Uchaguzi 2020 Njia pekee ya Mwita Waitara kuwa mbunge wa Bunge lijalo ni kuteuliwa. Hakuna jimbo analoweza kuchaguliwa kwa kura, hana ushawishi wowote

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,106
Huyu Jamaa kwa sasa ni naibu waziri Tamisemi, aliingia bungeni kwa mbeleko ya Chadema 2015, kabla ya "kununuliwa" na ccm kwa bei ya kushangaza, ambapo kwenye hati ya makubaliano (nimeiona) kulikuwa na kipengere cha unaibu waziri .

Hata hivyo mambo yamembadilikia na kwa sasa hakuna jimbo lolote analoweza kushinda ubunge hata kama atapelekwa kwenye majimbo yenye wapiga kura duni ya Mkoa wa Dodoma, hii ni baada ya kushindwa kuiendeleza Ukonga , huku akiwanunulia bia watu wote wanaohoji ubovu wa barabara, (wewe kunywa bia barabara itakusaidia nini?), hata Tarime ambako ndio kwao hawataki hata kumsikia, na hivi karibuni alihojiwa na CCM Mkoa wa Mara kwa kuanza kujipitisha kabla ya wakati.

Njia pekee ya Waitara kuwa Mbunge ni kuomba huruma ya kuteuliwa viti maalum na Rais iwapo CCM iliyokaliwa kooni na wananchi kutokana na ugumu wa maisha itashinda Urais.
 
  • Jibuni hoja zake acheni upigaji wa ramli. Hata Mbowe harudi bungeni vilevile.
Ambaye anaweza kumfanya Mbowe asiwe mbunge ni Mungu pekee , vinginevyo hakuna takataka ya kumzuia .

Hifadhi andiko hili
 
Ufipa mnajipa faraja, hadi mnatia aibu. Chama kinazidi kukimbiwa na wabunge na wanachama, bado tu mnamsapoti DJ? mwambieni ukweli chama kinakufa hicho,
Wanachama wa wapi waliokimbia ?
 
[QUOTE="Erythrocyte, hata kama atapelekwa kwenye majimbo yenye wapiga kura duni ya Mkoa wa Dodoma ,


Futa hiyo sentence hii ni dharau kuwaita wanainchi/wapiga kura
 
Back
Top Bottom