Njia panda ya Rais Samia

love life live life

JF-Expert Member
Sep 12, 2021
2,529
2,894
Ni dhahiri kuwa Uraisi sio kazi ndogo mara kadhaa Rais Samia amenukuliwa akiongea kwa upole na unyenyekevu(sijui kama unatoka moyoni) katika medani za kisiasa.

Mara ya mwisho aliwaasa wateule wake kuchapa kazi na kuwa hatatumia nguvu kuwasukuma
bali atatumia wino kuwanyoosha(akili).

Katika hali isiyotegemewa Rais Samia ameonekana kwa mara ya kwanza akifoka kwa jazba na kulaumu

Awamu zilizopita(kimsingi ni iliyopita kwa ushahidi wa mazingira) japo hakutaka kuweka wazi ni awamu ipi haswaa.

Kinachooonekana ni kuwa Rais Samia hana imani na viongozi wa awamu iliyopita na havutiwi nao hilo sio tatizo

Kwani marais wote huchagua safu ambayo itakuwa na mwelekeo na falsafa za awamu husika ambayo raisi atakuwa na imani nayo.

Tatizo ni kuwa Rais Samia anaonekana kuwa njia panda na hapa ndipo nikakumbuka play ya dillema of the ghost

Kwenye tamthilia hii kuna kijana(Ato Yawson) aliyeenda kusoma ulaya na kurudi na mlibwende afroamerica(Eulalie)

Kwa fahari kubwa huko kijijini kwao Ghana. Kwa masikitiko makubwa kijana huyu hakufikiria ni kwa jinsi gani mlimbwende huyu ataweza kuishi na kuendana na jamii na mazingira yake kitu kilichopelekea culture clush(a situation in which the diverging attitudes, morals, opinions, or customs of two dissimilar cultures or subcultures are revealed) kitu kilichopelekea kuvunjika kwa ndoa yao.

Ni wakati muafaka kwa Rais Samia kuchagua moja aachane na watangulizi wa Magufuli awe huru(huru kweli kweli)

Au akubali kuwa mtumwa wa Magufuli kuwaridhisha magufulist kwa kutenda kama Magufuli.
Kwa vyovyote vile Samia haonekani kuweza kuendelea kufanya kazi na Magufulist kama wafuasi wake watiifu isipokuwa kwa kutaka kulilidhisha kundi hilo tu. Hata kama Magufulist hawa watafanya kazi kwa kiwango gani.

Rais Samia haonekani kuwa na imani nao kwani inaonekana kunaajenda ziko nyuma yao.

Ni wakati sasa umefika kwa Rais Samia kuvuka mto ng'ambo ya pili na kuachana na mtangulizi wake ili aweze kuendelea na safari yake, ili aanze kutengeneza matatizo yake mwenyewe badala ya kuishi kuendelea na matatizo ya mtangulizi wake.

Sisemi kuwa wateule wa Magufuli walikuwa wabaya walikuwa wazuri na walimufaa Magufuli, Samia ni wakati wake wa kuchagua wateule watakao mfaa ili awe huru kuwajibika kwa wateule wake na si kuangushiwa jumba bovu tena.

Yawezekana magufulist(sukuma gang) wasimuelewe/tusimuelewe leo, kesho watamuelewa badala ya kustack sehemu moja.

Namtakia mafanikio mema katika safari yake mpya ninayotarajia anaenda kuianzisha.

NB: Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge.
 
Kunan
Samia. Shughulikia mijizi yote usicheke na nyani. Hata wasukuma wakikuzingua, weee sukumia ndani
Kuna mmoja juzi kaweka mkataba wa bilion 75 na wahindi sasa huyo nae usukuma umemjaa,
Mama kashindwa mwenyewe,
Anacheka na nyani mwenyewe wacha wamtafune,
Wale walio onekana na madhambi ndo anawaweka wamsogezee gurudum hivi inawezekana kweli?
 
Kunan

Kuna mmoja juzi kaweka mkataba wa bilion 75 na wahindi sasa huyo nae usukuma umemjaa,
Mama kashindwa mwenyewe,
Anacheka na nyani mwenyewe wacha wamtafune,
Wale walio onekana na madhambi ndo anawaweka wamsogezee gurudum hivi inawezekana kweli?
Bado hajaweza kuwatambua maadui zake likija suala la ufisadi.
 
Samia. Shughulikia mijizi yote usicheke na nyani. Hata wasukuma wakikuzingua, weee sukumia ndani
Hili neno "AWAMU YA 6" ni lugha tu ya KISIASA na ni MWAMVULI wa kujifichia ili kuepuka JOTO KALI la kisiasa na kukwepa UWAJIBIKAJI. Serikali ya sasa INAMALIZIA ile miaka 5 ya Hayati JPM, lkn Viongozi ni WALE WALE! Tuache PROPAGANDA zisizo na MASHIKO. Kukubali MAKOSA siyo UDHAIFU.
 
Hao waliopiga pesa ndefu wizara ya fedha mbona ni wateule wake,kuanzia waziri na katibu mkuu. Hapo napo sukumagang.
Vipi bodi aliyoivunja ya TPA si zao lake?

Nitajieni rais aliyepita bila kupigia magoti sukumagang,ndo maana Hangaya Kona mbili anarudi Kanda ya sukumagang.
Chezea sukumagang ni Kama upepo huwezi kuuzuia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom