Njombe kuwa mkoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njombe kuwa mkoa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kimatire, May 22, 2009.

 1. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Katika mchakato wa bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu hapo jana Mh.Pinda alisema kuna maombi ya kuwepo kwa Mkoa mpya wa Njombe, pamoja na wilaya kadhaa.Swali langu kwa wadau JF,Serikali inasema sasa hivi inakabiliana na swala la Global Fincial Crisis linaloikabili dunia nzima,Hivyo tubane matumizi.Je huku kuongeza Mkoa na Wilaya kadhaa ndiko kubana matumizi au kuongeza matumizi kwa walipa kodi?
   
  Last edited by a moderator: May 22, 2009
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mzee kabla ya kuhoji gharama nadhani ingekuwa busara kama ungejua sababu za kufanya hivyo. Unaijua vizuri wilaya ya Njombe?unajua hasara inayopatikana kwa ukubwa wa wilaya hii kiutendaji?
   
 3. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja ya uwepo wa mkoa mpya wa njombe ambao utasaidia kuinua maendeleo ya southern corridor, kama wakuu wanapitia humu tafadhari mzee mizengo hii ni fursa chanya kwa wana ulanga magharibi kupata wilaya mpya ambayo itachagua aidha iende morogoro au iringa ama ruvuma. Tunawasilisha
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kwa nini Geita yenye watu karibu watu Milioni 1 isiwe mkoa..kwa kuungana na wilaya kama Chato na zingine za Tabora?

  Mpanda pia ni wilaya kubwa sana!

  Kwa Njombe pengine wamerge baadhi ya Wilaya za Iringa, Mbeya na Ruvuma ziwe mkoa!

  Je swala la kuongeza mikoa naona ni kuongeza tu administrative costs: kwa nini wilaya zisiongezwe kwa kuwa ndiko shughuli za maendeleo hufanyiaka?
   
  Last edited: May 22, 2009
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hivi ni idadi ya watu ndio inafanya Wilaya kugezwa Mkoa?
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ni moja ya kigezo, hutumika vilevile toka katika hadhi ya mji kwenda kwenye Jiji
   
 7. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja. Kwa kumbukumbu zangu hilo sio ombi jipya kwani lilishawahi tolewa miaka ya nyuma japo kuna Kiongozi mmoja(simkumbuki) alipinga wazo bila kutoa sababu za kutokukubaliana. Ni sahihi kuwa kuongeza mkoa kunaambatana na kuongeza administrative cost. Hata hivyo ni vema watu wakatambua kuongeza mkoa ni sawa na uwekezaji wa aina yeyote (kama gharama zikiwa nyingi kuliko mapato then project itafeli/hasara). Ikumbukwe pia kuifanya Njombe kuwa mkoa kutastimulate economy ya pale pia (multiplier effect), hii ni kutokana na ukubwa wa wilaya hii hasa kiutendaji. Of course one of the obvious impact ni kushuka kwa mapato kwa mkoa wa Iringa kwani unategemea sana wilaya hii ya Njombe.

  Wito, kama kunamtu anaweza pata economic profile ya wilaya ya njombe na mkoa wa iringa naomba atuwekee hapa ili tuweze kutoa a detailed economic analysis ya hoja hii. Though meanwhile based on personal observation, this is among a very feasible idea which needs to be fast-tracked.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni upuunzi tu.
  Tunahitaji majimbo ili kurahisha na kuharakisha maendeleo kuliko huu mtindo wa kutenga nchi yetu katika vipande vipande vya kikabila na kuongeza gharama bila maendeleo. Nasema tena kwa hakika na kutoka katika moyo wangu ni upuuzi.
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Kama ni move ya kisiasa kwa ajili ya kukinufaisha chama naweza kukubali. Lakini siamini kama kuna lolote linaloweza linalofanana na kugawanya mikoa. Hivi kuna mabadiliko gani toka manyara ipewe hadhi ya mkoa, zaidi ya kuwapa watu ulaji?
   
 10. g

  geek Member

  #10
  May 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njombe kama wilaya iko productive kwa kilimo na biashara kuliko baadhi ya mikoa mingi ya Tanzania.

  Mimi sina pingamizi kwa Njombe kuwa mkoa, pingamizi langu ni mpango wa kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi kwa Tanzania nzima.

  Majimbo yakiongezwa yataipatia CCM majority ya ajabu, lakini kwa gharama ya kudumaa kwa demokrasia na mzigo wa kuendesha uchaguzi na shughuli za bunge.

  Kisingizio chao ni kuchochea maendeleo, lakini hata Dar Es Salaam yenye wajanja wote wa nchi bado ina matatizo yanayotia aibu ingawa yako ndani ya uwezo wetu kama watanzania. Hii ni mifano tu:-

  - Wanafunzi wanakaa sakafuni

  - Wakazi wanachota maji ya visimani, hakuna maji ya bomba

  - Huduma za zimamoto ni kama hazipo

  - Hospitali wagonjwa wanalala chini

  - Hakuna umeme wa uhakika, mgao ni jambo la kawaida

  We're expanding too rapidly bila kufanya consideration ya kuimarisha miundo mbinu na huduma muhimu kwa umma ziendane na objectives zenyewe.

  Sisi ni watu wa vituko, na vituko tunavipenda. Huu utamaduni wa kusifiana ujinga utakapoisha tutaona mabadiliko, lakini kwa sasa viongozi wa kisiasa ni kama miungu.
   
 11. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  That's true man, of course we still need constituency policy. I suppose Njombe being a Region is still a good proposal and with this policy it can be among the states/constituency.
   
 12. O

  Orkesumet Member

  #12
  May 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Bila ushabiki wowote, kwa wale wanaoujua mkoa wa Iringa na jinsi wilaya zake zilivyojipanga wanaweza kutambua hilo. Uundaji wa mkoa wa njombe unalenga zaidi katika suala la kiutawala zaidi kuliko idadi ya watu. Kimsingi mtazamo wangu hupo katika vipengele vifuatavyo:
  1. kufanya njombe kuwa mkoa itarahisisha ufanisi katika taratibu za kiutawala kwa wilaya kama za ludewa na makete. Hizi wilaya ziko mbali sana na Iringa na inahitaji zaidi ya masaa si chini ya 6 kufika katika wilaya hizi.
  2. serikali inapoteza pesa nyingi kwenye mafuta, marupurupu ya watendaji katika wilaya hizi. Chukua mfano wa wilaya ya ludewa, kupeleka taarifa inamlazimu mtumishi wa serikali kutumia karibu siku nne kuifikisha Iringa na kurudi ludewa. Je kuna safari ngapi za namna hii zinazofanywa na watumishi wa idara mbalimbali za serikali?

  Kwa upande wa maendeleo bado nina shaka kwani hakuna uwiano wa moja kwa moja. Nafikiri ukiangalia kwa upana zaidi 'saving' kubwa inaweza kupatika katika kubadilisha mfumo mzima wa uongozi katika wilaya. Hebu fikiri:
  1. DED ndio kama accounting officer wa wilaya na idara zote ukitoa polisi wako chini ya DED
  2. Mkuu wa wilaya ni cheo cha kisiasa zaidi kuliko utendaji na zaidi haina ufanisi wowote katika kuleta chachu za maendeleo katika wilaya.

  Mtazamo wangu: sioni tatizo la kuongeza mkoa ila nina tatizo kubwa la 'organigram' ya wilaya na mkoa kwa ujumla. Kwa kipindi hiki kuna council 133 bila shaka na wilaya ni 133, sasa tufanye udhanifu ufuatao:
  Kila mkuu wa wilaya anapata Shs 100m - bajeti ya mwaka 133 x 100m = 13,300,000,000
  Kila wilaya ina land/cruiser angalau moja 50 m x 133 6,650,000,000
  Kwa makadirio ya chini wilaya zote zinaweza kuwa na bajeti 19,950,000,000

  Je Shs 20bn haziwezi kuleta mabadiliko katika idara nyingine na tukatoa 'inefficiency' inayotokana na ofisi hii?
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Maombi ni ya muda mrefu,kwa mara ya mwisho Lowasa alikataa wazo hilo. Kutoka Iringa mpaka Njombe inakaribia km 250 hivi na Njombe Ludewa ni km 130 hivi. Kwa hiyo kutoka beach ya ziwa nyasa mpaka ludewa mjini ni km 100 tena. Mkulima huyu ili aende mkoani anakula km 480. Kutoka Dsm mpaka Iringa mjini ni km 510. Kwa wasiojua Iringa inatoka Morogoro mpaka ziwa nyasa.

  Kiuchumi Njombe/Makete/Ludewa hali sio mbaya. Ni kweli Iringa itaathirika kwa mabadiliko haya,lakini watu wa Makete/ludewa watanufaika sana. Wilaya zote tatu ni wazalishaji wazuri sana. Njombe wapewe hadhi hiyo ikiwezekana haraka.
   
 14. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #14
  May 22, 2009
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  I beg to differ with most of you who are in support of this bizarre proposal. Kama suala ni umbali wa wilaya toka makao maku ya mkoa, then kinachotakiwa ni kwa serikali ku-invest katika miundo mbinu ya barabara na njia za kisasa za mawasiliano. Inashangaza kusikia mtu anatolea mfano wa mtumishi wa serikali anayepeleka taarifa toka wilayani kwenda mkoani na kutumia siku nne for that purpose. Why not use fax to send that information? Au kama serikali yetu ingekuwa na watu wenye "akili timamu" then wangehakikisha kila wilaya na kila mkoa zinaunganishwa kwenye mtandao maalum wa serikali ambapo taarifa hata za siri zinaweza kupelekwa kunakotakiwa na hivyo kupunguza gharama na kuharakisha ufanisi.

  Lakini kwa kuwa hakuna mtu yeyote serikalini mwenye nia wala lengo la kuiendeleza Tanzania, na badala yake ni kutafuta mianya ya kula kwa njia za marupurupu ya safari, then tutajikuta tunaongeza idadi ya mikoa, wilaya and with them idadi ya wakuu wa mikoa na wilaya and with them gharama za kuwahudumia hao wakuu.

  This is just SICKENING
   
 15. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni sawa tu.
  Ikiwa mkoa, ndo bajeti zitaelekezwa huko,
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Haya ni makosa. Kama mgawo wa bajeti utaongezwa huko kwa Wabena ina maana kutakuwa na tilt ktk mgawo ambapo mikoa mingine italoose same amount equal to that increment. Kanuni ya system inasema kama bajeti ni ileile, unapoongeza mgawo mahali X ina maana kuna sehemu zitapungukiwa mgawo. Na hili si sahihi.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wazo lako ni zuri.

  Sijui mipango ya mbeleni ikoje kwa hawa magwiji wa TAMISEMI, lakini nimeshuhudia wilaya fulanifulani ambazo wameweza kuinstall internet services zenye spidi ya kuridhisha tu sina hakika kuhusu fax. Nadhani kwa kiasi kikubwa mkazo unabidi utiliwe kwenye kuboresha mifumo ya habari, utunzaji data na training ya watendaji ktk hizi applications. Sehemu nyingi utunzaji na upatikanaji wa takwimu ni tatizo kubwa mno. Nionavyo ni kuwa kama kweli serikali ina nia ya kuleta mabadiliko ya kweli ni vyema ikaweka misingi ya kukusanya takwimu sahihi kila wakati.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, sina hakika na hizo Kms ulizoweka, lakini kama tatizo ni usafiri wa mazao nadhani jibu ambalo litaleta ahueni moja kwa moja kwa common wananchi ni kujenga au kuimarisha barabara.
   
 19. O

  Orkesumet Member

  #19
  May 23, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nitaendelea kutofautiana na wanaopinga njombe kuwa mkoa! tatizo kubwa naona ni ukosefu wa ufahamu wa jinsi utendaji wa serikali ulivyo. Unasema mtu wa ludewa atume fax wakati hakuna umeme (labda wawe wameunganishwa sasa), sasa itatumwa vipi? Pia suala la infrastructure limekuwa tete tu, na si geni kwa watanzania wengi tu. miundo mbinu ni mibovu tu na hakuna jitihada zozote ya kuendeleza! Ukiangalia bajeti imetilia mkazo kwenye spot maintenance ya barabara na sio kuziboresha katika kiwango cha lami barabara za wilaya na sababu kubwa tu tumetegemea zaidi wahisani katika sekta hii! Mi mtazamo wangu ni kuondoa milolongo ya utawala isiyo na tija na savings kuiwekeza katika wilaya husika.
  Pia ni muhimu kuangalia umbali kati ya wilaya moja hadi nyingine. Wengi wetu tumekuwa na experience ya ilala, temeke, kinondoni and it all rosy that umbali siyo kutoka wilaya siyo issue kabisa! Nafikiri, 255 texter inabidi atembelea maeneo husika kuona jinsi hali ilivyo na labda mtazamo wake utabadilika.
   
 20. M

  Malila JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mtu anayeanza safari toka Iringa kwenda Makete kwa basi anatumia zaidi ya masaa nane ili afike (hii ni safari ndani ya mkoa,km 200 zikiwa lami, kipande kingine vumbi),wakati anaye kuja Dsm kwa basi anatumia masaa saba km 500,( hapo kavuka mikoa miwili). Wanaoteseka ni wakulima na wafanyakazi wanaofuata huduma huko mkoani.
   
Loading...