Njia nzuri ya kupambana na rushwa

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,225
56,885
habari wana jf...?
kama tujuavyo rushwa imekuwa kero ktk bara letu la Afrika na kwengineko,sababu zake nazani ni tamaa na umaskini.
kikubwa kilichonisukuma kuandika hii mada ni kukamatwa kwa wala rushwa huku wakiwa wameisababishia serikali hasara kubwa, na hata kama wakiwakamata mharifu huishia jela huku hasara ikiwa palepale ikileta shida serikalini.

Kama wasemavyo waswahili "usipoziba ufa utajenga ukuta".
Ni heri kuzuia mianya ya ulaji rushwa kuliko kusubilia rushwa ishaliwa ndo unagutuka.
Huku kuwafunga wala rushwa ni njia nzuri kwani huleta onyo kwa wengine, lkn mharifu anakuwa tayari amesababisha hasara kubwa.

Hivyo basi binafsi ningependelea serikali izuie mianya ya upatikanaji wa rushwa nazani hapa watakuwa wanapambana na rushwa...
"Heri kinga kuliko tiba"

Wewe kama mdau unashauri ni njia gani itumike ili kupambana na rushwa..?
 
Kwanza Kumaliza Rushwa Tufukue Makaburi Kwanza
Halafu Wafungwe Wote Ndiyo Tuje Sasa
 
Kwanza Kumaliza Rushwa Tufukue Makaburi Kwanza
Halafu Wafungwe Wote Ndiyo Tuje Sasa
acha tuangalie ya sasa,hata kama ukifanya hivyo sizani kama umetatua tatizo coz hasara ishatokea
 
Wangefata mifano ya EFCC, wao wanavuta mali na kesi inakuvaa... Nilisoma moja juzi ntandaoni, nilitamani iwe hapa nchini.
 
Rushwa ni Adui wa haki-nimefundishwa Shule ya Msingi drs la kwanza 1981! na mwl Lumanyika na Binadamu wote ni sawa! ilitumika sana! domo la Siasa Mwl Nyerere aliikazia sana Shuleni! kumweka wazi tawala za magharibi na uhuru na utu wetu! Wadhibiti ndo wanaofanya biashara patakatifu Ikulu tukiwaweka! Njia ya kudhibiti ni Kunyonga kwa Risasi! Report ya CAG inaonyesha Police +mahakama ndo wala Rushwa wakubwa we utakimbilia wapi? Kunyonga unatumia Jeshi la wananchi
 
duh.. kumbe kazi ipo...
 
Rushes dawa yake ni lazima ufukue makaburi kwa sababu harufu ile inasambaa kwa vizazi had i vizazi. Mtake msitake. Lakini mkishaingiza habari ya kulindana hamtaweza kuishinda rushwa. Sisi tuliokulia wakati wa NYERERE ndo tunajua
 
Back
Top Bottom