Njombe: Mama kujifungulia nyumbani faini Tshs 30,000/=?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
IPO risiti ya halmashauri inazagaa mitandaoni ikionyesha malipo faini ya 30,000 kwa kosa la kujifungulia nyumbani.

Naomba kufahamishwa, hii faini ni kwa mikoa yote nchini au ni Njombe pekee?

Je, kujifungua mwanamke lazima apatwe na uchungu hospitalini?

Je, akipatwa na uchungu akiwa nyumbani na hakuna kituo Cha afya karibu aache kujifungua Hadi afike hospitalini?

Huyu Mkurugenzi, DC, RC na madiwani wanaosimamia hizi faini kwanini wasishtakiwe?

Kwanini wanasiasa wa awamu hii wanaamini kuwanyonyo wananchi kupitia sheria na kanuni za kinyonyaji zisizo na utu?

Chama cha WANASHERIA wanawake haya mnayaona? Watu wa Halki za binadamu haya mnayaona au mmekaa huko DSM mnakula viyoyozi?
 
Ni sawa kumchaji 30k?
Mpaka ikawekwa nadhani kuna watu walikuwa wanafanya kusudi (yaani tu hataki, binadamu wa aina hii ni wengi tu).

Na sidhani kama huwa inatozwa kwa iliyotokea bahati mbaya ila ni kwa wale wa makusudi.

JAPO SINA UHAKIKA NA SIJUI KAMA HUWA INATOZWA.
 
Pakujifungulia hauwezi kupachagua kama una kubali kuna na watoto njiti. Ila Tukimchagua Lissu hizi tozo za ki CCM ( Chanzo Cha Matatizo) hazitakuwepo tena. Usisahau Kumchagua Lissu Tafadhali!
Mtoto njiti hii tunaweza iita ajali nje ya uwezo wa kibinadamu.

Hakuna kiumbe mwenye roho hiyo ya kukutoza faini kwenye hali kama hii.

Kwa uelewa wangu hii imewekwa kuwafanya watu wawe makini, wakajifungulie hospital ili kupunguza vifo vya Mama na mtoto.
 
Hiki nacho kinaitwa chanzo cha mapato?
Hii si sawa, wahusika wachunguzwe.
 
Mkuu inatokea sana tu watu kujifungulia nyumbani na si kwa kupanga bali kujifungua huja kwa namna nyingi tu. Kwa mfano mama kijacho kuambiwa due date ni tarehe fulani na mtoto akaja wiki mbili au hata tatu kabla ya due date.

Mtoto njiti hii tunaweza iita ajali nje ya uwezo wa kibinadamu.
Hakuna kiumbe mwenye roho hiyo ya kukutoza faini kwenye hali kama hii.
Kwa uelewa wangu hii imewekwa kuwafanya watu wawe makini, wakajifungulie hospital ili kupunguza vifo vya Mama na mtoto.
 
Mkuu inatokea sana tu watu kujifungulia nyumbani na si kwa kupanga bali kujifungua huja kwa namna nyingi tu. Kwa mfano mama kijacho kuambiwa due date ni tarehe fulani na mtoto akaja wiki mbili au hata tatu kabla ya due date.
Kwa hao mkuu Sidhani kama wanatozwa (ila nna asilimia nyingi wao haiwahusu)

Sababu kama anahudhuria clinic watampa zile tarehe. Ila kama ikatokea tofauti na hapo mtu ajieleze ataeleweka.

Mkuu wewe ulikuwa unashauri ambao wanafanya kusudi wafanywaje?
 
Mtoto njiti hii tunaweza iita ajali nje ya uwezo wa kibinadamu.
Hakuna kiumbe mwenye roho hiyo ya kukutoza faini kwenye hali kama hii.
Kwa uelewa wangu hii imewekwa kuwafanya watu wawe makini, wakajifungulie hospital ili kupunguza vifo vya Mama na mtoto.
Viumbe wenye roho mbaya namna hii wapo, na ndo kama hawa watawala, ambaye anadiriki kukuambia hatakuletea maendelea ukichagu asiyempenda na bado kila siku anakugongea mlangoni anataka kodi
 
Una ushahidi kama wanafanya kusudi?

Kwa hao mkuu Sidhani kama wanatozwa (ila nna asilimia nyingi wao haiwahusu)

Sababu kama anahudhuria clinic watampa zile tarehe. Ila kama ikatokea tofauti na hapo mtu ajieleze ataeleweka.

Mkuu wewe ulikuwa unashauri ambao wanafanya kusudi wafanywaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom