Njozi ya rais wangu ajaye 2015-2020!

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Tanzania, nchi yangu niipendayo kwa moyo wangu wote. Ndio maana hadi leo pamoja na kutembelea nchi nyingi za wenzetu na kuona mengi ya kutamanisha, bado nimekomaa hapa hapa na sina mpango kuikimbia nchi yangu pamoja na matatizo yake yote. Nina imani bado kuwa iko siku itageuka na kuwa paradiso yenye kutamaniwa na walimwengu!

Tanzania, nchi yangu iliyonilea na kunipa tumani jema. Najisikia mnyonge sana pale ninapotazama utajiri wa mali na rasilimali tulizopewa na Mwenyezi Mungu, Jinsi mali hizi zilivyobakia kama maua mazuri yaliyochorwa daftarini tu Maua ambayo ni picha nzuri kutizamwa lakini haina maana kwa sababu ya kukosekana namna nzuri ya kumfanya kila mtu afaidike na utajiri huu.

Tanzania, nchi yangu ya ajabu na maajabu. Ninashindwa kuelewa tumemkosea nini Rabuka hadi tujikute katikati ya rindi la dhiki na umasikini ilhali Muumba katusheheni na utajiri wa almasi na lulu Tumekosea wapi hadi tusiione thamani ya neema inayotuzunguka? Najua na wewe wajua kuwa sote ni wana wa Tanzania. Najua nawe wajua kuwa Tanzania ni yetu wote. Nafahamu nawe wafahamu kwamba njaa haichagui wala haibagui.

Naamini ila sijui kama unaamini kwamba "uhai" wetu na vizazi vyetu tumekabidhi mikononi mwako ewe kiongozi uliyechaguliwa na wananchi. Uongozi ni dhamana na siyo ufahari. Uongozi ni dhamana inayotisha na siyo kulewesha. Uongozi ni mzigo na siyo lelemama. Iweje dhamana hii isikuogofye ewe kiongozi? Iweje isikunyime usingizi ewe mwakilishi wangu niliyekuchagua kwa kura yangu? Iweje ujisahau na usahau ahadi zako lukuki ulizomwaga siku unakampeni?

Ahadi ni deni na hivyo basi ujue unadaiwa! Dawa ya deni ni kulipaHakuna jinsi nyingine. Usipolipa wewe leo ujue kizazi chako kitadaiwa hata mbele ya Mungu! Ninaotea kwamba kiongozi wangu ajaye ameshajionea mengi kwa waliotangulia. Amesikia malalamiko na vilio vya wanyonge wa Tanzania.

Ninaamini kabisa kwamba anajua ufahamu wa watanzania ni mkubwa kuliko enzi zileeeeeeeeeeeeeeeeee Ninaamini kwamba watanzania nao "wamefundishika" vya kutosha mpaka hapa tulipofiikia. Natamani kiongozi ajaye awe mwenye uchungu na maskini wa Tanzania wasiokuwa na makazi ya staha...( nyumba bora), wanaoshindia mlo mmoja kwa siku, waliokosa tumaini la kuiona kesho.

Awe mwenye hofu ya Mungu Awe mwenye kupima ufanisi wa wale anaowateua kwa kipimo kinachoeleweka. Hili siyo shairi wala ngonjera bali ni mawazo yangu yanayonijia kila nikitafakari kuhusu nchi yangu Tanzania. Msinizodoea kwamba mbona hakuna vina na mazagazaga mengine.

Mwenye njozi zake naye amwage hapa ili baadae tuchanganye ................. wanaosikia wasikie. Kuna msururu wa wanaotaka urais 2015. Tunataka watusome wajue 2015 siyo lelemama. Hatutadanganyika kwa maneno yale yale ya enzi zileeeeeee, Tutajipanga sana na kuwabana.
 
Hmmm haya tutaona ila kwa jinsi niijuavyo miafrika sitegemei lolote lile. Muda utatueleza
 
Shimwe vijana popote mlipo tumekuwa tukiambiwa vijana ni taifa la kesho hiyo kesho mpaka lini? Nawaomba vijana wote ambao hawajajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wafanye hivyo wakati ukifika, kwani vijana kwa wingi wetu na akili zetu kwapamoja tukiamua tunaweza kuleta mabadiliko ya nchi hii.
 
tatizo sio kiongozi asiye na uchungu...

tatizo ni kiongozi mwenye skillz needed kwa kuongoza watu.......

tunahitaji Rais CEO anayejua kukusanya details na kusoma takwimu

sio hawa wanasiasa wanaojua kubwabwaja majukwaani.....

but mfumo tulionao, ma CEO hawako hata kwenye consideration ya watu....
 
nafikiri pia ni wrong kusubiri mabadiliko yaje na mtu mmoja

so ndo maana katiba mpya inaweza kuwa na majibu zaidi kuliko rais ajaye..
hasa kama kutakuwa na mgawanyo wa madaraka mzuri..
magavana
wilayani
halmashauri
n.k...

belgium wamekaa mwaka mmoja bila serikali kuu
lakini mambo yalikuwa yanaenda.....
 
Nadhani tatizo lililopo la sasa ni kubwa zaidi ya kiongozi, the all system stinks, kuanzia viongozi, watendaji, mpaka sisi wanajamii wenyewe, it seems hatuna uchungu na nchi yetu, na mbaya zaidi tumejijengea culture ya ajabu ya ufisadi na uvivu, kwahiyo tunawalea watoto wetu katika maadili ya ajabu ajabu, yaani sitaki kabisa kufikiria maadili ya wajukuu zetu kwa malezi haya ambayo tunawapa watoto wetu :(
 
tatizo sio kiongozi asiye na uchungu...tatizo ni kiongozi mwenye skillz needed kwa kuongoza watu.......tunahitaji Rais CEO anayejua kukusanya details na kusoma takwimusio hawa wanasiasa wanaojua kubwabwaja majukwaani.....but mfumo tulionao, ma CEO hawako hata kwenye consideration ya watu....
mimi nadhani tunahitaji watu na sio mtu tu mwenye skill set(s) za kuongoza, bali pia walio wabunifu na wenye uchungu na wenye uadilifu uliotukuka. Mimi napenda pia wawe wakali na wafuatiliaji wa mambo pia.
 
watu wanaweza kuwa corupt na bado wana knowlegde ya nini kifanyike
kuondoa umasikini na wakafanya kazi

mfano ni south korea
marais watatu wamepelekwa mahakamani kwa rushwa
wawili wako jela....
but still south korea sio tanzania
 
mimi nadhani tunahitaji watu na sio mtu tu mwenye skill set(s) za kuongoza, bali pia walio wabunifu na wenye uchungu na wenye uadilifu uliotukuka. Mimi napenda pia wawe wakali na wafuatiliaji wa mambo pia.

mtu anaweza kuwa na uchungu na muadilifu
lakini hana uwezo wa kubadilisha hali iliyopo
wa nini huyo mtu...

usisahau management na leadership
kuna skills na talent pia......
 
Nadhani tatizo lililopo la sasa ni kubwa zaidi ya kiongozi, the all system stinks, kuanzia viongozi, watendaji, mpaka sisi wanajamii wenyewe, it seems hatuna uchungu na nchi yetu, na mbaya zaidi tumejijengea culture ya ajabu ya ufisadi na uvivu, kwahiyo tunawalea watoto wetu katika maadili ya ajabu ajabu, yaani sitaki kabisa kufikiria maadili ya wajukuu zetu kwa malezi haya ambayo tunawapa watoto wetu :(

mkuu generalization pia sio nzuri
mimi naamini hata ndani ya ccm wapo wenye uchungu na uadilifu
na hata ndani ya chadema kuna corrupt leaders...

tatizo ni mfumo unaotegemea zaidi mtu mmoja
tunahitaji mfumo ambao rais atawajibishwa na atapewa
guideline ya nini anatakiwa kufanya na nini haruhusiwi kufanya
 
Komredi ukipewa kacheo vp utaibadilisha khali ya miafrika ndivyo ilivyo?
hakika komredi ila sidhani kama ntaishi muda mrefu baada ya hapo maana ntakuwa mnoko sana na rasilimali za walipa kodi. Mambo ya ma-vx na sijui allowance zisizo na kichwa wala miguu yatakuwa nehi nehi. Tutahakikisha hakuna mwanetu hata mmoja anayesomea chini ya mbuyu au mgonjwa anayelala sakafuni huku mawaziri husika, kwa mfano, wakitanua kwenye ma vx
 
tatizo sio kiongozi asiye na uchungu...

tatizo ni kiongozi mwenye skillz needed kwa kuongoza watu.......

tunahitaji Rais CEO anayejua kukusanya details na kusoma takwimu

sio hawa wanasiasa wanaojua kubwabwaja majukwaani.....
but mfumo tulionao, ma CEO hawako hata kwenye consideration ya watu....

Boss,
Rais Tanzania siyo executive President hivyo hatuwezi kumtegemea "kutenda" kiviiiile. Anachopaswa kufanya ni kuhakikisha the right people are in the right positions basi.Kinachofuata baada ya hapo ni kuwa monitor. Tatizo ninaloliona kwa nchi kama yetu ni "uwajibikaji" wa wale walioketishwa vitini kwenye bus. Kwanza je dereva anajua basi linaenda wapi? Akishajua ahakikishe waliomo ndani ya bus wanakubaliana na safari yenyewe.IF NOT basi kutakuwa na utata kwenye safari na kila mara itabidi ama aburuze bus au asimame kila mara na kuchelewesha safari!Hata baada ya safari inabidi from time to time kufanya ukaguzi kuona kila kitu kiko sawa.Je haya yanafanyika? au tunaburuta bus weeee hadi tunafika na kugundua mbona njia siyo?!Hapo tushapoteza muda, mafuta, tear and wear ya gari, etc!

dadangu, hayo mabadiliko kama yapo basi ni kiduchu sana na hivyo kupelekea kuonekana kama hayapo.

Haba na haba siyo haba mbili NN! LOL

nafikiri pia ni wrong kusubiri mabadiliko yaje na mtu mmoja

Kweli kabisa. Ila kwa mukhtadha huu, wale critical kwenye team ya uongozi hutegemea mtu mmoja!
so ndo maana katiba mpya inaweza kuwa na majibu zaidi kuliko rais ajaye..
hasa kama kutakuwa na mgawanyo wa madaraka mzuri..
magavana
wilayani
halmashauri
n.k...

Uko sahihi kabisa.Katiba ya sasa inatoa mwanya wa kuzembea uwajibikaji karibu katika kila muhimili wa dola.Chukulia mfano mahakama, pamoja na kuwa huru "independent" haimaanishi kutokufanya kadri ya matakwa ya wananchi. Haki itendeke na siyo izuiliwe.Jaji au hakimu hawezi kutokuandika hukumu au kuchelewesha kwa kisingizio cha "uhuru wa mahakama". Au Executive kuteua watu wasio competent just because wako ndani ya chama chake na considerations nyingine! Huenda kwa vile viongozi wanatokana na wabunge tena wa chama fulani basi hujikuta kafungwa na hali hiyo. I can imagine kama Katiba ingerehusu wagombea binafsi labda CEOs kutoka private sector wasiotaka siasa za vyama wangeweza kugombea ubunge na hatimaye kuweza kuchaguliwa kuwa mawaziri.Huenda tungeona maendeleo ya kasi zaidi kuliko sasa.

.

Nadhani tatizo lililopo la sasa ni kubwa zaidi ya kiongozi, the all system stinks, kuanzia viongozi, watendaji, mpaka sisi wanajamii wenyewe, it seems hatuna uchungu na nchi yetu,

Kweli kabisa VOR!
Tatizo ni systemic. Miaka ya nyuma watu walikuwa hawavutiki sana kutaka kufanya kazi serikalini kwa vile mishahara ilikuwa midogo na hata marupurupu hayakuwepo.Sasa hivi watu wanafanya kila mbinu kutaka ajira serikalini.Kwanini? Mfumo wa utendaji kwanza hauna mifumo ya kupima na kutathmini ufanisi ( not results based). Hata kama hufanyi kazi kwa kiwango hakuna consequences.Pia kumejengeka 'reward system' ambayo siyo formal lakini imeshakuwa a culture - posho za kila aina huvutia watu kuwemo humo.Nadhani hata ile OPRAS haifanyi kazi na kama inafanya basi ina walakini mkubwa sana.

na mbaya zaidi tumejijengea culture ya ajabu ya ufisadi na uvivu, kwahiyo tunawalea watoto wetu katika maadili ya ajabu ajabu, yaani sitaki kabisa kufikiria maadili ya wajukuu zetu kwa malezi haya ambayo tunawapa watoto wetu
:(
Hili ni jambo la kuogopesha sana ndugu yangu!!
 
Wahusika to date amba ndio very likely kua viongozi bado hamna hata mmoja
mwenye qualifications za kuweza fanya hayo unayotazamia... qualifications pia
inaweza onekana sio neccessary the most important aspect ni UZALENDO...
Unfortunately hatuna viongozi ambao kweli ni wazalendo... inaumaa...
Na kama you are talking about 2015 then hapa ni CCM Vs CDM... woote wanasiasa tu!
Uki observe CCM wao sasa ni ubabe ubabe.... whereas CDM ni kukuza jina...
Hio hata waje chama kingine ndani ya nyumba, Mtanzania wa kawaida life
itakua ile ile hamna kitacho badilika (IMO) Ila tu kitacho badilika ni viongozi wa
former Leading party kutiwa kashi kashi mpaka wajute!!!
 
mtu anaweza kuwa na uchungu na muadilifulakini hana uwezo wa kubadilisha hali iliyopowa nini huyo mtu...usisahau management na leadership kuna skills na talent pia......
ndo maana nikasema watu na nikasema wawe wabunifu (innovative & resourceful)
 
Nadhani tatizo lililopo la sasa ni kubwa zaidi ya kiongozi, the all system stinks, kuanzia viongozi, watendaji, mpaka sisi wanajamii wenyewe, it seems hatuna uchungu na nchi yetu, na mbaya zaidi tumejijengea culture ya ajabu ya ufisadi na uvivu, kwahiyo tunawalea watoto wetu katika maadili ya ajabu ajabu, yaani sitaki kabisa kufikiria maadili ya wajukuu zetu kwa malezi haya ambayo tunawapa watoto wetu :(

Mfano mzuri saana ni wanafaunzi wa vyuoni... migomo kila siku but always
wakililia posho zao or anything related to their needs... huwezi sikia kua wanafunzi
wa UDOM or UDSM wamegoma baada ya kugundua jamii fulani imeonewa ili or lile...

Na kikubwa ikumbukwe kua Viongozi wa jana ni wanafunzi wa Juzi, Viongozi
wa leo wanafunzi wa jana thus wanafunzi wa sasa viongozi wa leo... it seems as if we are doomed...
 
mkuu generalization pia sio nzuri
mimi naamini hata ndani ya ccm wapo wenye uchungu na uadilifu
na hata ndani ya chadema kuna corrupt leaders...

tatizo ni mfumo unaotegemea zaidi mtu mmoja
tunahitaji mfumo ambao rais atawajibishwa na atapewa
guideline ya nini anatakiwa kufanya na nini haruhusiwi kufanya

The Boss hapa wale wano run show ndio hao ambao tunalenga....
wewe kama kiongozi kweli na ni muadilifu, yaani hamna means kabisa
ya wewe kuleta change hata to a small extent?? na ionekane na jamii?
 
Back
Top Bottom