sisi pia tunajifunza mengi toka kwako mwl. usiache kutuweka sawa tunapopinda.......
kiukweli kila mtu anapenda sana kukaa na watoto wake, hasa sisi akina mama. lakini kuna kipindi inabidi kuna mambo pia yaende. hao hao watoto hata kama unawakumbatia sana lakini huwezi kuwapatia vitu wanavyotaka inakuwa shida. mimi huwa najiwekea kila ninapotoka nje ya watoto wangu lazima nikirudi watamani nisafiri tena ili nikirudi wafurahi. kuna siku mtoto wangu aliniuliza kwani mama utasafiri lini? nikamwuliza umenichoka, akasema hapana, nahitaji kitu fulani..... niliishia kucheka tu.
sasa baba akafanya kosa kasafiri akaagizwa kitu, si unajua wababa, ntanunua airport duty free shop, si walipofika hapo ikawa ni mchaka mchaka hakuna cha kupita shop wala nini. kufika home anaulizwa akasema nimeshindwa kununua, akaambiwa tunajua mummy akisafiri atatuletea maana anakoendaga kuna kila kitu, lol