Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 14,621
- 35,353
UZI WA VAYOLENSI; Njoo utoe makavu kama unayo!
- Kama wewe ni mwanamke usiyejishughulisha, maisha yako yanategemea kudanga au kuomba omba wanaume hela - jua unatumia kikojoleo chako kama shughuli ya kiuchumi na huna tofauti na changudoa anayejiuza barabarani, .
- Kama wewe ni mwanaume unayejali zaidi mawazo, fikra na namna anavyoonekana na rafiki zako wa kiume kuliko mke wako na familia yako - jua una chembechembe za tabia za wanaupinde, jitathmini.
- MwanaJF unayetukana na kukebehi wengine pale unapokosa hoja au jibu lenye mashiko, hasa chawa wa CCM na CDM kwenye nyuzi za siasa - jua wewe ni hamnazo.
- Kama wewe ni Mwanamke / mwanaume unayesifia matumizi ya mihadarti au ulevi (unywaji wa pombe kupita kiasi) na unakuja kujisifia humu jukwaani - tunakuonea huruma maana wewe ni mgonjwa usiyejijua bado.
- Kama wewe ni Mwanaume unayehonga hela kwa michepuko na vibinti vidogo wakati hajatimiza mahitaji ya msingi kwa watoto wako - jua wewe ni takataka ya hovyo sana.
- Kama wewe ni mwanamke unayekopa hela ili ujionyeshe kwa kuvaa vitu vya thamani ambavyo haviko kwenye uwezo wako kiuchumi - jua wewe ni limbukeni na badilika.
- Kama wewe ni mwanaume unayeshupaza shingo kusema single mothers wakati umezalisha watoto na wanawake tofauti na huwahudumii - wewe ni hayawani usiyejitambua.
- Endeleza na nyingine .......................🤷♀️