Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Wakuu naomba ku share na nyinyi hii tabia nahitaji msaada for real.

Mimi ni kijana wa miaka 27, na tabia hii ambayo sio ya kuiificha. Weekend hii nilikuwa naona mnamsema Kitwanga lakini Kuna vitwanga wengi JF na mitaani. Kilevi/beer natumia kupita maelezo. Maisha yangu yamekuwa ya kula bata viunga vya jiji la marahaba. salary yote inaishia kwenye vyupa.

Nashindwa kuelewa tatizo ni nini, najaribu kuacha nashindwa. Nisipokunywa nakuwa very decent & smart young man. Lakin nikinywa tu nakuwa chakaramu.Mbaya zaidi imenifanya nisiwe serious kabisa hata kwenye issues ambazo ni very critical. Na offisini nimeanza ku underperform.

Nimekuwa mtu wa mawazo sana nisipokunywa. Kinachonishangaza ni kwamba mchana siwezi kugusa beer. Lakini ikifika saa tatu usiku shetani ananishawishi naondoka kwangu kuelekea viwanja vya mbali. Huko nitapiga kamnyeso mpaka kumi za usiku nikirudi hoi. Pombe ni source of all evils trust me people.Na mbaya zaidi inazeesha sana.

I wish to change, i wash to focus on life. I wish to have a beautiful family Lakin sijui nachomoka vipi. Naweza jizuia wiki Mbili lakini nikizipatia nafidia siku zote ambazo sijapata. This is not normal.

Maji haya ya Mzungu yamenikamata akili mpaka naona soon nitatumbuliwa jipu.I was handsome mpaka namaliza chuo. Nilikuwa nikitembea wasupaaaa (babies) wanani admire. But currently nipo very rough hata kesho sijui nitavaa nini kwenda officin.Sina savings, sina kiwanja, sina mchumba

Jina kubwa maendeleo zero.Nilikuwa na aminika Lakin sasa hivi hakuna anae ni trust including my family members.Nataka toroka kwenye hili pepo chafu. Kama Kuna sehemu ya maombi/tiba ya ki science ya uhakika please naombeni msaada. Na kama mpo young men wa type hii badilikeni kimea sio kitu kizuri.

Note. Hii excuse ya ku control it's not real. Pombe huwezi control, overtime itakuzidia tu.
Mambo ya kunywa huku una stress za kuacha n msalaa...pombe itazid kusulubu we kunywa kadri uwezavyo itakuzuoea tuu..na utajikuta unanyooka fresh usipende kuangalia wanao kubeza we yatwange

Pombe n tamu jamaniii
 
MAMBO VP WANA JF..

MIMI NI KIJANA WA MIAKA 27...NIMEFANIKIWA KUPATA KAZI NZURI TU LAKINI TATIZO LANGU NI ULEVI... NIMEKUWA NIKITUMIA PESA ZANGU VISIVYO... NIMEKUWA MLEVI KUPINDUKIA NIMEJARIBU KUJI CONTROL BIA 3-5 LAKINI NIMESHINDWA... JUZI NIMEKOSWA KOSWA NA AJALI NILIKUA NIKI DRIVE UKU NIMELEWA...

MSAADA JAMANI KAMA KUNA DAWAYOYOTE YA KUACHA KUNYWA POMBE MNISAIDIE IWE MITISHAMBA AU DAWA ZA KAWAIDA... NIOKOENI KIJANA MWENZENU
 
MAMBO VP WANA JF..

MIMI NI KIJANA WA MIAKA 27...NIMEFANIKIWA KUPATA KAZI NZURI TU LAKINI TATIZO LANGU NI ULEVI... NIMEKUWA NIKITUMIA PESA ZANGU VISIVYO... NIMEKUWA MLEVI KUPINDUKIA NIMEJARIBU KUJI CONTROL BIA 3-5 LAKINI NIMESHINDWA... JUZI NIMEKOSWA KOSWA NA AJALI NILIKUA NIKI DRIVE UKU NIMELEWA...

MSAADA JAMANI KAMA KUNA DAWAYOYOTE YA KUACHA KUNYWA POMBE MNISAIDIE IWE MITISHAMBA AU DAWA ZA KAWAIDA... NIOKOENI KIJANA MWENZENU
Wakuu msaada kwa huyu ndg tumpeni namba ya Kalapina apelekwe Soba house Hakuna msaada zaid wa dawa la kuacha pombe! Hiyo kibaolojia tunaita addiction na vgum mtu aliekuwa addiction kuacha pombe kizembe
 
Usiogope, siku ukipata ajari ulevini utaacha. Mimi nililewa nikaendesha gari. Nikasinzia nikiwa nagonga gia, nilistukia nikiwa kwenye mtaro halafu gari halitamaniki halafu llilikuwa la kuazima.

Pombe ziliniisha, kulitoa gereji nilitokwa jasho, nikaapa kuacha pombe, baada ya mwezi nilirudi kwa kasi mpaka leo ni gambe mtu
 
Ulevi umekuwa ni janga la kitaifa...utasikia mara kajisaidia haja zote kwenye suruali,mara kalala mtaroni n.k
Hivi tuwafanyie nn huku kitaa ili wasidhalilike jamani....toa maoni yako hapahapa!
 
hawa ni watu wa kuheshimiwa sana, wanaendesha bajeti ya nchi kwa kiwango kikubwa. Hawa ndio wananunua madawa, wananunua ndege za Ngosha. Usiwadharau hata siku moja.
Shika adabu yako
 
Akishalewa muache mpitishe kwa wahuni kisha mkimbie aje mwenyewe nyumbani....kesho akija bila nguo ujue keshapona huyo....
 
Aisee mi pombe siezi acha nikiapa sinywi tena ndio nazidisha mazima!! Saivi hapa niko maji mbaya mungu tu anisaide niache
 
Njia ya kuacha pombe ni kuacha kwenda baa na kuacha kunywa pombe popote, ni hivyo tuuu, utadanganywa na dawa za kila aina basi tuu kukuibia pesa zako. Wakati unaanza kunywa ulitumia dawa yoyote? Jibu ni Hapana, hivyo basi kuacha pia ni UACHA KUNYWA TUUU baada ya muda utazoea
 
Mimi ni kijana nilianza pombe nikiwa kidato cha nne na nilikuwa nakunywa kawaida tu hata miezi mi nne ilikuwa inapita bila hata kuonja sasa nikaingia chuo na kuanza cheti na kupindi hicho nilikuwa situmii japo nilikuwa naishi na watu wanatumia siku moja rafiki yangu alininunulia, sitasahau na nilikoma kuchanganya bia na konyagi nilizima nilishtuka ni asubuhi.

Nikafanikiwa kuingia diploma hapo sasa nilivyobahatika kupata kazi ya kusimamia pooltable nilianza kunywa hovyo nikishinda kamaritu basi ikatokea nikaanza kupenda pombe haipiti week lazima ninywe mara moja mbili.

(Nafupisha) sasa kwa sasa hivi nimekuwa napenda pombe kiasi kwamba haipiti siku sijatupia kiroba yani saizi bia sipendi napenda viroba tu na pia kila nikijaribu kusema niache nashindwa hata saizi confidence ya kuonge sina hadi nitupia na hata pia kutongoza inakuwa ngumu na pia huwa natetemeka sana kupita kiasi kama nisipo kunywa siku mbili nimejaribu kuacha lakini wapi.

Jamani hakuna anaejua dawa ya hii kitu kweli maana nina malengo mengi sana. nisaidieni ana JF.
 
Back
Top Bottom