NMB wana makato ya ajabu ajabu

Nikisoma nabadili maamuzi tu hata sijui nihamie bank gani ili nitulie. Nimeona wengi wanaongelea vizuri Equity Bank naomba kujuwa tu je wana App ya mobile unaweza kufanya miamala na kulipia kama hawa CRDB au NMB.
 
unawajua crdb wewe, wanakutoa chozi wale jamaa😀
Kuna siku nimetumiwa $114 crdb, nikashangaa kuna 134000, mpaka leo sijajua shida ilikuwa nini na wala sikwenda kuuliza.
 
1.BancABC visa cash card , unaweza kusave +online transaction hakuna makato ya mwezi

2.NMB chap chap mastercard , haina makato ya mwezi
 
1.BancABC visa cash card , unaweza kusave +online transaction hakuna makato ya mwezi

2.NMB chap chap mastercard , haina makato ya mwezi
Hiyo BANC ABC nimeshaacha kuitumia nilishakaa miezi miwili bila kupata huduma ya card maana natumia Visa Cash Card kwa ajili ya malipo na online transaction

Naona hawa wakenya wa Equity Bank ndo wapo active sana, yaani hata hela ikirudishwa kutoka Paypal inaingia direct kwenye account yangu ya bank
 
Suuh tatizo walikueleza ni nini hadi ukae muda wote huo?
 
Suuh tatizo walikueleza ni nini hadi ukae muda wote huo?
Walianza kutuma sms kwamba kutakuwa na maboresho kwenye mfumo wa kadi, hivyo nikajua ni swala la masaa sita, mwisho wa siku nikaenda mpaka kwenye tawi lao naambiwa mfumo wa kadi bado unafamyiwa marekebisho, ulivyokuja kukaa sawa nikafanya malipo then nikaachana nao
 
Kuliko kuweka Hela nmb heri kuchimbia chini ,mchwa wanaweza kukuhurumia lakini sio nmb!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…