Njia tatu za kuweza kuvunja au kutovunja mkataba wa bandari au makubaliano ya bandari kama wanavyoyaita

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
1. Hatuwezi kuurekebisha vifungu vya makubaliano hadi mshirika wetu Dubai akubali.

Njia hii imependekezwa na watu wengi kwamba tuurekebishe mkataba huu na tufute vipengele vinavyo lalamikiwa. Je njia hii inawezekana? Haiwezekani, kwa mkataba huu mshirika wako ni lazima akubali ndipo marekebisho yafanyike.

Mshirika ananufaika na vifungu hivyo tunavyotaka kuvirekebisha hivyo hatoweza kukubali kurekebisha, na hata tukisema anakubali, je, mkataba huo sasa baada ya kurekebishwa utarudi tena bungeni? Kwa sababu huo ulio rekebishwa utakuwa haukupitishwa na Bunge!

2. Kesi Mahakamani kama wanasheria wengi walivyofanya hapa kuna matatizo, kama tunavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu sana kufanya maamuzi, pale kesi itakapo kuja kusikilizwa muda utakuwa umepita na wahusika watakuwa wamesha saini project agreements. Mahakama itashindwa kufanya maamuzi ya haki baada ya muda huo kupita na kwa kuwa uamuzi wake kwa kipindi hicho hautakuwa na maana yeyote ndivyo watakavyo sema.

JINSI YA KUVUNJA NA KUZUIA MKATABA HUU WA BANDARI


1. Kufile case na kuomba inaction ili kuzuia serikali kusign any proporsal about agreement mpaka pale kesi ya msingi iwe imeamuliwa, inategemea kiasi gani wataweza kuwasilisha hoja zao lakini kisheria inawezekana hiyo. Swali ni je, utakapoingia mahakamani utakuwa unachallenge nini?

Huwezi ukachallenge mkataba (IGA) bali utakuwa unachallenge "AZIMIO LA BUNGE NI UNCONSTITUTIONAL" kwasababu limeridhia mkataba ambao ni "unconstitutional" Kwa hiyo azimio la bunge liwe ni "Unconstitutional"kwa kuridhia mkataba ambao ni "unconstitutional" hili ndilo jibu la kisheria kuzuia mkataba huo danganyifu wa bandari.

2. Wananchi wawashinikize na kuwalazimisha Wabunge wao wakae tena bungeni WAREVORKE azimio hilo na kufunga huo mjadala, hapa inategemea na uamuzi wa wananchi.

3. Bunge haliko chini ya Dubai, hata sheria za kimataifa haziwezi kuli zuia ndio maana ya sovereignity of parliament kwa hivyo uamuzi wa Bunge utaheshimiwa na mkataba utazuiwa.
 
Back
Top Bottom