Njoo uniunganishie dot tafadhali

Njoo uniunganishie dot tafadhali

Apologise lady

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2013
Posts
5,980
Reaction score
3,115
Ni hivi jirani yangu aliibiwa simu siku ya jumapili, wakati anafanya shughuli zake aliingia ndani akaacha sim nje kwa kuwa ni sehemu ambayo haina wizi wizi hakuwa na shaka, kuja kutoka nje kakuta sim ishapitiwa, ikatafutwa haikupatikana, mama yule akaondoka taratibu hadi kwa mganga siku hiyohiyo.

Yakafanyika yakufanyika mganga akamwambia rudi nyumbani ndani ya siku 7 utapata simu yako, mama yule akarudi kimya kama kaisahau simu yake, jambo la ajabu leo hii asubuhi mme wake anaamka kujiandaa kwenda kazini anakuta simu mlangoni, ndio kuita watu kwa furaha.

Sasa naomba mniunganishie dot,  kuna connection gani ilifanyika kati ya mganga na mwizi hadi simu ikarudi? Bado nina mshangao wa ajabu, mara zote naamini waganga ni waongo na hutumia mchezo wa kisaikolojia zaidi kumwahadaa mtu.
 
Uyo ni mganga au mtaalam? Safi taaluma yake inaweza ikawa sahihi!!
 
Ndio maana siamini kwenye nguvu za giza.

Full kudanganyana.

Kama umeibiwa simu basi mtafute mwizi, ukimkosa basi nunua nyingine.

Ila hii ya kwenda kwa mganga ni kujidanganya.
 
mie O level nimesomaga huko bush, wakati nasoma kuna dada
mmoja tunakaa hosteli next room akaibiwa vistiker sijui na vitu gani vingine
hata sikumbuki akasema anaenda kwa mganga huyo mganga eti
akasema mimi ndio nimeiba Dah, wakati hata sikuwahi kuiba wala kujua vikoje
alinisababishia mfadhaiko mbaya.....
 
mganga kutoka sumbawanga tunatoa huduma zifuatazo~kusafisha nyota ,kurudisha waliopotea,kuzindika ma bwana za watu,chuma ulete ktk biashara na kuwa na mvuto kimapenzi Kwa wanawake.
 
Wachawi wapo tena Sana, wanga wapo tena kila mahali matapeli pia wapo na hubahatisha... Nimekaa kwenye hii fani nikajifunza vyote nikapractice tena kwa kufanya colabo ya uchawi na supernatural powers, nikakumbana na vitisho na vigagula hasa kwenye fani
Wachawi wa kweli Wanatumikia nguvu wasizomiliki na chochote kinachopatikana si chao wao ni mawakala tuu na ndio maana huwa maskini wa kutupwa
 
Umbali toka kwa kada wa ccm na huyo mganga ukoje??

Ila hii hadithi inazidi kunithibitishia kuwa miCCM inaendekeza sana ushirikina.
 
mie O level nimesomaga huko bush, wakati nasoma kuna dada
mmoja tunakaa hosteli next room akaibiwa vistiker sijui na vitu gani vingine
hata sikumbuki akasema anaenda kwa mganga huyo mganga eti
akasema mimi ndio nimeiba Dah, wakati hata sikuwahi kuiba wala kujua vikoje
alinisababishia mfadhaiko mbaya.....

Unakumbuka siku ile uliponiibia boxer yangu gesti?
 
Umbali toka kwa kada wa ccm na huyo mganga ukoje??

Ila hii hadithi inazidi kunithibitishia kuwa miCCM inaendekeza sana ushirikina.

Kwakua nilikuwa natoka sikupata muda wakumdadis vizur, ila nikirudi nitamuulza ili anipeleke siku ukiniudhi nikugeuze popo
 
Ngoja na mimi najaribu kuunganisha dot.

Ni hivi…… Wewe Apologise lady kuna jambo linakutatiza hapo ulipo, huoni solution kama njia ya kuliebuka, unasita kwenda kwa sangoma kuhofia utatapeliwa au kusutwa na nafsi baada ya kwenda kwa kuwa una mashaka. Kwahiyo mada yako hii umeileta ili kupima maoni ya watu kama huko u.nakotaka kwenda(kwa sangoma) kuna uhakika wa kupata ufumbuzi au lah.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom