Kaka hakuna dola inayolindwa kwa njia moja tu. Hata kabla ya ujio wa wakoloni kuja Afrika, machifu wetu walikuwa wakiwaathibu wasaliti wa himaya zao kwa kuwauza kama watumwa. Wakoloni walikuwa wanawanyonga wabishi na wapingaji utawala. Baada ya uhuru wasaliti na wapingaji wa dola wana adhabu kwenye awamu zote. Hata hizi keleletunazozisikia hivi sasa ni watu wanaojihamu wasiadhibiwe na wenye wake zao. Bro ni hatari, heshima katiba mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo. Katiba hii ni haki na wajibu kwa viongozi na raia; isomeni vizuri kila mpatapo muda. Ndiyo maana JPM alipoingia madarakani aliisomaaaaaaaa na akaiangaliaaaaaaaaaa na kusema katiba siibalishi ng'oooo, wacha niitumie hiihii kuinyoosha nchi. Maana yake anafahamu kuwa Katiba hii inamfanya kiongozi wa nchi kuwa "Mungu mtu". Hata hivyo utaratibu wa kubadilisha au kuandika katiba unafahamika; haiwezekani mtu mmoja au kikundi cha watu 3 wakampa ultimatum Rais wa nchi lazima abadilishe katiba leoleo ili wao waweze kwenda Ikulu. Kufanya hivyo ni kutweza Katiba, Rais, rais na mchakato wa kubalisha Katiba. Maana kila mtu anaweza kuja na madai yake kuhusu katiba ambayo lazima yatekelezwe kwa kuzingatia precedency ya sasa.Umeacha kujiheshimu mkuu au siyo?
Umeelewa niluchoandika au ulijibu tu?Mungu hapendi kuombea mtu mabaya, yatakurudia, waulize watu wa ubaya ubwela watakwambia kilichowakuta.