Nna wasiwasi na huduma hizi (M-pesa, Zpesa, tiGO pesa & ZaP) 'mobile banking'.

Lakini ni afadhali coz wateja watarecover some kuliko kukosa kbc
 
Sawa ila deposit wapi sababu hata huko kwenye deposit mambo yakienda kombo ni yale yale
Afadhali Bank unaweza ukapata kitu kidogo, kampuni la simu likifilisika na pesa zetu ndo zimeenda... Nadhan tunahitaji SHERIA itakayoongoza makampuni haya na hizi huduma zao za kiujanjaujanja!
 
...mwisho wa siku benki ikiilisika ww huna pa kuzipata pesa zako isipokuwa utapewa fidia tu..wkt kwenye m-pesa kampuni ikifilisika ww hela yako bado unayo mikononi mwako.
Ndugu, kumbuka kwamba hela iliyopo kwenye LINE yako ya simu haina tofauti na hela uliyonayo kwenye ATM card yako... ukumbuke kwamba kampuni unapofilisika huwa inafilisika hadi shilingi ya mwisho na hakuna la kufanya (sheria yawalinda). Utachukuaje hela zako!? Hapa tungekua na upeo mzuri na kuyatambua makampuni haya kama yanatoa huduma za kibenki then walipe kodi inayostahili na kuwe na amount wanayodeposit B.O.T just encase!..
 
Good question aisee!.. Ukisha kufa inabidi ndugu zako wamchague mrithi then akadai, procedures zake sasa.....!

Hapa shida kubwa inayokuweko ni kuwa, waTanzania wangapi tuna utaratibu wa kuarifu ndugu zetu wa karibu kuwa kwa sasa nina TZS 1 Million kwenye M Pesa (kwa mfano). KIbaya zaidi, hata kwamba unakufa lini pia unakuta hujui. Ninachooona hapa ni kuwa ukifa (mara nyingi TZ na Afrika vifo vingi unakuta ni vya ghafla) hata hao ndugu zako wanakuwa hawana habari kuwa una pesa kwenye M Pesa. So, hata kama utaratibu upo practicability yake inakuwa ngumu kidogo. Wataalam watujuze!
 
Mkuu, Nnadhan nimekuelewa vizuri sana... Ila limitation ya transactions (1,000,000) ina limit transactions za mteja per day? Kama ndio hapo sasa ndipo tatizo linapotokea kwasababu hiyo haijalimit amount ambayo nnatakiwa kuwa nayo katika account yangu ya simu....Hii inamaananisha nna uwezo wa kuweka 900,000 kila siku kwenye account yangu ya M-pesa, Zpesa, tiGO pesa or ZaP?.. Inabidi tujue na hili pia!

Kama nimekuelewa vema, unachouliza ni iwapo unaweza kuwa na kiwango cha fedha hii kwenye huduma zote (M Pesa, Tigo Pesa na ZAP) kwa maana kuwa badala ya kuwa na limit ya TZS 1 Million ukajikuta umeweka 3 Million (kila service 1 Million), hii nafikiri inawezekana maana nijuavyo hii mitandao (huduma) haina interoperability. KIla mmoja yuko kivyake vyake.
Ila kama ulimaanisha kwenye huduma moja, mfano M Pesa, issue ni kwamba leo nikiweka 1 Million, nikizitumia zote sawa tu, kesho nitaweka tena 1 Million na kutumia zote bila shida (kumbuka msisitizo hapa ni huduma za ku transfer hela na kufanya malipo na sio savings). Ila kama jana nimeweka TZS 1 Million, kwa jana nikatumia TZS 100,000 zikabaki laki tisa, ina maana akaunti yangu itakuwa na room ya kuongeza kwa leo laki moja tu, ili ziwe million moja. Ila kwa kutumia, sina limit ya kutumia, nina uwezo wa kutumia hizo million moja zote kwa siku ya leo (maana ndizo ninazo kwenye akaunti yangu).
 
Kuna madaraja yanaitwa Tier 1 na Tier 2(naongelea m-pesa). Mteja wa Tier 1 maximum transaction anayoweza kuifanya kwa siku ni tsh laki 5 hii ni either kuweka au kutoa. Huyu mteja anakapofanya transaction zake zoote zikafikia 1.7 million(kutoa na kuweka kwa kipindi fln) inamwekea limit ambpo sasa atatakiwa kujaza fomu na kuhamishiwa tier 2 ambpo maximum limit ni 10 million km cjasahau.
Heshima yako mkuu, hizi tier ziko kulingana na mtumiaji. Kwa watu binafsi mimi na wewe ama ni shs laki tano ama million moja, kwa kitaalamu wanaita hizi ni P2P transactions (person to person). Kwa makampuni (au biashara) hizi ndio zinakuwa na limit kubwa, mfano malipo ya B2C (Business to ....nimesahau hapa) hawa wenyewe wanaweza kufanya transaction kubwa tu kwenye M Pesa. Of course unakuta wamelazimishwa kufanyiwa controls za kutosha. Mfano wa B2C transactions ni pale kampuni kubwa kama Coca Cola inapotumia M Pesa katika kusambaza vinywaji vyake. Wenyewe utaratibu wao unakuwa strict zaidi kuliko kwetu kwenye P2P.
 
Ni Kampuni ya pesa ikifilisika leo utaona kwamba agents wote wataacha kulipa wateja na pesa zitafia pale zilipo wale maagent watazingangania na wale waliotuma hawataweza kuzichukua tena na waliotumiwa watakuwa hawana sehemu ya kwenda kuzichukua.. Nothing is Full Proof mkuu
Kuna mambo mawili hapa, hii mifumo inatumia technology, transactions zote zinazofanyika ziko traceable (kuna audit trail). Sasa kampuni (kama vodacom mathalan) ikifilisika rekodi zake kuhusu fedha zilivyokuwa zinazunguka ndani ya system ziko kwenye system. Pia hizi zinakuwa mirrored kwenye akaunti ambayo kila huduma (kama M Pesa) imefungua kwenye one of the commercial banks. Kwa lugha nyingine, kila unachofanya kwenye M Pesa kinarekodiwa kwenye system za M Pesa na za kwenye benki yake wanayotumia, mfano CRDB. Kwa mantiki hiyo, Vodacom ikifilisika agent hawezi kung'ang'ania fedha alizonazo. Zile rekodi zitatumika kumfidia kila mtu kilicho chake. (hii ni kwa mujibu ya maelezo ya yule mtaalam wetu, nafikiri nimemnukuu sawa sawa). Asanteni
 
Great!!! Zinatakiwa zifanye deposit pia aise
The moment zikifanywa deposits maana yake M Pesa, ZAP na Tigo Pesa wanakuwa mabenki, maana ni mabenki tu ndiyo yanaruhusiwa (kisheria) kuwa deposit taking institutions.
 
Silence! ukituma ikafika, unamshukuru Mungu hayo mengine wandugu tunatafuta ugonjwa wa moyo.
Duh! Caroline, ndio umefunga mjadala? Hivi kweli huduma zao ni mbovu kiasi hicho? Mi nashukuru tangu zimekuwepo walau faida kubwa niliyopata ni kuepuka kupanga "foleni" masaa mawili mpaka matatu pale NBC Corporate Branch, just kutuma laki moja tu mkoani. Hizi huduma zinaweza kuwa na matatizo madogo madogo ya hapa na pale lakini pia umuhimu wake kwa jamii umeonekana. Anyway, ni mtazamo wangu huu
 
Haya makampuni kabla ya kuanza kutoa huduma hizi ni lazima wapate kibali toka BOT. Hivyo BOT wanafanya control yake, tatizo nnaloliona ni jinsi gani BOT wapo makini kufuatilia maana nakumbuka mambo ya meridian biao watz waliizwa
 
Kwa watu binafsi mimi na wewe ama ni shs laki tano ama million moja, kwa kitaalamu wanaita hizi ni P2P transactions (person to person).
Hapa cha msingi ni kukubaliana ya kwamba watu wanahifadhi hela zao huko!... Swali langu ni kwanini hawajaweka limited time ya fedha hizo kukaa huko... Kama walivyofanya NMB!???
 
Vodacom ikifilisika agent hawezi kung'ang'ania fedha alizonazo. Zile rekodi zitatumika kumfidia kila mtu kilicho chake. (hii ni kwa mujibu ya maelezo ya yule mtaalam wetu, nafikiri nimemnukuu sawa sawa). Asanteni
Mkuu, ukumbuke kwamba kampuni hadi inatangazwa kufilisika INAKUA HAINA HATA SHILINGI record za transactions kwenye computer zitakuwepo ndio, lakini physical money watakua hawana... Na mimi ninataka kujua serikali yetu inatulinda vipi na hatari hii!???
 
Haya makampuni kabla ya kuanza kutoa huduma hizi ni lazima wapate kibali toka BOT. Hivyo BOT wanafanya control yake, tatizo nnaloliona ni jinsi gani BOT wapo makini kufuatilia maana nakumbuka mambo ya meridian biao watz waliizwa
Of cause lazima B.O.T wawe wanawacontrol... swali ni siku hawa mabwana wakifilisika tutapona!??.
 
Ufanyaji kazi wa haya makampuni ya simu hautofautiani sana na ile iliyokuwa kampun ya DECI, ila ktk haya makampun ya simu kuna ki2 wakubwa wananufaika nacho so wameamua kuyafumbia macho huku yakiendelea kuvunja sheria tajwa hapo juu.
 
Ufanyaji kazi wa haya makampuni ya simu hautofautiani sana na ile iliyokuwa kampun ya DECI, ila ktk haya makampun ya simu kuna ki2 wakubwa wananufaika nacho so wameamua kuyafumbia macho huku yakiendelea kuvunja sheria tajwa hapo juu.
Ngoja siku moja lifilisike ndo watakaposhtuka!..
 
MKuu hili ni suala serious unajua? Naona kama watu wanalichukulia kimasiala!
 
Back
Top Bottom