Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,238
- 12,753
Ulevi wa pombe haupo wa aina moja. Kuna aina kuu tatu.
1. Hamu kali ya pombe. Ulevi wa aina hii ni ule ambao mtu anakuwa na hamu kali sana ya pombe kiasi kwamba hawezi kufanya wala kuwaza jambo lingine mpaka aipate.
2. Kushindwa kujizuia kutoendelea kunywa. Mlevi wa aina hii akianza kunywa hajui kusema imetosha. Mtu wa hivi anaweza kuwa hana hata hamu ya pombe. Anaweza kwa muda mrefu asifikirie wala kunywa pombe. Lakini mara tu aanzapo kunywa huwa hawezi kujizuia. Atakunywa hadi atazima. Kama alikuwa na pesa ni mpaka ziishe.
3. Aina ya tatu ni pombe kutawala mwili. Mlevi wa aina hii ni kuwa mwili wake hauwezi kufanya kazi bila pombe. Mtu wa aina hii akikosa pombe anakuwa kama mgonjwa. Mtu wa hivi akikosa pombe anaweza hata kufa.
Unaufahamu ulevi wa aina gani?