Who Cares?
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 3,507
- 3,378
Hakuna tikiti linalojenga sukari kwa kiwango sahihi ndani ya hizo siku tajwa.Sisi tunalima hybrid ndani ya usiku 56
napata sh ngapi uwii nije au ushamaliza kugawa mkuuSh.80,000 kukodi mkuu
umemaanisha kuwa tunadanganywa ama nini? what do you meanMkionyesha uitikio ntarudi kumalizia makisio ya gharama na kipato kwa ekari moja ya tikiti. Kumbukeni hesabu haidanganyi ila uhalisia wake hukamilishwa zaidi endapo utazingatia JUHUDI na MAARIFA.
CC Angelaone Mulhat Mpunga Baba yenu Konda wa bodaboda etc
Nakusubiri mkuu...Mkuu laurentie hongera kwa kuwahamasisha raia kuhusu kuzikamatia fulsa zilizopo shamba!
Mimi ni mkulima mzoefu wa mazao karibu yote ya bustani.
Nimesoma na kujionea picha zako ulizo bandika hapa;
Zipo kasoro nyingi sana nimeziona kwenye hili bandiko. Ningependa kuweka masahihisho ya jumla iwe kama tahadhari kwa wale waliovutiwa na huu uzi hatmae kuja kufanya kazi.
1) Ipo kasoro kwenye upandaji wa hizo tikiti. Umepanda kienyeji sana. Upandaji wako utaathiri huo mmea kipindi cha umwagiliaji maji hasa kwa hiyo hybrid(zebra)
2) kuna mapungufu katika uainishaji wa gharama za uendeshaji. Kwanini huwi realistic kuchambua hatua kwa hatua mpaka mavuno.
Nk nk nk
Nikipata muda, ntatoa mchanganuo wa upandaji, cost na kipato halisi kwa ekari moja ya tikiti ili kuwarahisishia watakaovutika kuingia kwenye sekta hii na hatmae wajue mbivu na mbichi kuhusu kilimo.
Hapana, fuatilia mtiririko wa uzi vizuri. Nipo hapa kuboresha pale aliposahau mleta mada make wadau wamehitaji ufafanuzi zaidi wa uhalisia wa hiki kilimo.umemaanisha kuwa tunadanganywa ama nini? what do you mean
Hongera sana mkuu. Wewe ni mdau mhimu sana kwangu. Siku zote kwenye biashara tunategemeana pande zote mbili. Endapo upande mmoja ukikiuka vigezo na viwango, lazima hasara itatokea upande mmoja. Nipo tayari kufanya kazi na mtu anaejali muda na rasilimali make ndo mwanzo wa kufanikiwa.Mimi ni mfanya biashara wa matunda hususani hayo matikiti maji, lakini nifanyacho mimi ni ulanguzi...
Nimefurahi kukutana na uzi huu, kwa yoyote anaehitaji trading partner naomba anijurishe, nahitaji sana mtu ambae ni mwaminifu hawezi kuniuzia bidhaa zitakazonipa hasaraa
300000+100000+80000+240000+80000= so total ni laki nane sio?Inaendelea...
5)Makisio ya gharama kwa ekari1 ya tikiti.
Kama nilivyosema mwanzo, endapo miundombinu ya umwagiliaji ipo vizuri na ukitumia waterpump 3" hp5.5( cost yake ni sh300,000) deliverypipe 50metres(sh 100,000) inlet pipe(price cost per ft sh15000 i.e ft6=sh80000)
Shamba la ekari1 litamwagiliwa kwa tanki2 lenye ujazo wa 3litres(total 6litres) so cost/acre/whole period 2000sh*6litres*{20'}= sh 240,000(hii ni gharama ya petrol) nb {20'} ni idadi ya awamu za umwagiliaji wa shamba toka kupanda hadi kukomaa kwa tikiti siku ya 75.
6) Gharama za mbegu na viuatilifu;
Bei inatofautiana kulingana na sehemu na aina ya mbegu.
Hybrid SukariF1 ama SugarQueen kopo la gram500 lina range kuanzia sh250,000-270,000/- ambayo ndani yake kuna karibu punje4000. Inatosha kwa ekari1 ila itakulazimu uwe na mbegu ya dhiada endapo mashimo mengine hayataota.
7)gharama ya viutilifu: fungiside ridomily au ebony kilo1 sh40,000 kwa ajili ya ukungu
Insectside blasty kikopo cha mil500*10*sh8000=80,000.
Dawa ya panya pia mhimu.
Hongera sana mkuu. Wewe ni mdau mhimu sana kwangu. Siku zote kwenye biashara tunategemeana pande zote mbili. Endapo upande mmoja ukikiuka vigezo na viwango, lazima hasara itatokea upande mmoja. Nipo tayari kufanya kazi na mtu anaejali muda na rasilimali make ndo mwanzo wa kufanikiwa.
Tuungane maana tunategemeana.
Nakukaribisha sana na nipo tayari kufanya kazi na wewe endapo uaminifu utazingatiwa kama ulivyotangulia kusema.
Karibu sana.