SACO
JF-Expert Member
- Jul 25, 2011
- 2,877
- 3,789
Kama kichwa kinavyojieleza.. Ni kuwa mwezi wa Julai nilichukua mkopo NMB. Katika mkataba ni kuwa nitakatwa laki lakini baada ya makato kuanza nikagundua wanakata zaidi ya laki tatu, nilifika fasta kwenye ofisi zao za mikopo na wao walipoangalia kwenye compyuta zao wakagundua kama kuna kitu kama hicho. Hivyo wakaniambia nilete salary slip ili iambatanishwe na fomu watakayonipa.
Tatizo ni kuwa kwa sisi watumishi wa umma salary slip hazijatoka toka mwezi wa Juni, na nilipoenda kwenye ofisi za mishahara wakasema hawawezi kunipa document yoyote ya mshahara mpaka salary slip zitoke na benk wao wanasema hawawezi kunisaidia chochote mpaka nilete salary slip , hivi ninavyoandika ni kuwa jamaa wanaendelea kunikata hela kubwa tofauti na mkataba nilionao..... Kwa wale wenye uzoefu naomba mnishauri nifanye nini kutatua hilo tatizo?