Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,440
- 1,029
Mchungaji mmoja akiwa katika mji fulani,alikuwa haijui njia ya kwenda posta.Akiwa bado anahangaika,aliwakuta watoto uwanjani wakicheza chandimu(mpira wa makaratasi),akawaomba wamwonyeshe njia ya kwenda posta.Hawakusita,walimpa maelekezo ya kutosha ya jinsi ya kufika posta.Baada ya kusaidiwa,mchungaji aliwashukuru sana wale watoto kisha akawapa mwaliko kesho waje kanisani kwake ili awasaidie kuijua njia ya uzima,njia ya kwenda mbinguni.Watoto wakamjibu kwa kejeli,"we nenda zako huko posta,umeshindwa kuijua njia ya kwenda hapo posta tu,utaijuaje njia ya kwenda mbinguni?"totally impossible!.