GE2025 No reforms no election itatekelezwaje, raia tujiandaeje?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Usalama kwanza

Tusilichukulie poa neno hili la no reforms no election. Watanzania tuna haki ya kujua kama siku hiyo tutarajie kuona, kusikia au kupatwa na kitu gani kutokana na harakati za kuzuia uchaguzi kama hizo reforms hazitatekelezwa ili tujiandae mapema.

Kuna wakati nilitaka kuamini kuwa no reforms no election itatekelezwa kwa kuhamasisha watu wabaki majumbani wasiende kupiga kula lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, hasa baada ya kumsikia Mh. Lissu akisema watakinukisha vibaya sana siku hiyo. Hapo ndiyo nikajua kuwa huwezi kukinukisha vibaya sana kwa kulala nyumbani siku ya uchaguzi usiende kupiga kura.

Kukinukisha vibaya sana nchi nzima siku ya uchaguzi ambayo watu wengi watakuwa kwenye misululu mirefu ya kusubiri kupiga kura mbele ya askali polisi wanaolinda usalama wa wapigakura, wasimamizi na masanduku ya kura bila shaka yoyote lazima kutasababisha mzozano mkubwa sana kati ya wanaotaka kupiga kura dhidi ya wasiotaka kupiga kura, vyombo vya usalama dhidi ya wanaozuia watu wasipige kura, na wanaotaka kupiga kura wakisaidiwa na walinzi wa uchaguzi dhidi ya wanaopinga uchaguzi. Kwavyovyote vile mzozano kama huu lazima utazalisha hasira, kugombana, majeraha na mauaji kwa raia na wanausalama. Hii inanitia hofu na sipendi mimi na familia yangu kuichukulia poa.

Kama mimi nimeogopa hivi bila shaka hata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na vyombo vyote vya ulinzi na usalama huenda navyo vimeogopa kama mimi au zaidi pengine kuliko mimi; maana hawa tumewapa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Naomba watu hawa watuhakikishie usalama wetu na watueleze mapema wajibu wetu siku hiyo ili tujiandae.
Endelea na shughuli zako tu hakuna kupiga kura
 
Ipo, no reforms no election
Hii agenda emexpire, watu wamepata muda mwingi wa kuitafakari wakaona ni utapeli tu. Lema mwenyewe yuko Canada na familia yake, ameondoka na tonetone zetu, na mhe, Lissu anazunguusha ngumi korokoroni, kuna nini tena hapo. Atatoka baada ya watu kuapa na nchi kupata viongozi wake.
 
Hatwendi kwa kumuangalia mtu mmoja sio Mungu huyo!
 
Kuna sehemu nilimsikia mtu ikibidi bendera ipepee nusu mlingoti.

Ni mchungaji mmoja hivi.

Sasa sijui kamba ya kuipandisha bendera imekuwa fupi au upepo wa kuipepea umeshuka chini kwa mujibu wa TMA, anyway iwe iwavyo itekelezwe.
 
Unajuwaje kama wazazi waks hawajatekwa?

Daini bongo zenu huko ccm
Kila alfajiri lazima wanipigie simu kuulizia kama nimetekwa na mimi.

Bro wanaotekwa wanajijua orodha yao na kosa lao, Hizi kelele za utekaji ni njia yao ya kujihami wasitekwe. Acheni tabia ya kutembea na waumini wenu wake za watu la sivyo mtatekwa kweli. Kama wewe uko kwenye orodha ya waliokuwa wananataka Rais Samia asiwe Rais si utakuwa unadhani kuwa utatekwa? Utakuwa unaogopa kivuli chako mwenyewe.
 
Hayo ni mapinduzi, na ndiyo uhaini wenyewe sasa unaosemwa. kama watu hawatajitokeza kupiga kura maana yake nchi haitakuwa na Rais, wabunge, na madiwani; hivyo hakutakuwa na mawaziri wala bajeti. Katiba yetu itakuwa imeparaganyika maana haisemi kitu kuhusu hilo.
Ndipo sasa ulipo mizizi wa tatizo.

Bila Reforms, hapatafanyika uchaguzi. Ili ufanyike, shart reforms ziwwpo kwa katiba kupata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.

Ili yote yawepo, lazima tupate sanduku la kura lisilonajisiwa,

Tupate viongozi watakaochaguliwa kwa haki si kwa hila.

Kama kuzuia uchaguzi batili usifanyike, kama kuzuia wizi wa kura ni uhaini, basi kumbe wahaini tupo wengi sana.

NRNE 💪 🔥
 
Kwani Lumumba si mnaenda kutiki kwa Bi Mwenda hiyo October wasiwasi wenu ni upi?

Mlishasema CHADEMA imejifia msajili na mahakama wameizuia kufanya shughuli zote za kisiasa bila kujulikana zuio hili litaisha lini.

Wanalumumba sasa kwanini muumie wakati kwenye sanduku atakuwepo bi Mwenda pekeyake mtatiki hadi mtikise viuno hilo bado haliwapi furaha ?

Mmjeiandaaje kusherekea ushindi wa kishindo zaidi ya ule wa Magufuli 2020?

Maana bi Mwenda atapata 100% na hilo hata mtoto wa shule ya vidudu analijua.

Saa hizi nadhani mlitakiwa mtuambie mmejiandaa vipi na sherehe ya kumuapisha rais aliyepita bila kupingwa kwa 100% ni rekodi kubwa kwenu na Africa nzima au hilo hamlijui?
 
Kuna sehemu nilimsikia mtu ikibidi bendera ipepee nusu mlingoti.

Ni mchungaji mmoja hivi.

Sasa sijui kamba ya kuipandisha bendera imekuwa fupi au upepo wa kuipepea umeshuka chini kwa mujibu wa TMA, anyway iwe iwavyo itekelezwe.
Hivi huyo alinacha alikuwa mtu wa wapi?
 
Ndipo sasa ulipo mizizi wa tatizo.

Bila Reforms, hapatafanyika uchaguzi. Ili ufanyike, shart reforms ziwwpo kwa katiba kupata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.

Ili yote yawepo, lazima tupate sanduku la kura lisilonajisiwa,

Tupate viongozi watakaochaguliwa kwa haki si kwa hila.

Kama kuzuia uchaguzi batili usifanyike, kama kuzuia wizi wa kura ni uhaini, basi kumbe wahaini tupo wengi sana.

NRNE 💪 🔥
Ni vigumu kutabiri kama kura zitaibwa au la, Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Sugu, Msigwa, nk waliwahi kuwa wabunge wa kuchaguliwa kwa kutumia katiba hiihii, sijui iliwezekana vipi hilo kutokea kwenye tume mbaya kama hiyo unayosema.
 
Naongelea kura ya Urais.

Kura hiyo isiibwe,

Na Tume huru iwe mpya itayoruhusu matokeo ya Urais kukatiwa rufaa Mahakamani.

Sijui unaelewa?
 
Muundo wa tume ya uchaguzi uko kwenye katiba ya nchi. Kuibadilisha tume lazima uibadilishe vifungu vya katiba. katiba ni ya wananchi wote 65m sio ya viongozi wa siasa tu. Hivyo kuibadilisha katiba lazima tuhusishwe sisi wote hata tusiojuwa na vyama, Unaposema no reforms no election ni juhudi za kikundi kulazimisha kupora madaraka ya wananchi. Lazima tupate muda wa kurudi kwa wananchi wote waamue juu ya madaraka.

Huko nyuma wabunge wachache walikuwa wanachakachua katiba kwaajili yetu, hiyo hatuitaki sasa hivi.
 
Usalama kwanza

Tusilichukulie poa neno hili la no reforms no election. Watanzania tuna haki ya kujua kama siku hiyo tutarajie kuona, kusikia au kupatwa na kitu gani kutokana na harakati za kuzuia uchaguzi kama hizo reforms hazitatekelezwa ili tujiandae mapema.

Kuna wakati nilitaka kuamini kuwa no reforms no election itatekelezwa kwa kuhamasisha watu wabaki majumbani wasiende kupiga kula lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, hasa baada ya kumsikia Mh. Lissu akisema watakinukisha vibaya sana siku hiyo. Hapo ndiyo nikajua kuwa huwezi kukinukisha vibaya sana kwa kulala nyumbani siku ya uchaguzi usiende kupiga kura.

Kukinukisha vibaya sana nchi nzima siku ya uchaguzi ambayo watu wengi watakuwa kwenye misululu mirefu ya kusubiri kupiga kura mbele ya askali polisi wanaolinda usalama wa wapigakura, wasimamizi na masanduku ya kura bila shaka yoyote lazima kutasababisha mzozano mkubwa sana kati ya wanaotaka kupiga kura dhidi ya wasiotaka kupiga kura, vyombo vya usalama dhidi ya wanaozuia watu wasipige kura, na wanaotaka kupiga kura wakisaidiwa na walinzi wa uchaguzi dhidi ya wanaopinga uchaguzi. Kwavyovyote vile mzozano kama huu lazima utazalisha hasira, kugombana, majeraha na mauaji kwa raia na wanausalama. Hii inanitia hofu na sipendi mimi na familia yangu kuichukulia poa.

Kama mimi nimeogopa hivi bila shaka hata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na vyombo vyote vya ulinzi na usalama huenda navyo vimeogopa kama mimi au zaidi pengine kuliko mimi; maana hawa tumewapa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Naomba watu hawa watuhakikishie usalama wetu na watueleze mapema wajibu wetu siku hiyo ili tujiandae.

Mungu Yuko kazini kwa namna ya ajabu. Niwaombe waTanzania wenzangu hasa waTanganyika, tuendelee kumwamini Mungu.

Sikiza hii
 
Attachments

Kwani Lumumba si mnaenda kutiki kwa Bi Mwenda hiyo October wasiwasi wenu ni upi?

Mlishasema CHADEMA imejifia msajili na mahakama wameizuia kufanya shughuli zote za kisiasa bila kujulikana zuio hili litaisha lini.

Wanalumumba sasa kwanini muumie wakati kwenye sanduku atakuwepo bi Mwenda pekeyake mtatiki hadi mtikise viuno hilo bado haliwapi furaha ?

Mmjeiandaaje kusherekea ushindi wa kishindo zaidi ya ule wa Magufuli 2020?

Maana bi Mwenda atapata 100% na hilo hata mtoto wa shule ya vidudu analijua.

Saa hizi nadhani mlitakiwa mtuambie mmejiandaa vipi na sherehe ya kumuapisha rais aliyepita bila kupingwa kwa 100% ni rekodi kubwa kwenu na Africa nzima au hilo hamlijui?
Lengo ni kulinda ustawi wa raia kijamii, kiuchumi na kisiasa. Uhuru wako unaishia pale unaponza uhuru wangu. haiwezekani kwa mwaka mzima barabara hazipitiki kwa maandamano ya wanasiasa.
 
Wew mjinga,

Hakuna mpiga kura atajitikeza siku hiyo akisikia kuna maandamano nchi nzima.

Bila Reforms kwenye katiba kupata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya,na CHADEMA kushiriki na Lissu kuachiwa,

Uchaguzi batili UTAYEYUKA.

NRNE 💪 🔥

Hakika
 
Attachments

  • LEO_TAR_20_08_2025_BILA_WOGA_HUMPHREY_POLEPOLE_AWATAJA_WAHUNI_WOTE_KWA_MAJINA,_AMSHAURI_RAIS_S...mp4
    19.2 MB
Usalama kwanza

Tusilichukulie poa neno hili la no reforms no election. Watanzania tuna haki ya kujua kama siku hiyo tutarajie kuona, kusikia au kupatwa na kitu gani kutokana na harakati za kuzuia uchaguzi kama hizo reforms hazitatekelezwa ili tujiandae mapema.

Kuna wakati nilitaka kuamini kuwa no reforms no election itatekelezwa kwa kuhamasisha watu wabaki majumbani wasiende kupiga kula lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, hasa baada ya kumsikia Mh. Lissu akisema watakinukisha vibaya sana siku hiyo. Hapo ndiyo nikajua kuwa huwezi kukinukisha vibaya sana kwa kulala nyumbani siku ya uchaguzi usiende kupiga kura.

Kukinukisha vibaya sana nchi nzima siku ya uchaguzi ambayo watu wengi watakuwa kwenye misululu mirefu ya kusubiri kupiga kura mbele ya askali polisi wanaolinda usalama wa wapigakura, wasimamizi na masanduku ya kura bila shaka yoyote lazima kutasababisha mzozano mkubwa sana kati ya wanaotaka kupiga kura dhidi ya wasiotaka kupiga kura, vyombo vya usalama dhidi ya wanaozuia watu wasipige kura, na wanaotaka kupiga kura wakisaidiwa na walinzi wa uchaguzi dhidi ya wanaopinga uchaguzi. Kwavyovyote vile mzozano kama huu lazima utazalisha hasira, kugombana, majeraha na mauaji kwa raia na wanausalama. Hii inanitia hofu na sipendi mimi na familia yangu kuichukulia poa.

Kama mimi nimeogopa hivi bila shaka hata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na vyombo vyote vya ulinzi na usalama huenda navyo vimeogopa kama mimi au zaidi pengine kuliko mimi; maana hawa tumewapa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu. Naomba watu hawa watuhakikishie usalama wetu na watueleze mapema wajibu wetu siku hiyo ili tujiandae.

Ukiona hujaelewa na unataka notes ukakariri ujue haikuhusu na ipo nje kabisa ya IQ yako acha tu ipite watanzania milioni 10 tu wakielewa na ukabaki ww na wengine milioni 50 kama wewe inatosha tu

Sio kila kitu ushiriki, ukishiriki ulanzi ni chaguo lako na maisha yataendeea tu, NRNE ni English ujue na kiingereza sio kalio kwamba kila mtu analo

Una haki ya kujua yes km ulivosema lkn sio kila kitu utajua vingine viko juu sana ya uwezo wako waachie wanaoweza utakuja kujua baadaye sana laggards lazima kwenye jamii yoyote na sio dhambi wala jinai
 
Kumbuka....

Alisema msisiemu mwingine miaka kadhaa nyuma!

WATANZANIA WANA IQ NDOGO KULIKO NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI.

Na Thadei Ole Mushi.

Niliwahi kufundisha kidogo hapa kuhusu uwezo wa akili au kitaalamu (IQ) yaani Hisa ya akili.

Mwaka jana kuna ripoti ilitoka ikiwa inaitaja Tanzania kushika nafasi ya 9 katika nchi zenye watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri.

Kwa mujibu wa orodha hiyo,Tanzania inashika nafasi ya 9 wananchi wake wakiwa na uwezo wa kufikiri (IQ) 72, Ghana inashika nafasi ya 8 kwa wananchi wake kuwa na kiwango cha chini cha IQ yaani 71. Nafasi ya saba ni Nigeria (67), nafasi ya sita ni Guinea (66), nafasi ya tano ni Zimbabwe (66), nafasi ya nne ni DR Congo (65), nafasi ya tatu ni Sierra Leone (64), nafasi ya pili ni Ethiopia (63) na nafasi ya kwanza ni Equatorial Guinea (59).Katika nchi zote hapo Tanzania pekee ndio inayojitokeza kwenye orodha hiyo ikiwa imetokea ukanda wa Africa Mashariki.

Kuna wengi watashindwa kupata tafsiri ya kilichomo kwenye mabano yaani number zilizomo kwenye mabano hivyo ni vizuri nikafafanua tena hili.

Mwaka 1904 mwanasaikolojia Alfred Banet alitambulisha nadharia ya namna ya kupima Uwezo wa mtu wa kufiki (IQ) Baadaye 1979 alitokea mtu mwingine aliyekuja kuboresha kidogo tu nadharia hii anaitwa Hilgard huyu aliainisha viwango vya akili ya mwanadamu.

Wananadharia hii kwa pamoja hawajawahi kutofautina na maana halisi ya Hisa ya akili. Wote wanakubaliana kuwa hisa ya akili kipimo cha maendeleo ya kitaaluma kwa kuwianisha UMRI wa kuzaliwa wa mtoto na UMRI wa akili.

Ili uweze kupata hisa ya akili ya mtu unatakiwa uchukue UMRI wa akili ×100 halafu gawanya kwa UMRI wa kuzaliwa.

UMRI wa akili hupatikana kwa kukadiria matendo ayafanyayo mtu. Kwa mfano nyumbani una mtoto wa Miaka 10 lakini matendo yake na uwezo wake unalingana na mtoto wa Miaka 15 basi miaka hiyo 15 ndio UMRI Wake kiakili hivyo utachukua (15×100 ) ÷ 10 = 150.

Nini tafriri yake? Wanasaiokolojia hawa katika nadharia hii wameonyesha pia matokeo ya ukokotoaji kwa mfano hapo jibu tumepata ni 150 mtoto huyu atakuwa ni mwenye kipaji maalumu kwani hawa huanzia 139+ .

Chini ya hapo 129-139 ni wenye Akili za juu sana sana, 110-119 hawa wana akili za juu,90-109 wastani, 80-89 wapo chini ya wastani na 70-79 wana akili duni, chini ya 70 hawa wana mtindio wa ubongo (tahira).

Tunapozungumzia hisa ya akili hatumaanishi uwezo alionao mtu katika kukokotoa hisabati au kujibu maswali ya physics kwa ufasaha bali ni ule uwezo wa mtu kutafsiri na kuchambua taarifa mbalimbali zinazofikishwa kwenye ubongo kitaalamu huitwa ABSTRACT REASONING.

Kwa maana hiyo ukichukua mtanzania ukamweka kwenye kundi la wakenya, wanyarwanda nk basi atashika nafasi ya Mwisho katika kutafsiri na kupata ufahamu kwa mambo ambayo yatakuwa mbele yao.

Kuwa na hisa ndogo ya akili hakutokani na kukosa tu elimu ya Darasani japokuwa nayo huchangia bali hutokana na sababu nyingine nyingi kama vile Lishe duni, afya duni, aina ya genes tunazorithi toka kwa mababu zetu nk.

Dr James Watson aliwahi kusema " black people are less intelligent than white people" Huyu Dr alifanya justification ya argument yake kwa kusema kuwa ujinga ni kitu cha kurithi na ni kama ugonjwa. Hili limeshawahi kudhihirishwa na nadharia nyingine nyingi za kisayansi na za kisaikolojia.

Tuangalie sasa ni mambo gani ambayo hata hivyo yanaweza kuwa ni ushahidi wa ujinga wetu:-

1. Pitia scandal ya UPATU ya DECI.

2. Agalia jinsi ukawa ilivyomtukana Lowassa na baadaye wanamsafisha.

3. Angalia jinsi babu wa Loliondo alivyo tuburuza

4. Angalia michango ya wabunge wetu bungeni na jinsi tunavyowashangilia.

5. Angalia rasilimali tulizonazo na uchumi wetu kama vinaendana.

6. Angalia kwa nini Sumaye alihamia Chadema na bado tunaendelea kushangilia na kupiga makofi

Kuna mambo mengi tu yanayodhihirisha ujinga wetu hata wewe unaweza kuyaongeza katika huo mtiririko.Hata comment yako pia inaweza kukutambulisha aina ya IQ uliyonayo.

Ole Mushi.
 
Lengo ni kulinda ustawi wa raia kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Ustawi upi huo?

Wa mtu kuuwawa na tunaambiwa kifo ni kifo?

View: https://youtu.be/fxKshd29204?si=Hr2z050Wi_676SdS
Uhuru wako unaishia pale unaponza uhuru wangu. haiwezekani kwa mwaka mzima barabara hazipitiki kwa maandamano ya wanasiasa.
Uhuru upi huo unaouzungumzia hebu elezea vizuri, nani yuko huru na nani hayupo huru.

Kwanini pia katika nchi barabara zisipitike maana barabara zisipopitika kwa majanga ya asili basi itakuwa kwa vitu ambavyo chanzo chake ni binadamu je unafikiri chanzo cha watu kuandamana kinaweza kuchagizwa na nini?
 
Back
Top Bottom