Taasisi za mikopo Mungu anawaona... hususani NMB

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,825
Habari...
Kwanza kabisa baada ya salamu nianze kwa kudeclare interest

Mimi ni mwajiriwa wa serikali katika sekta ya elimu ngazi ya msingi au kwa neno la jumla mimi ni Mwalimu wa shule ya msingi

Pia nitoe angalizo kwa haya utakayoyasoma hapa chini yawezekana nikataja/ponda/sifu au hata nikauliza maswali lakini haiwi na maana kwamba napalilia mwingine ili kumshusha mwingine bali mimi naeleza ukweli wa kile nilichokumbana nacho mimi

Kwenye hoja yangu... ni kwamba kama ilivyo hakuna maendeleo bila mikopo basi nikaamua nikachukue mkopo ili nifanye mambo yangu kadhaa basi nikaenda NMB kuomba mkopo wa milion 3 na laki 1nikaambiwa nitakatwa 63000 kila mwezi kwa miaka 7! Nilimuuliza nakato akanambia wanakata asilimia 17

Lakini NMB huwa wanachelewesha sana yaani unaandika mkopo leo hela unawekewa pengine hata baada ya miezi mi3 (kwa maelezo niliyopewa na waliowahi kazini kabla yangu ambao wameshachukua chukua mikopo NmB) basi me nkaona niende kukopa kampuni inaitwa Maboto Enterprises ambayo inasifiwa sana kwa huduma zake bora nikakopa 1m na point ilikuwa mwezi wa tisa mwaka huu. Basi pale nikaambiwa nitalipa asilimia 20 riba nikasign mkataba na mshiko nikawekewa masaa kadhaa tu baadaye

Basi bwana mwezi wa tisa nikaanza kukatwa 156000 kama tulivyokubaliana kwenye mkataba kadhalika wa kumi nikakatwa kiasi kile kama kawaida (maana wao-Maboto huingiza kwenye system mojakwamoja)

...ilipofika mwishoni mwezi wa kumi mara naona sms kutoka nmb mobile kuwa nimewekewa fedha kucheki ni kiasi kile niliomba nilipoandika mkopo tangu mwezi wa nane-tisa. Basi nikafurahi sana maana sikutarajia wala kwanza mpaka naenda Maboto ni kwamba nilishakata tamaa

Sasa mshahara wa Nov ndo mambo yanapoanzia hapa ambapo ilibidi nikatwe 156000 ya Maboto kama kawaida na nikatwe pia 63000 ya NMB basi mshahara ukaingia kama kawaida sms imeonesha sh.135,553 nikapiga hesabu kweli nikaona ni sahihi kabisa

Nakumbuka ilikuwa tar23 nikachukua usafiri bana niende nikakatoe hako kasungura nijazie kwenye mambo yangu kufika kwenye machine natoa naambiwa salio halitoshi basi nikadhani labda nimekosea nikarudia tena bado nikaamua kupunguza kiasi nakumbuka hadi 80000 iligoma kutoka

Kwasababu ilikuwa jumapili nikashindwa kupata msaada pale basi nikaamua kumpigia simu yule meneja wa mikopo aliyenisainisha mkopo maana namba yake ninayo nikamuuliza tatizo lile akasema mpaka angekuwa pale ofisini ndo angeweza kulishuhulikia akanisihi niende siku ya kazi...

Sikuangalia salio nikaondoka kwa hasira maana siku ile nilipoteza muda sana pale nikawa kama nimevurugwa huku vi hiace kule stendi navyo vinakaribia kuniacha. Sikurudi tena pale bank na sikuwa na wasiwasi na lile swala kwakuwa ni la kimtandao na viambata vyote nilitunza. Nilikuja kutoa elfu70 ndo ikakubali na ndo kukawa empty kabisa kwenye akaunti

Kufika tarehe 2o mwezi huu tena kama kawaida sms -kiasi cha 135,553 kimewekwa nikaenda kutoa tena naambiwa salio halitoshi nikashangaa
Nikasema nitoe pamoja na ile ya novemba labda watakuwa wamefix pesa yangu ipo lakini ikagoma nikapunguza zaidi na zaidi lakini bado ikagoma. Kuangalia salio nakuta elfu 60 hakuna tena Hapo ndo nikapata wazo la kudownload bank statement

Stetment ilikuwa ya miezi mitatu from oct to dec basi hapo nikaona mchanganuo wote wa hela yangu inaonesha tarehe 23 nov iliingia 135553 na makato yote yameainishwa isipokuwa ya NMB kisha tarehe 27 nov ndo inaonesha nmb walikata chao lakini ni 58 elfu na point zake sio 63 elfu.

Hapo nikapatwa na bumbuwazi kidogo kwamaana tarehe 23 nilikuwa natoa hela naambiwa salio halitoshi lakini tar 27 kuna hela imekuja kukatwa!. Basi hapo nilikusanya kila kitu nikafunga safari mpaka benki nikamuuliza yule jamaa wa mikopo inakuwaje akasema...

Akanijibu "...ujue ndo juzi tu nimetoka kwa afisa utumishi kuchukua barua yako hii (huku akiitoa kwenye droo na kunionesha) tulikuwa tunafanya marekebisho ya mkopo wako maana kumbe ulikuwa na mkopo Maboto halafu hukuwa ukikatwa kwahiyo tulivyoingiza na huu wa kwetu kwenye system ndomana unaona mabadiliko hayo

Me nikaona ananichanganya kusudi nikamwambia maboto walishaanza kulipwa hela yao tangu mara tu nilipochukua mkopo kwao hata bank statement inaonesha ninayo hapa angalia... akasema nenda kalete salary slip ya Nov na Dec ili uone basi me nikamwambia siendi popote ngoja niidownload hapahapa nikadownload akasema nitumie nikamtumia kwenye email yake pale kazini

akafanyafanya anavyojua huko akanipa fomu ya kufanyiwa refund nikajaza akasema nisubiri ndani ya siku 3 za kazi wakishajiridhisha nitarudishiwa hela hiyo na ujumbe ukaingia kabisa kwamba asante kwa kuwasiliana na NMB na swala langu limepewa namba rejea kabisa sasa tangu tar 20 nikasema ngoja labda Christmas bado haijaisha vizuri basi leo ikabidi nimpigie tena kumuuliza anasema ametoka kidogo lakini akifika angeangalia tatizo nini maana yeye alishamaliza kila kitu kujaza ilibaki tu hela kurudishwa au taarifa tu ya kilichofanyika...

Jamaa yule ndo jumla hakuniambia chochote tena ikabidi nimtumie sms kwamba kama wanakwama anambie nijue nafanyaje lakini hakunijibu

Sasa hapa nabaki njia panda tu sielewi kwamba

afisa utumishi ndiye kachanganya taarifa zangu mpaka yanatokea yote hayo? Lakini hapana kwasababu mbona moja ya tatu ya mshahara wangu inasoma/inaingia kama kawaida- maana sheria inaruhusu ukope ukopavyo lakini uhakikishe theluthi ya basic salary inabaki

yule jamaa wa mikopo kuna anachonizungukalabda amevuruga yeyewakati wa kunisainisha mkopo given that mkopo umechukua muda sana mpaka kupewa lolote linaweza kujipenyeza katikati au

amenifanyia hivyo kwa makusudi na kuna faida anapata katika hiyo hali inayonikumba au vipi? Maana kuna walioniambia benki kuna wezi na wizi huo upo kwa namna anuai... lakini sitaki hata kumdhania hivyo kwakweli

inawezekana vipi salary slip inaonesha kabisa kwamba kuna kiasi hiki then kinapungua/zwa bila kuoneshwa sehemu yoyote -maana hiyo juzi kiasi kilichowekwa ni 135553 ilipokataa kutoka kuangalia salio nakuta elf 73 lakini slip natoa pamoja na statement zinaonesha ileile 135553

inakuwaje hela bado haijakatwa lakini ishindikane kutoka mpaka tarehe hiyo itakapokatwa- sawa tufanye hilo linawezekana lakini je...

inakuwaje nikatwe mara mbili tena amounts tofauti tofauti -kwenye salary slip inaonesha vyema 63000 lakini kwenye bank statement inaonesha elfu 58 na ushee ilikatwa tena baadaye

kama ni kosa la mmoja wapo kati yao je naweza kumchukulia hatua za kisheria kwa kuniingiza matatizoni-maana kwangu sidhani kama kuna kosa kwasababu nilienda pale kama mteja na nilimfafanulia kila kitu kwamba nataka mkopo lakini tayari nina mkopo Maboto akanipigia hesabu yeye mwenyewe kwamba itawezekana tu

hiyo 17% yenyewe mpaka kesho sielewi inakatwaje ni shida tu zinafanya nikubaliane bila kuhojihoji sasa bado machungu hayajatulia tena nachinjwa elf60 tena bila mpangilio- nakumbuka kwenye kuandika mkopo nilim'bana sana yule jamaa anifafanulie lakini alishindwa nakumbuka alinijibu tu kwa kifupi "tunakata 17% lakini tunatumia cumulative discount si kwa hivyo unavyofikiria wewe" hapo pia aliniacha ikabidi nifunike kombe tu

angalia Maboto mfano ambao wao ni asilimia 20 riba; unachukua mfano 5m maana yake utarudisha 6m na utakatwa laki kila mwezi kwamiaka mi5 yaani miezi 60 kwisha huna deni... lakini hiyo hiyo 5m chukua NMB wanaojidai kukata 17% riba dadeki uone makato yao kwa mwezi halafu uone utakatwa kwa miaka mingapi... sasa hapa ndo huwa sielewi nini shida ni kichwa changu na hesabu zake za msingi msingi au vipi

najikuta naona tena bora wale wa mikopo ya mkononi unapewa laki unarudisha laki mbili mkono kwa mkono japo riba yao ni kubwa 50% lakini unaelewa ukifanyacho kuliko huku unakatwa hela tu bila mpangilio wala maelezo hayaeleweki

Inawezekana nimeandika mengi sana lakini Mwisho niseme tu kwamba hapo mambo ni mawili tu la kwanza ni msaada juu kukatwa hela hiyo na la pili ni kueleweshwa namna NMB wanavyokopesha kwa riba ya %17 maana taaasisi zetu hizi zinazotukopesha funds huwa zina utaratibu unaotofautiana kwahiyo nisijekuwa nimekariri

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana.
Huwezi kusonga mbele bila kuumia.Mungu atakusaidia tu na utachomoka mdogo wangu.
Jikite ktk shughuli za kilimo na usindikaji wa mazao kama alizeti mahindi uza msimu wa shida pia hakikisha unatunza kwako siyo kwa mtu usije ukaliwa.
Angalia uwekezaji wa miradi ambayo unaweza ukaiwekeza na ukawa karibu nayo kwa urahisi wa usimamizi kama mashine,duka,air compressor machine and other related.
Usidharau kazi iheshimu itakutoa vizuri wewe yatumie vyema mazingira hayo kujikwamua.

Makampuni yote ya fedha yana unyonyaji ndani yake na tunakoelekea watu wataacha kukopa kwao.
Ukitaka kujua formula zinazotumika ni za hesabu za sequence and series amortization formula ambayo kwao inakuwa Sinking formula yaani unapewa mkupuo pesa nyingi ila unairudisha kwao kidogokidogo mfumo wa kabubu sinking .

Ukitaka kujua kanuni itumikayo nenda google andika Amortization formula in business kama una idea ya hesabu utaelewa vzr.

Asante KakaMkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu.. Ni vihela vidogo sana ila kwa uchumi wako ni kubwa, sasa umepata funzo mikopo si mizuri hata kidogo.
Pambana nao warekebishe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao jamaa ni kiboko ya masela.niliwahi kuomba mil 4 nikakaa miezi 3 hela haionekani.nakwenda kwa afisa mikopo nakuta kuna jamaa aliomba mil17,hela hawajampa ila wameanza kumkata.NMB ingeshajifia sema zabuni ya kupitisha mishahara inawabeba.
 
Hata CRDB wana upuuzi huo wanaanza kukufyeka kabla hujapokea hata pesa
 
Back
Top Bottom