NMB mawakala wenu ni tatizo

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,630
2,000
Nimepata taarifa za uhakika kutoka kijiji cha Lugarawa, wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, kuwa kuna wakala wa NMB mmoja maarufu kwa jina la Deo, amewaibia wateja wake kupitia biashara yake ya uwakala huo.

Story iko hivi, mteja akifika kutoa fedha benki, anaingiza kadi kwenye mashine kisha anamwambia mteja wake kuwa mtandao umesumbua. Atamtaka mteja arudie tena.

Kinachotokea hapo ni kutoa kiasi kilekile cha fedha kama alivyoomba mteja, halafu mteja anakabidhiwa fedha ya muamala mmoja tu.

Kwa mfano, mteja ameomba kutoa sh. 3m, basi itatolewa 3m kisha atarudia 3m, kisha mteja anakabidhiwa 3m tu.

Tukio hilo lilimpata mteja mmoja ambaye baada ya kufuatilia alitulizwa ili wayamalize. Mteja huyo anafuatilia arejeshewe jumla ya sh9m alizoibiwa kwa awamu tatu. Ufuatiliaji huo uliwafumbua macho wateja wengine na kuwafanya wafuatilie mwenendo wa akaunti zao na baadhi yao kugundua kuwa wameibiwa pia.

NMB chukueni hatua kuwaondoa mawakala kama hawa kwa kuwa si tu wanawaibia wateja, bali pia wanapoteza image nzuri ya taasisi yenu.
 

Devid01

Member
Jan 10, 2020
42
125
Hapo shida n wakala ko hata akibaili bank lakn wakala yule yule atafanya huo ujinga so Cha msng hap mawakala wanaofanya huo ujinga wasukumwe ndani.
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,410
2,000
Kwani huyo mteja alipotoa pesa kwa mara ya kwanza si aliweka namba yake ya siri? Na si alipata message kwenye simu au?
Kupata message hadi uwe umejiunga na bank mobile,so Lugalawa ni kijijini Sana njia ya kwenda Ludewa,wananchi wengi hawajajiunganisha na NMB mkononi .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom