NMB watangaza mgomo kushinikiza mafao

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
Posted Date::1/13/2008
NMB watangaza mgomo kushinikiza mafao
Na Salim Said, MUM
Mwananchi

WAFANYAKAZI wa Benki ya Taifa ya Biashara (NMB), wameazimia kufanya mgomo ukiwa na lengo la kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao kabla ya kuuzwa kwa hisa za benki hiyo.

Mgomo huo unatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya wafanyakazi 1,200 kutoka matawi yote ya NMB nchini.

Azimio hilo lilifikiwa jana baada ya majadiliano makali ya wafanyakazi hao katika mkutano wa wafanyakazi, uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 100 kutoka katika matawi mbalimbali ya NMB nchini.

Akisoma maazimio ya mkutano huo, Mwenyekiti wa Mkutano huo, Joseph Massana alisema wametangaza mgomo wa kitaifa wa wafanyakazi wa NMB kuanzia Jumatano ijayo ili kushinikiza serikali kama mdau mkuu benki hiyo, kuwapatia mafao yao kama walivyopatiwa wenzao wa benki nyingine.

Kama Katibu Mkuu wa TUICO taifa hatatupa majibu mazuri Jumatano hii, basi ndani ya saa 48 tunaazimia kutangaza mgomo halali wa wafanyakazi wa NMB, alisema Massana.

Awali Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani na Taasisi za Fedha (TUICO) Mkoa wa Kinondoni, Salim Katanga alisema, tatizo lao limeshafikishwa kwa serikali na kazi iliyopo ni kupambana na serikali ambayo haitaki kuwapatia haki zao.

Hakuna njia nzuri na ya haraka ya kupambana ili kupata haki zetu zaidi ya kuweka chini kalamu zetu. Serikali inatuhitaji basi ni wajibu wetu kuiambia kwamba inatuhitaji, alisema Katanga.

Naye Ali Kulunge ambaye ni mfanyakazi wa benki hiyo alisema inavyoonekana wanadanganywa kwani wao hawajaajiriwa na serikali, bali wameajiriwa na NMB.

Wafanyakazi hao pia wameazimia kufungua kesi mahakamani, kwa lengo la kutaka mfuko wa kukopeshana wa benki hiyo usimamiwe kwa ushirikiano baina ya mwajiri na waajiriwa tofauti na sasa ambapo unamilikiwa na mwajiri pekee.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom