Avatar Myg
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 675
- 118
Kwa ninavyojua Bank za kawaida e.g. CRDB, NBC etc. zimesajiliwa B.O.T na zimedeposit fedha kiasi fulani B.O.T just encase zikafilisika fedha hizo hutumika kuwafidia wateja wao....Wasiwasi wangu ni juu ya haya makampuni ya simu yanavyo offer some banking services (M-pesa, Zpesa, tiGO pesa & ZaP) na watanzania tumezichangamkia huduma hizi kwelikweli!!... 1. Hivi haya makampuni yamefuata utaratibu kama mabenki?... 2. Wamedeposit amount kiasi gani B.O.T as their collateral?... 3. Endapo kama yakifilisika watanzania hatutapata hasara kweli? Usalama wa pesa zetu upoje?... 4. Wanalipa kodi kama mabenki au kama makampuni ya simu? Inabidi tupate mchanganuo kidogo hapa!Tujadili..