jambo lao litekelezwe kama lilivyo. Vinginevyo, watanzania wanayo haki ya kuishi bila vitisho na serikali lazima iwahakikishie ustawi watu wake na iwalinde dhidi ya lugha na vitendo vinavyotia hofu.

Hata huko China, Urusi, NKorea, cuba, Rwanda, Uganda Kuna wanaopinga serikali zao lakini ni kama hawapo tu.
 
Unaandika Uzi Kisha unajijibu mwenyewe! Tz tunasafari ndefu sana!
Demokrasia hiyo ya tume huru tunayoidai kwa nguvu zote itatusaidia nini sisi waafrika? Africa tunazo nchi ambazo zimepiga hatua kwenye tume huru za uchaguzi kama vile Kenya, Malawi, na Zambia ambako hata wagombea wa upinzani wanaweza kushinda uchaguzi. Lakini hata kwenye nchi hizo hali za wananchi wao sio za kutamanisha kuwaiga. Tume huru inasaidia tu kupata wahuni wapya Ikulu lakini hali za wananchi ama zinabakia vilevile au zinarudi nyuma kabisa.

Yaani vyama vinaokoteza wagombea Urais na ubunge eti vishike Dola halafu utarajie hali bora kwa wananchi, ni ndoto. Demokrasia baado kabisa Africa kwakuwa shida yetu kuu sio ukosefu wa demokrasia. China, Urusi, Cuba na uarabuni hakuna demokrasia pana lakini hali za raia zinafurahisha. Kudai demokrasia Africa ni sawa na kukaribisha the survival for the fittest, utaumia Bure.
 
Usalama kwanza

Tusilichukulie poa neno hili la no reforms no election. Watanzania tuna haki ya kujua kama siku hiyo tutarajie kuona, kusikia au kupatwa na kitu gani kutokana na harakati za kuzuia uchaguzi kama hizo reforms hazitatekelezwa ili tujiandae mapema.

Kuna wakati nilitaka kuamini kuwa no reforms no election itatekelezwa kwa kuhamasisha watu wabaki majumbani wasiende kupiga kula lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, hasa baada ya kumsikia Mh. Lissu akisema watakinukisha vibaya sana siku hiyo. Hapo ndiyo nikajua kuwa huwezi kukinukisha vibaya sana kwa kulala nyumbani siku ya uchaguzi usiende kupiga kura.

Kukinukisha vibaya sana nchi nzima siku ya uchaguzi ambayo watu wengi watakuwa kwenye misululu mirefu ya kusubiri kupiga kura mbele ya askali polisi wanaolinda usalama wa wapigakura, wasimamizi na masanduku ya kura bila shaka yoyote lazima kutasababisha mzozano mkubwa sana kati ya wanaotaka kupiga kura dhidi ya wasiotaka kupiga kura, vyombo vya usalama dhidi ya wanaozuia watu wasipige kura, na wanaotaka kupiga kura wakisaidiwa na walinzi wa uchaguzi dhidi ya wanaopinga uchaguzi. Kwavyovyote vile mzozano kama huu lazima utazalisha hasira, kugombana, majeraha na mauaji kwa raia na wanausalama. Hii inanitia hofu na sipendi mimi na familia yangu kuichukulia poa.

Kama mimi nimeogopa hivi bila shaka hata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na vyombo vyote vya ulinzi na usalama huenda navyo vimeogopa kama mimi au zaidi pengine kuliko mimi; maana hawa tumewapa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Naomba watu hawa watuhakikishie usalama wetu na watueleze mapema wajibu wetu siku hiyo ili tujiandae.
KUKINUKISHA maana yake ni nini mkuu?
 
Lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi; hata kwa bahati mbaya serikali isikae kimya pale ustawi wa wananchi kijamii, kiuchumi na kisiiasa unapotishiwa na mtu wala kikundi fulani
Ustawi wa wananchi wakati WaTanganyika wanaibiwa na kuchomekewa tozo za kila aina kila kona! Amka usingizini!
 
Nadhani kuendelea kuweko korokoroni ni mojawapo ya serikali kulinda ustawi wa wananchi kijamii, kiuchumi na kisiasa. Maandamano na mikutano ya kila siku inaharibu ustawi wa wananchi kiuchumi. Lazima kipindi cha maandamano na mikutano kijulikane na isiwe ni wakati wote mwaka mzima.
We kama nani upinge katiba inayotoa uhuru huo?
Ukishakuwa ccm tu unakuwa mpumbavu
 
kumbuka kwamba hapa tunahangaika na watu ambao walitaka kubadilisha Katiba ili makumu wa Rais asiapishwe kuwa Rais baada ya mpendwa wetu JPM kufariki dunia. Kwanza hatujui walitaka kufanya hivyo kwasababu gani, pili hatujui baada ya kushindwa kubadilisha Katiba na Makamu kuapishwa kuwa Rais watu hao wanasemaje, wanafanya nini au wanapanga kufanya nini. Taarifa zao na idadi bila shaka ziko mahali fulani kwenye vyombo husika. Kwahiyo kila tunachokiona sasa hivi tunadhani kiko sahihi tu.
 
Yaani wewe mtu kama atakwambia utakiona cha mtema kuni utabaki unakenua tu. Unaijua nguvu inayoweza kutumika kuzuia uchaguzi nchi nzima ni kubwa au ndogo kiasi gani? Kama wewe huogopi mimi naogopa aisei!
Sasa kama sijui maana ya CHA MTEMA KUNI nipate mawenge ya kutoka wapi?
Kwa hiyo unataka kuaminisha kwamba KUKINUKISHA=CHA MTEMA KUNI?
 
Back
Top Bottom