Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Sikuona shida kurudi Kijijini kumhudumia Mama mkwe, alikua Mzee sana na kutokana na umri wake na hali yake alikataa katakata kuja Dar. Kisingizio chake ilikua hataki kutupa hasara ya kubeba maiti, mume wangu aliponiambia nilimuelewa, kwanza mimi pekee ndiyo nilikua sifanyi kazi ya kuajiriwa, watoto wake wote wakike walikua wakifanya kazi na wakiume pamoja na wake zao walikua wanafanya kazi hivyo sikuona sababu hata yakubisha.
Sababu nyingine tena kubwa ya kwenda kumhudumia ni kutokana na roho nzuri ya Mama mkwe wangu, katika maisha yangu sijakutana na mwanamke mnyenyekevu na mwenye roho nzuri kama yeye, hata Mama yangu mzazi pamoja na kumpenda sana lakini kama nitakua mkweli kwa Mungu alikua hamfikii hata robo Mama mkwe wangu hivyo kwangu niliona kama fahari kwenda kumuuguza.
Mume wangu alinipeleka kwa gari yake, hii ilimpa fursa ya kumuangalia Mama yake pia alitaka kuona wajukuu zake, hivyo tuliona kwakua wote wako shule basi tuende nao akae nao siku mbili kisha mume wangu arudi nao. Tulienda na kumsalimia, alifurahi sana na kama kawaida yake asivyo na makuu alishangaa ni kwanini naacha kazi zangu mjini na kurudi kijijini kumhudumia yeye. Nilimuambia sina kazi na hata kama ningekua na kazi basi yeye ni wa muhimu kuliko kazi yenyewe.
Mume wangu alikaa siku mbili na kuondoka, aliniacha pale na Mama mkwe, baada ya mume wangu kuondoka maisha yaliendelea, hali yake haikua mbaya sana, kubwa lilikua ni uzee na miguu alikua hawezi kunyanyuka na kutembea hivyo alikua ni mtu wa kukaa tu na kusaidiwa mambo mengi. Lakini kiuhalisia bado alikua na ka afya kidogo na hakua na maumivu sana. “Umesema hufanyi kazi, wewe si msomi mwanangu? Si mlikutana na mumeo huko chuo kikuu?”
Siku moja aliniuliza, nilishangaa kwani suala la kufanya kazi tulilizungumzia kidogo tu tena kama utani, sikujua kama atalichukulia siriasi. “Ndiyo ni msomi lakini Baba Jesca hataki nifanye kazi, nilikua nafanya nikaacha sasa hivi nalea waototo.” Nilimjibu harakaharaka na kuleta mada nyingine, sikutaka kulizungumzia hilo swala kwani hata mimi nilikua naona aibu kuitwa msomi halafu sifanyi kazi. “Hataki, kwahiyo unakaa tu asubuhi mpaka jioni?”
Aliniuliza ni kama hakutaka hiyo mada iishe, nilijaribu kuu ibadilisha lakini alikazania. Ilibidi kumuambia ukweli namna ambavyo mume wangu aliniachisha kazi. Nilimuambia nilikua nafanya kazi nzuri ya kipato kizuri tu lakini nilipopata ujauzito na kujifungua mume wangu aliniambia niache kazi ili kulea mtoto na taratibu nikijua niarudi nilijikuta tayari nishafikisha watoto watatu na kazi sina hivyo nikaridhika na kuwa Mama wa nyumbani. “Lakini sasa hivi watoto wamekua wakubwa, si urudi kazini?”
Aliniuliza lakini sikua na jibu, nilimuambia mwanae hataki watoto wake walelewe na Dada wa kazi, alishangaa na kuniambia kama hataki mbona sasa hivi wanalelwa. Nilinyamaza kwani sikua na jibu, sikutaka kuendelea kuiongelea ile mada kwani niliona kama vile hataki mimi kukaa tu.
Nilianza kuhisi vibaya labda anaona kama namtia hasara mtoto wake waka kuwa kula kulala tu. Kwa mara ya kwanza nilianza kuona upande wa pili wa Mama mkwe wangu, tangu siku ile ni kama alibadilika flani na kuwa mtu mpya kabisa.
Hakua na raha tena, nikama alikua na wasiwasi na kitu flani, nilijaribu kuwa mchangamfu na kusahau mambo lakini hakusahau. “Lakini anakushirikisha katika vitu vyake, mnafanya mambo pamoja?” Aliniuliza siku nyingine, sikumuelewa kama anamaanisha nini lakini nilijibu ndiyo. “Nasikia ana biashara, unaijua lakini?
Unajua namna ya kuiendesha?” Aliniuliza, sasa nilijua kama ananidodosa kuona kama najua mali za mwanae. Nilitaka kumdanganya lakini niliamua kusema ukweli. “Mimi sijui kuhusu vitu vyake, mara nyingi hufanya na Baba John na Baba Angel (wadogo zake) mimi huwa hanishirikishi.”
Nilijibu kwa ufupi sikutaka kutoa maelenzo mengi lakini ndiyo ulikua ukweli, mume wangu alikua na biashara nyingi lakini nilikua sijui chochote kuhusu biashara zake. Mara nyingi nilikua nikimuuliza anakasirika na kuniuliza kwani unakos a nini hapa? Ili kuepusha ugomvi niliamua tu kukaa kimya.”Si ana na nyumba nyingi lakini au hujui?” Aliniuliza nikamuambia sijui, najua tu tuna nyumba moja ambayo tunakaa. Hapo alionekana kuwa na wasiwasi kidogo.
“Lakini kwanini unauliza hayo mambo Mama?” Nilimuuliza kwani niliona dhahiri kama ananichota akili. Pamoja na kwamba mume wangu alikua si mtoto wa kwanza lakini kwao ndiyo alikua kila kitu, yeye ndiyo alikua msomi zaidi akiwa na PHD, alikua na kazi nzuri na biashara nyingi na ndugu zake pamoja na kazi zao lakini walikua wakimtegemea na alikua karibu na ndugu zake akiwashirikisha kwa kila kitu, mimi nilikua kama mgeni, sikuruhusiwa kuhoji chochote.
Ili kuepusha shari nilikua nabaki kimya tu kwani kila mara nilipouliza alikua akikasirika, hata wakati akifanya vikao nvyake na ndugu zake vilikua vya siri. “Hamna kitu nilitaka kujua tu kama unajua vitu vya mume wako.”
Alijibu kwa mkato na sasa hivi yeye ndiyo alibadilisha mada na kutaka kuzungumzia mambo mengine kabisa. Nilifurahi kwani nilishajua nia yake ilikua kunichota akili na kujua kama nataka kumuibia mwanae. Kadri siku zilivyokua zinaenda hali ya Mama mkwe wangu ilizidi kuwa mbaya, alishindwa hata kunyanyuka na ongea yake ilikua ya shida, kusema kweli tulikua tunasubiri tu lolote kutokea.
Hospitalini walishashindwa na walikua wakimpa dawa mbalimbali za kupunguza maumivu na kumfanya asichoke sana. Siku moja akiwa katika hali ya uchungu aliniita na kunaimbia anataka kwenda Dar, nilishangaa kwani ni muda mrefu alikataa, lakini nilifurahi kwani niliona labda kwakua kaona hali imekua mbaya hivyo kaona ni bora kukubali matibabu. Nilimpigia mume wangu simu ambaye naye alifurahi kwani alijua Mama akifika Dar atapata matibabu zaidi.
Tulifanya mpango wa kwenda na ndege na siku iliyofuata alikua Dar tayari, hatukutaka kupoteza muda, watoto wake wote walikuja kumpokea lakini alitaka kuingia kwenye Gari la Mume wangu na mimi tu. Aliwaambia wengine watafute usafiri mwingine atawakuta nyumbani, kwakua walikuja na gari moja walilazimika kuchukua Tax na sisi tukaondoka na Mama. Mume wangu alikua ashaongea na Daktari Muhimbili ili akija tu apelekwe lakini.
Ile kuingia tu kwenye gari Mama mkwe alimuambia mume wangu ampeleke kwa Baba zake wadogo na Shangazi zake. Mume wangu alikataa na kusema hawezi kwenda huko, alimuuliza kwanini alisema hawezi tu kwakua waliwatelekeza kipindi wakiwa waodgo hawana kitu. Lakini Mama alisisitiza apelekwe na hatakubali kwenda Hospitalini mpaka apelewe huko.
Mume wangu hakua na namna, aliwasha Gari na kuanza kuzungukia nyumba za Baba zake wadogo wawili na Shangazi zake watatu. Lakini cha ajabu tulipofika nnje tu, Mama hakutaka kuingia, alitaka tuone tu na kupita, tulipita katika nyumba zotee na hatukuingia hata moja ndio alimuambia mume wangu anataka kurudi nyumbani kuwaona wajukuu. Alimuambia awapigia simu watoto wake wote kuja na wajukuu nyumbani ili awaone kwa pamoja, mume wangu alifanya hivyo.
Aliendesha Gari mpaka nyumbani lakini alipokaribia hata kabla ya kufika gentini Mama mkwe alimuambia mume wangu asimamishe Gari hatukujua kwanini lakini alifanya hivyo. Huku akiongea kwa shida kutokana na kuchoka kwa ugonjwa na safari alisema. “Unajua kwanini nimewapeleka kwa ndugu wa Baba yako?”
Aliuliza na hatukua na jibu ndipo alipoendelea kwa shida. “Nilitaka uone mali za Baba yako, nyumba zote tulizopitia alijenga Baba yako kipindi niko na yeye, tulikua wote mjini na naamini unafahamu hilo. Wewe ulikua mdogo kukumbuka lakini Kaka zako wanakumbuka.
Baba yako alikua na hela nyingi na aliwajali sana wadogo zake.” Alitulia kidogo na kuomba maji, nilimpa maji akanywa kisha akaendelea. “Aliwaamini ndugu zake na kuwashirikisha kwa kila kitu, Baba yako alikufa kwaajali ya gari, hakufa ghafla alipata ajali na kuumia kiodgo na kabla ya kufa aliwakabidhi nyinyi wanae kwa ndugu zake akiwaamini na kuwaambia wawatunze wewe na ndugu zako. Bado nakumbuka maneno yake, nilikua nnje ya chumba alichokua amelazwa, aliniambia nitoke kwani alitaka kuongea kitu na ndugu zake, nilitoka kama mkiwa na kusimama nnje.
Hakujua kua nasikia lakini aliwaambia kua nyie ndiyo ndugu zangu wa damu, nawaachia wanangu. Nyie ndiyo mtawatunza na kuwalea, mke wangu huyu ataolewa na atakua na maisha yake. Sitaki mali zangu ziondoke nataka zibaki hapahapa kwaajili ya wanangu.” Aliwaaga na kuwakabidhi nyinyi watoto wake kwa ndugu zake. Mama aliongea kwa uchungu huku machozi ya kimtoka, nilimtuliza na kumuambia hakuna haja ya kuongea alinikatisha na kuniambai anataka kuongea.
Kisha akaendekea. “Baba yako alifariki, siku hiyo hiyo, lakini siku hiyo hiyo hata kabla ya kuzikwa ndugu zake walianza kugawa na amali. Hata alikua hajapoa vizuri walipangiana nyumba mpaka nyumba tuliyokua tukiishi na Baba yako alipozikwa Kijijini basi ndiyo ulikua mwisho wenu. Waliwatelekeza na hawakuwasaidia chochote na mimi niliyekua sina kazi nililazimika kurudi Kijijini kuwalea najua mnajua nilivyowasomesha kwa shida mpaka mlipofikia.”
Alitulia mume wangu alimuuliza kwanini unaniambia yote haya Mama. Alimjibu “Nakuambia mwanangu kwakua unataka kufanya kosa kama alilolifanya Baba yako, kuwaamini ndugu zako na kudhani watawapenda wanao kuliko mkeo atakavyowapenda. Baba yako aliwaamini na walimdhulumu na wewe naona unawaamini, umemtenga mkeo hafanyi kazi, hajui mali zako na hajui hata biashara.
Umewaamini ndugu zako, ni kweli wanakupenda sasa lakini usidhani ukifa watawapenda na wanao. Kama huamini mwanangu waangalie Baba zako wadogo na Shangazi zako je waliwakumbuka, nani alihangaika na nyinyi kama si mimi?” alitulia, mume wangu alijaribu kumuambia kua yale mambo sio ya kuongelea pale lakini alimuambia hapana. Wapende ndugu zako wasaidie wafanikiwe, wewe ndiyo mwneye uwezo lakini kama hutamfundisha mkeo kutafuta basi pamoja na mali zako zote watoto wako watateseka kama mlivyoteseka nyiny siku ukifa.
Aliongea kwa shida sana, nguvu zilimuishia, aliomba kupelekwa nyumbani, kule aliwakuta wajukuu na kuwasalimia, hakuka hata masaa mawili alifariki dunia. Baada ya mazishi maneno yake yalimuingia sana mume wangu. Aliyafanyia kazi na kuanza kunishirikisha, ndugu zake walikasirika lakini hakujali, alinishirikisha na nilijua kila kitu. Sijui ni kama Mama mkwe wangu alijua lakini mwaka mmoja baadaye mume wangu alikufa kwa Presha kilikua ni kifo cha ghafla tu.
Baada ya kifo ndugu zake walianza kuzungumzia kuhusu mali, walijaribu kuficha baadhi ya mali lakini walishangaa najua kila kitu, nilisimama kidete na kuwaambia zile ni mali za mume wangu na ni kwaajili ya wenetu. Nilipambana mpaka mahakamani ambapo nilichaguliwa kuwa msimamizi wa mirathi. Walishangaa najua kila mali ya mume wangu hata zile ambazo walikua shea.
Nilipambana sana mpaka kupata haki za wanangu, ingawa walinichukia mwanzoni ila sasa wamenywea na tunaishi vizuri. Ni mwaka mmoja umepita tangu kifo cha mume wangu na na mshukuru Mungu kua kwa kiasi flani nimeweza kusimamia mali zake sijatetereka na namshukuru Mama mkwe wangu kwa hilo pumzika kwa amani Mama mkwe, pumzika kwa amani mume wangu.
%%%
MWISHO