Tathmini ya madhara ya kiuchumi juu ya hizi tozo na makato miamala ya simu

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
1,450
2,702
Natanguliza shukrani wasomi Evelyn Richard, University of Dar es Salaam Business School Pamoja Eliamringi Mandari, Bank of Tanzania
Katika utafiti (study) uliochapishwa na chuo kikuu cha dar es salaam juu ya umuhimu wa mobile banking na lengo la kuanzishwa kwake.

Katika utafiti wao walichukua sample ya idadi ya watu 120 ili wapate kugundua ni nini hasa kinawavutia watu kupenda kutumia miamala kwa njia ya simu kupitia mitandao kama mpesa, tigo pesa, airtel money nk.

Kwa mujibu wa data zilizo tolewa na TCRA pamoja na Bank of Tanzania zinaweka wazi kwamba kulikuwa na ongezeko la watumiaji wa miamala ya simu pamoja na faida kubwa kutokana na kuongezeka kwa miamala ya simu.

“number of registered mobile customers surged from 14,000 in June, 2008 to 28.1 million in March, 2014 (TCRA, 2014). The average number of monthly transactions increased from 272,700 in 2009 to 74.9 million in June, 2013 (BOT, 2014); and money stored in mobile accounts increased from Tanzanian shillings (TZS) 3 billion in June, 2009 to TZS 308 billion in March, 2014 (BOT, 2014).”

Hapo juu nimezungumzia kuhusu faida upande wa miamala ya simu nataka niweke hasara bank walizopata kutokana na kukua kwa sim banking kwa mujibu wa hii study ya wasomi hawa wawili.

“However It was noted further that the percentage of those who are excluded from using banking services decreased from 55.3 percent in 2009 to 26.8 percent in 2013, because of the increased use of non-bank formal products from 6.7 percent in 2009 to 43.5 percent in 2013. Despite all these developments in use of mobile phone services and mobile money transfers, usage of banking services and mobile banking, in particular, has remained low in Tanzania.”

Bank zinapata hasara juu ya simu banking sana kwani mapato yao yana shuka pamoja na wateja wao kupungua kwa kiasi kikubwa.

Watumiaji wakubwa sana wa benki ni watu wa tabaka la juu katika miamala yao. Mobile banking ni kwaajili ya watu wa tabaka la kati pamoja na tabaka la chini.

Kinachofanyika hapa ni kuua uchumi wa watu wa tabaka la kati na kuwalazimisha kutumia huduma za benki. Watu wa tabaka la kati nazungumzia wafanya kazi na watumishi. Kinacho fanyika hapa ni kupora uchumi wa watu kutoka mikononi mwao na kuhamishia benki.

Watanzania mjue ongezeko kubwa la kodi hii ni kuwaumiza watu wa kipato cha chini juzi mliongeza mia moja kwenye mafuta sasa tumewapa nchi ya nini sasa,? Nchi inaongozwa na mwanamke alafu mafuta ya kula yanapanda bei. Huruma ipo wapi.

Kutoa shilingi Millioni moja benk gharama yake ni elfu moja mia mbili hadi elfu moja miatano lakini kutoa shilingi milioni moja kwa simu gharama yake ni elfu nane mia tisa (8900). Tunaporwa uchumi wetu wa mkononi halafu banki zinaingia kuendesha maisha yetu. Tunarudishwa nyuma polepole kwani mwakq kesho watapqndishq ten kamq tukikaa kimya.

Watu wa kawaida wanaweza kudhani nachukia mabenki hapana ila kila kizuri kina kasoro. Kiukweli uchumi wa kuyagemea Banki na riba sio kitu kizuri. Kinachofanyika hapa watanzania ni mwanzo wa kutengeneza matabaka mawili. Maskini na matajiri watu wa tabaka la kati ndo mwanzo wa kuvunjwa hapa.

Sababu zilizopelekea kukua kwa sim banking au mobile money ni urahisi wake, kuchukua waakati mfupi, uaminifu wa mtoa huduma, usiri na usalama huwezi kuvamiwa na majambazi labda wakuone unatoka benki, hakuna foleni, makato/gharama ya kuridhisha pamoja na unafuu wa mtoa huduma.

Katika utafiti huo ulio chapishwa na chuo kikuu cha dar es salaam, nanukuu

“Majority of mobile banking services users are those with informal employment. This could be explained by the nature of formal employment absorption in the country. After all, majority of the population is employed by SMEs, which are in the informal sector. However, results showed that the difference in percentage from those with formal employment is small (30 % against 27%). FinScope (2013) shows that 78.6 percent formally employed have/use bank products.”

Kwamba idadi kubwa ya watumiaji miamala ya simu wengi wao hawana ajira rasmi ni watu wanaofanya shughuli kwa muda au kazi ikipatikana leo hana kitu anaomba watu wanamtumia hela m pesa anaishi siku zinae da. Watu walio ajiriwa serikalini au kwenye taasisi na makampuni ndio watumiaji wakubwa wa benki ambao ndio tabaka la kati sababu kubwa ni kuwa mshahara unaingilia bank. Lakini mshahara ukisha ingia anautoa wote anasafishq account na na katika hizo hela zingine anaweka kwenye simu.

Watu wana vikumdi vyao vikoba pesa wanaweka kwenye mobile banki wajikomboe wewe unawarudisha nyuma.

Kwa mujibu wa utafiti huu. Sababu gani zinapelekea sim banking kufa au kupungukiwa na watumiaji? Kwa mujibu

“Rumanyika (2015) used Diffusion Innovation Theory and reviewed literature from 14 papers on obstacles to adopting mobile banking in Tanzania. He (ibid.) used descriptive analysis and identified that theft of mobile handsets, poor network coverage, lack of knowledge of m-banking, high mobile transaction fees, irregular standards of mobile money payments, lack of enough mobile money agents”

Sababu kubwa kati ya hizo ni gharama kubwa katika kufanya miamala.

Mpaka sasa hivi Gavana Benki kuu ya Tanzania yupo ofisini kimya tunasubiri muongozo vipi kuhusu makato mengine mfano kwenye malipo ya serikali, luku dawasco tra huko mmepqndisha pia. Toeni ukakasi juu ya hilo kama na huko kwenye malipo mmepandisha tujue na kama hamja pandisha tujue pia.

Najua sitakiwi kuomba lakini ngoja tu nitoe Ombi langu kwa serikali kuna mtu anaitwa Adam Smith ni mchumi haswa kwenye kibabu chake kinaitwa Wealth of a Nation ameelezea misingi inayopaswa kufuata ili kukusanya kodi yenye baraka kutoka kwa raia kwani kodi zenye malalamiko kama hizi hazina msaada kwa taifa watu wanawachukia.

Msidhani kwamba kukata kodi kubwa kwa watu ndio kuleta maendelea hapana mnazidi tuu kuleta chuki kati yenu na mnao waongoza na hiyo hela ta mkiipata hamtafanyia chochote kuweni na usawa. Nyie ni viongozi simamieni rasilimali za nchi sio kusimamia watu. Au mmetumwa kuwa viranja kwetu?

“taxation should follow the four principles of fairness, certainty, convenience and efficiency. Fairness, in that taxation should be compatible with taxpayers’ conditions, including their ability to pay in line with personal and family needs. Certainty should mean that taxpayers are clearly informed about why and how taxes are levied. Convenience relates to the ease of compliance for the taxpayers: how simple is the process for collecting or paying taxes? Finally, efficiency touches on the collection of taxes: basically put, the administration of tax collection should not negatively affect the allocation and use of resources in the economy, and certainly shouldn’t cost more than the taxes themselves”

Huyu waziri wa fedha mimi simjiu wala sijawahi kumuona ila asitumike vibaya kwenye system kama wewe umesoma tumia taaluma yako kwa weledi. Umepewa hiyo nafasi sio kwamba wewe ni bora kuliko wengine hapana. Umepewa hiyo nafasi kwa lengo kubwa zaidi ya wewe unavyo dhani. Kaa chini tafakari. Aliyekupa hayo mamlaka sio huyo aliye kuchagua.

Kuongeza kodi kwakigezo cha miradi ya maendeleo ni sababu gani hiyo wekeni wazi kuwa hamna ujasiri tena wa kusimamia madini, gesi na rasimimali zingine.

Kuwalimbikizia raia wenzako mzigo wa kodi ikiwa mali wamewapa msimamie ni udhaifu mkubwa sana. Unaacha madini na gesi unakata kodi kwenye miamala ya simu ili uendeshe nchi?
 
kwa hiyo unapenda vya buree eeehh!!!
unataka usadiwe na mataifa ya ulaya eeeh!!!
kumbuka pia misaada tunayo ipata kutoka nchi za ulaya ni KODI ZA WANANCHI WA MAREKANI, UGERUMANI, DENMARK, NEWZELAND, FRANCE, CHINA, UINGEREZA N.K, wananchi wazalendo wa nchi hizo wanatozwa kodi ambazo zingine ndio tunapewa ss misaada na wakati mwengine tunakopeshwa.
acheni kuwa walemavu wa akili lipeni kodi ili itusaidie maendeleo yetu.
Taifa imara itajengwa na sisi watanzania wenyewe kwa kulipa kodi sio kutegemea misaada au mikopo.
 
Umeandika kitaalamu zaidi.

Mobile Money ilikuwa njia nzuri kwa Tanzania kuelekea "Cashless Society".

Hata mimi binafsi nilipendelea zaidi kulipa huduma kwa Mpesa. Ila kwa sasa kutumia Mpesa ni jambo la mwisho kabisa kuliwazia.

Narudi kwenye cash cash. Na bank account.
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!
 
Sijakuelewa
 
Kuna familia inafanya biashara, Baba mtaafu, Mama na mwana wanatunga sheria, kuna expert toka ng'ambo anapewa maelekezo na mstaafu ili kustawisha maslahi yake na familia yake
 
Hakuna ambaye hataki kuilipa kodi huu uzi unawazungumzia hasa wale wa hali ya chini ambao maisha yao ni hand to mouth , kwanini wasingewaza kupunguza mamishahara yao na maposho yasiyo na kichwa wala miguu wakaamini katika kukata vijihela vya masikini ambazo wakati mwingine huko kijijini wanatumiwa kwaajili ya kununulia hata dawa maana hata bima za afya wengi wao hawana, ni udhaifu mkubwa sana kuhangaika na vimiamala vidogo vya simu wakti ma giant hao wabunge hawakatwi hata senti kwenye posho zao, isije kufika mahala tukaanza tena kuchajiwa kodi ya kichwa ,huko ndiko tunakoelekea na ikibidi wataanza hata kodi ya kupumua kabisa, SHAME
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!
Marekani ndo nini wewe?
ishu zetu za kodi marekani anausikaje

Watu awajakataa kulipa kodi, watu wanalalamika makato ni makubwa ayaendani hali ya maisha
 
Natanguliza shukrani wasomi Evelyn Richard, University of Dar es Salaam Business School Pamoja Eliamringi Mandari, Bank of Tanzania
Katika utafiti (study) uliochapishwa na chuo kikuu cha dar es salaam juu ya umuhimu wa mobile banking na lengo la kuanzishwa kwake.

Katika utafiti wao walichukua sample ya idadi ya watu 120 ili wapate kugundua ni nini hasa kinawavutia watu kupenda kutumia miamala kwa njia ya simu kupitia mitandao kama mpesa, tigo pesa, airtel money nk.

Kwa mujibu wa data zilizo tolewa na TCRA pamoja na Bank of Tanzania zinaweka wazi kwamba kulikuwa na ongezeko la watumiaji wa miamala ya simu pamoja na faida kubwa kutokana na kuongezeka kwa miamala ya simu.

“number of registered mobile customers surged from 14,000 in June, 2008 to 28.1 million in March, 2014 (TCRA, 2014). The average number of monthly transactions increased from 272,700 in 2009 to 74.9 million in June, 2013 (BOT, 2014); and money stored in mobile accounts increased from Tanzanian shillings (TZS) 3 billion in June, 2009 to TZS 308 billion in March, 2014 (BOT, 2014).”

Hapo juu nimezungumzia kuhusu faida upande wa miamala ya simu nataka niweke hasara bank walizopata kutokana na kukua kwa sim banking kwa mujibu wa hii study ya wasomi hawa wawili.

“However It was noted further that the percentage of those who are excluded from using banking services decreased from 55.3 percent in 2009 to 26.8 percent in 2013, because of the increased use of non-bank formal products from 6.7 percent in 2009 to 43.5 percent in 2013. Despite all these developments in use of mobile phone services and mobile money transfers, usage of banking services and mobile banking, in particular, has remained low in Tanzania.”

Bank zinapata hasara juu ya simu banking sana kwani mapato yao yana shuka pamoja na wateja wao kupungua kwa kiasi kikubwa.

Watumiaji wakubwa sana wa benki ni watu wa tabaka la juu katika miamala yao. Mobile banking ni kwaajili ya watu wa tabaka la kati pamoja na tabaka la chini.

Kinachofanyika hapa ni kuua uchumi wa watu wa tabaka la kati na kuwalazimisha kutumia huduma za benki. Watu wa tabaka la kati nazungumzia wafanya kazi na watumishi. Kinacho fanyika hapa ni kupora uchumi wa watu kutoka mikononi mwao na kuhamishia benki.

Watanzania mjue ongezeko kubwa la kodi hii ni kuwaumiza watu wa kipato cha chini juzi mliongeza mia moja kwenye mafuta sasa tumewapa nchi ya nini sasa,? Nchi inaongozwa na mwanamke alafu mafuta ya kula yanapanda bei. Huruma ipo wapi.

Kutoa shilingi Millioni moja benk gharama yake ni elfu moja mia mbili hadi elfu moja miatano lakini kutoa shilingi milioni moja kwa simu gharama yake ni elfu nane mia tisa (8900). Tunaporwa uchumi wetu wa mkononi halafu banki zinaingia kuendesha maisha yetu. Tunarudishwa nyuma polepole kwani mwakq kesho watapqndishq ten kamq tukikaa kimya.

Watu wa kawaida wanaweza kudhani nachukia mabenki hapana ila kila kizuri kina kasoro. Kiukweli uchumi wa kuyagemea Banki na riba sio kitu kizuri. Kinachofanyika hapa watanzania ni mwanzo wa kutengeneza matabaka mawili. Maskini na matajiri watu wa tabaka la kati ndo mwanzo wa kuvunjwa hapa.

Sababu zilizopelekea kukua kwa sim banking au mobile money ni urahisi wake, kuchukua waakati mfupi, uaminifu wa mtoa huduma, usiri na usalama huwezi kuvamiwa na majambazi labda wakuone unatoka benki, hakuna foleni, makato/gharama ya kuridhisha pamoja na unafuu wa mtoa huduma.

Katika utafiti huo ulio chapishwa na chuo kikuu cha dar es salaam, nanukuu

“Majority of mobile banking services users are those with informal employment. This could be explained by the nature of formal employment absorption in the country. After all, majority of the population is employed by SMEs, which are in the informal sector. However, results showed that the difference in percentage from those with formal employment is small (30 % against 27%). FinScope (2013) shows that 78.6 percent formally employed have/use bank products.”

Kwamba idadi kubwa ya watumiaji miamala ya simu wengi wao hawana ajira rasmi ni watu wanaofanya shughuli kwa muda au kazi ikipatikana leo hana kitu anaomba watu wanamtumia hela m pesa anaishi siku zinae da. Watu walio ajiriwa serikalini au kwenye taasisi na makampuni ndio watumiaji wakubwa wa benki ambao ndio tabaka la kati sababu kubwa ni kuwa mshahara unaingilia bank. Lakini mshahara ukisha ingia anautoa wote anasafishq account na na katika hizo hela zingine anaweka kwenye simu.

Watu wana vikumdi vyao vikoba pesa wanaweka kwenye mobile banki wajikomboe wewe unawarudisha nyuma.

Kwa mujibu wa utafiti huu. Sababu gani zinapelekea sim banking kufa au kupungukiwa na watumiaji? Kwa mujibu

“Rumanyika (2015) used Diffusion Innovation Theory and reviewed literature from 14 papers on obstacles to adopting mobile banking in Tanzania. He (ibid.) used descriptive analysis and identified that theft of mobile handsets, poor network coverage, lack of knowledge of m-banking, high mobile transaction fees, irregular standards of mobile money payments, lack of enough mobile money agents”

Sababu kubwa kati ya hizo ni gharama kubwa katika kufanya miamala.

Mpaka sasa hivi Gavana Benki kuu ya Tanzania yupo ofisini kimya tunasubiri muongozo vipi kuhusu makato mengine mfano kwenye malipo ya serikali, luku dawasco tra huko mmepqndisha pia. Toeni ukakasi juu ya hilo kama na huko kwenye malipo mmepandisha tujue na kama hamja pandisha tujue pia.

Najua sitakiwi kuomba lakini ngoja tu nitoe Ombi langu kwa serikali kuna mtu anaitwa Adam Smith ni mchumi haswa kwenye kibabu chake kinaitwa Wealth of a Nation ameelezea misingi inayopaswa kufuata ili kukusanya kodi yenye baraka kutoka kwa raia kwani kodi zenye malalamiko kama hizi hazina msaada kwa taifa watu wanawachukia.

Msidhani kwamba kukata kodi kubwa kwa watu ndio kuleta maendelea hapana mnazidi tuu kuleta chuki kati yenu na mnao waongoza na hiyo hela ta mkiipata hamtafanyia chochote kuweni na usawa. Nyie ni viongozi simamieni rasilimali za nchi sio kusimamia watu. Au mmetumwa kuwa viranja kwetu?

“taxation should follow the four principles of fairness, certainty, convenience and efficiency. Fairness, in that taxation should be compatible with taxpayers’ conditions, including their ability to pay in line with personal and family needs. Certainty should mean that taxpayers are clearly informed about why and how taxes are levied. Convenience relates to the ease of compliance for the taxpayers: how simple is the process for collecting or paying taxes? Finally, efficiency touches on the collection of taxes: basically put, the administration of tax collection should not negatively affect the allocation and use of resources in the economy, and certainly shouldn’t cost more than the taxes themselves”

Huyu waziri wa fedha mimi simjiu wala sijawahi kumuona ila asitumike vibaya kwenye system kama wewe umesoma tumia taaluma yako kwa weledi. Umepewa hiyo nafasi sio kwamba wewe ni bora kuliko wengine hapana. Umepewa hiyo nafasi kwa lengo kubwa zaidi ya wewe unavyo dhani. Kaa chini tafakari. Aliyekupa hayo mamlaka sio huyo aliye kuchagua.

Kuongeza kodi kwakigezo cha miradi ya maendeleo ni sababu gani hiyo wekeni wazi kuwa hamna ujasiri tena wa kusimamia madini, gesi na rasimimali zingine.

Kuwalimbikizia raia wenzako mzigo wa kodi ikiwa mali wamewapa msimamie ni udhaifu mkubwa sana. Unaacha madini na gesi unakata kodi kwenye miamala ya simu ili uendeshe nchi?
Kuwalimbikizia raia wenzako mzigo wa kodi ikiwa mali wamewapa msimamie ni udhaifu mkubwa sana. Unaacha madini na gesi unakata kodi kwenye miamala ya simu ili uendeshe nchi?" ,,.....HII LINE BORA SANA IKITUMWA KWA VIONGOZI HUSIKA
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!
HAKUNA MTANZANIA HADI HAPA ALIPO LEO HAJAWAI KULIPA KODI EITHER DIRECT OR INDIRECT ...sijui wewe unawazia makalioni?
 
Sijakuelewa
unataka kutegemea misaada hadi lini?
hujakua tu ili ujitegemee hata baadhi ya mahitaji yako ya muhimu?!
huku kulalamika ni tatizo la kuzoweshwa kunyonya wakati umri wa kuacha umepita!
sasa hatuna budi tujitegemee kwa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yetu na kizazi chetu.
wananchi wa nchi hisani wamechoka kila mara kutegemea kodi wanazo lipa wao, je? sisi watanzania hatuwezi? la hasha! ila bado tunadeka!!
 
Umeandika kitaalamu zaidi.

Mobile Money ilikuwa njia nzuri kwa Tanzania kuelekea "Cashless Society".

Hata mimi binafsi nilipendelea zaidi kulipa huduma kwa Mpesa. Ila kwa sasa kutumia Mpesa ni jambo la mwisho kabisa kuliwazia.

Narudi kwenye cash cash. Na bank account.
si sehemu zote bank services ipo nearby,sehemu nyingine ni zaid hata ya km kumi hasa vijijini,so sis tuliopo huku mjini tunajaribu kuwa kumbuka ndugu na jamaa zetu huko vijijini hata kwa vijisent kadhaa via mpesa,tigo,halo pesa etc lakini leo hii makato haya mbana yanakatisha tamaa sana
 
kinacholalamikiwa hapa leo sio kodi bali ni ongezeko lake....usilolijua wewe bichwa maji hakuna mtanzania ambaye hajawai lipa kodi...kodi inalipwa direct or indirect via various services.....USIWE KAMA POLEPOLE NDUGU fungua ubongo na tafakali kwa kina na si kukurupuka tu .....kwanza marekani haipo ulaya
kwa hiyo unapenda vya buree eeehh!!!
unataka usadiwe na mataifa ya ulaya eeeh!!!
kumbuka pia misaada tunayo ipata kutoka nchi za ulaya ni KODI ZA WANANCHI WA MAREKANI, UGERUMANI, DENMARK, NEWZELAND, FRANCE, CHINA, UINGEREZA N.K, wananchi wazalendo wa nchi hizo wanatozwa kodi ambazo zingine ndio tunapewa ss misaada na wakati mwengine tunakopeshwa.
acheni kuwa walemavu wa akili lipeni kodi ili itusaidie maendeleo yetu.
Taifa imara itajengwa na sisi watanzania wenyewe kwa kulipa kodi sio kutegemea misaada au mikopo.
 
unataka kutegemea misaada hadi lini?
hujakua tu ili ujitegemee hata baadhi ya mahitaji yako ya muhimu?!
huku kulalamika ni tatizo la kuzoweshwa kunyonya wakati umri wa kuacha umepita!
sasa hatuna budi tujitegemee kwa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yetu na kizazi chetu.
wananchi wa nchi hisani wamechoka kila mara kutegemea kodi wanazo lipa wao, je? sisi watanzania hatuwezi? la hasha! ila bado tunadeka!!

Nchi ulizotaja hazina rasilimali zozote. Hazinq madini wala mafuta. Wote vitega uchumi vyao ni huku kwa sisi tusiojitambua. Lengo sio kulipa kodi lengo ni kwamba kodi iwe na usawa. Kodi ambayo haina usawa ni haramu.
 
Maskini huwa hatazamwi,na wengi ndio tunafanya miamala na kundi ambalo ni wazazi ndugu na hata rafiki ambao % hali ni za kawaida kabisa.
Hizi takwimu za kikundi cha watu flani ndio kujumuisha kwa wote hapana aisee.

Waliopitisha hata hawawazi hilo.Misumari hii na kukanyaga haya makao ya moto ni sisi ndio tutaendelea kula msoto.

Tuendelee na utamaduni wetu wa sala na maombi ya kimya kimya.
Alfa na Omega atajibu siku si nyingi hawezi kubali wonyonge kama wanyonge kupigwa hivi mchana.
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!
Tunavyanzo vingi bikra kabisa vya mapato, sema viongozi wetu hawataki kuumiza vichwa, huu mziko kwa resources zetu ni kukosa viongozi wenye maono
 
Siku zote uvumilivu una mwisho wake na mwisho wa uvumilivu huwa maangamizo........

Mkusanyiko na mtiririko wa matukio kama haya unaofanywa na serikali dhidi ya raia wake ndio huzaa mioyo migumu iliyokwisha kata tamaa na hali halisi inayoonekana kuwa kumepotea matumaini......

Ni dhahiri kuwa watawala wamelewa madaraka na sasa wanatenda kwa utashi wao na sio kwa matakwa ya wananchi......kuendelea kukithiri kwa hali hii na watawala kuendelea kukaa kimya kunaashiria anguko kubwa sana siku za mbele......maana kusikia kwa kenge ni mpaka damu zimtoke masikioni.......

TIME WILL TELL......
 
Back
Top Bottom