yupo zake rwanda wanaita house arrest lakini wapi kafichwa anakula bata ndani kwa ndani,hiyo yote ni ili asikamatwe akatoa siri nani walimtuma kupigana vita ile
africa zaidi ya uijuavyo
kuna sehemu nimewahi kusoma historia ya vita ya drc wanasema laurent kabila aliwashirikisha rwanda na uganda katika vita ya kumpindua mabutu kwa ahadi ya kuwagawia mkoa wa kivu kuwa ni makazi ya wanyarwanda(kusini) na waganda-kaskazini. Baada ya jamaa kufanikiwa hakutekeleza hiyo ahadi. Jamaa wakaingiza majeshi yao kwa lazima kwa kisingizio cha kuwalinda wanyarwanda. Lengo lilikuwa kuteka ile miji iwe chini yao waendelee kuchimba madini. Baada ya kufanikisha zoezi la kumuua kabila inaonekana aliyepokea kijiti naye akawa mbishi. Inaonekana baadaye walifanikiwa kumshawishi jose kwamba yeye ni mtutsi hivyo anatakiwa kulinda maslahi ya wanyarwanda. Wakakubaliana kusitisha hujuma kwa kuudanganya umma kwamba nkunda amekamatwa na anashikiliwa na serikali ya rwanda. Kagame ni noma.
Kama alikuwa anapigana vita si ungetakiwa afunguliwe mashtaka?