Njia mbadala hizi hapa km hutaki sindano,kijiti,
1. IUCD ya copper (Copper T)
- Haina homoni.
- Inawekwa kwenye mfuko wa uzazi na huzuia mimba hadi miaka 10.
- Baadhi hupata hedhi nzito mwanzoni, lakini ni salama kwa wengi.
2. Diaphragm au cervical cap
- Inawekwa ukeni kabla ya tendo la ndoa.
- Huzuia mbegu kuingia kwenye mji wa mimba.
- Haitumiki sana Tanzania lakini ipo.
3. kondomu za kike (female condoms)
- Hutoa ulinzi kama kondomu za kiume.
- Pia huzuia maambukizi.
Njia sahihi inategemea afya, mahitaji, na maisha yako Kwa ujumla wewe na mwenza wako!