Njelu Kasaka: Hakuna aliye salama ndani na nje ya CCM

Mbele kwa Mbele.........CCM

Ni kweli mbele kwa mbele, Ila iliwezekana kwa kuwa kulikua hakuna sauti tofauti leo ... sauti hii ipo na inakua kila kukicha ... vitabu vitakatifu vinasema "kweli" ndipo MUNGU anapoishi na ukiusema Ukweli unaumba matokeo....! Tutendelea kuusemea Ukweli na MUNGU atausimamia ... amtegemeae MUNGU hatumii vitisho vya bastola, SMG au Mahakama au Polisi .... ! Hua anaamini tu!

Mfano: Baba wa Taifa letu hatunaye leo, jiulize kwanini mwenyekiti wa CCM Leo hawezi kumrejea matamko ya Nyerere mwasisi wa chama? Kauli zake ni "Ukweli" na hua unatabia ya kuishi na kupambana... anaziogopa ka ukoma kwasababu hawezi kuziishi kwasbabubu ana ubaguzi na visasi moyoni mwake wapo wengi walioangamia kwa ajili yake na km hajui MUNGU amemuinua ili ajirejebishe lakini bado anatumikia ubinafsi wake
 
nimeupenda huu msemo `Adui wa Rais Magufuli n Joseph Pombe Magufuli'hahaha anaambili huyu adui make katiba inadai kuwa rais hashauriwi na mtu yoyote so sio raihc kushaurika kwan katiba inamruhusu kutopokea ushaur wa m2 yoyote! tatizo haya maneno kuntu ktk media platform wanaosoma asilimia wao husoma magazet ya udaku hasa wanawake na watu wa vjjn hawajui kuingia ktk mitandao kulingana na nature ya watanzania,ushaur wangu viongoz wa upinzan puuzen kaul ya rais ya kuto fanya mikutano mpaka 2020 il muende kumsemelea kwa raia huko vjjn lkn msipofanya hvyo wezenu wana2mia kaul ya elimu bure kuwa rubun wanavjj kwan mambo ya bombardier na flyover hata hawayajui huku kwe2!

Tuliza akili kwanza alafu uandike point inayoeleweka
 
Hakika hili ni neno na kila mmoja amkumbushe kila mmoja wetu ili ujumbe huu mzuri umfikie rais na marais waliopita tuizuie Tanzania yetu isiende inakoenda kwan imeshafika Uganda......
Miaka miwili tu ya utawala, TAIFA LIMESAMBARATIKA.....

SWALI LANGU KWA VIONGOZI WA DINI; "....BADO MNATUAGIZA TUMUOMBEE.....????????!!!!!!".
 
It is very true.

Kama imewezekana kwa Mheshimiwa mbunge wa CCM Nape Nnauye siku moja tu baada ya kuvuliwa uwaziri, akatolewa bastola na wanausalama wa nchi hii na kumwamuru arudi kwenye gari yake na haruhusiwi kufanya kikao kile na wale wanahabari ambacho dhumuni kuu lake lilikuwa kuwashukuru wanahabari kwa ushirikiano waliompa katika kipi
ndi alichohudumu kama Waziri wa Habari na Sanaa.

Sasa kama jambo hilo la kuinyeshwa bastola Mheshimiwa Mbunge wa CCM limefanywa hadharani mbele ya camera lukuki za wanahabari.

So what do you expect kwa sisi walala hoi wa mitaani?

Maana yake ni kuwa kwa kila mtanzania ambaye atataka kuikosoa serikali hii ya awamu ya 5, atakuwa anaishi katika mashaka makubwa.....

Ninachokiona kwa serikali hii ya awamu ya 5 ni ukiukwaji wa wazi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibata ya 18 ambayo inatoa Uhuru kwa kila mwananchi kuweza kuwa na Uhuru wa kutoa maoni yake.

inatisha kwa wadau walikuwa crirical sana kwa serikali....siku hizi hawasikiki tena. Kama itapendeza ni bora hii mitandao yote , radio na TV zifungwe zibaki za serkali ili tuishi kwa amani.
 
Robo ya habari nzima ni ya Kasaka, the rest ni ya Zitto ila heading ni ya Kasaka
 
  • Thanks
Reactions: BAK
if there is a leader in any organization, and then compares the incidence of Tanzania and what caused the genocide in Rwanda; That is boil!
 
kasaka-300x151.jpg


MWANASIASA mkongwe ambaye alipata kuwa mwenyekiti wa kundi la wabunge waliohitaji muundo wa Serikali tatu (G55) wakati wa utawala wa awamu ya pili, Njelu Kasaka, amesema hakuna mtu aliye salama ndani au nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano mkuu wa kidemokrasia uliofanyika jana jijini Arusha ambako alikuwa mgeni mwalikwa.

Pasipo kutaja jina la mtu, Kasaka alitumia kauli hiyo kwa kugusia matukio ya kisiasa yaliyojiri katika siku za hivi karibuni.

Moja ya matuko hayo ni lile lililotokea katikati ya wiki hii kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kukabiliana na changamoto ya kutishiwa bastola na mtu anayeaminika kuwa askari kanzu.

“Ingekuwa wakati CCM ilipokuwa imeshika hatamu, suala hili la RC wa Dar es Salaam tayari CCM ingekuwa imeishakaa na kumuelekeza Rais cha kufanya juu ya mkuu huyo wa mkoa,” alisema Kasaka.

Alisema siku hizi hali haiko hivyo ndiyo maana hata Katibu Mkuu wa CCM mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu, alitaka kodi kero zifutwe, lakini ndio kwanza zikaongezwa.

“Ni kwa kuwa CCM ya sasa haina nguvu hizo tena, wapinzani wakiungana na kuondoa tofauti zao wanaweza kuiondoa CCM madarakani,” alisema.

Kasaka ambaye amepata kuwa mbunge, waziri na mkuu wa mkoa, alijitoa ndani ya CCM mwaka 2015 na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mbali na Kasaka, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari hapa nchini sio maadui wa Rais Dk. John Magufuli bali adui yake ni yeye mwenyewe.

Alimtaka Rais Magufuli badala ya kukasirikia vyombo vya habari ambavyo vinafanya kazi kubwa ya kuuhabarisha umma wa Watanzania, yeye binafsi ajitafakari na awe na akiba ya maneno pale anapozungumza.

“Sijui kilichomkasirisha Rais ni kitu gani, mimi binafsi nashangaa, anasema kalamu za waandishi ndizo zitasababisha mauaji ya halaiki kama ilivyotokea katika nchi za jirani, sio kweli, badala ya kurudia rudia kutamka mauaji ya kimbari ya Rwanda, sisi tunamwambia aache na aweke akiba ya maneno.

“Kama kiongozi wetu awe makini, awe mnyenyekevu na ajue hawezi kujua kila kitu, atuunganishe Watanzania, kwa sababu kile kilichotokea huko anakotolea kama somo ni matokeo ya utawala mbovu, ni itikadi ya jamii moja kujiona bora kuliko jamii zingine na ni matokeo ya wananchi kukosa matumaini,” alisema Zitto.

Pia alitumia fursa hiyo kuendelea kulaani kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam cha kuvamia Clouds Media huku akiwa na askari.

“Adui wa Rais Magufuli ni John Pombe Joseph Magufuli, ni kutokana na kuacha kutumia mifumo katika kutawala, matokeo yake viwanda havipanuki, ajira haziongezeki. Akirudi na kutumia mifumo atafanya vizuri.

“Serikali haitakiwi kuhangaika na watu wadogo wadogo waliowekeza mitaji yao na kuajiri wafanyakazi, wala haitakiwi kuwafilisi, bali inapaswa kuangalia, kujadili na kuziba mianya yote ya ukwepaji kodi unaofanyika katika nchi yetu,” alisema.

Akizungumzia dhana ya ujamaa, Zitto alisema tangu ujamaa ulipotupwa miaka 25 iliyopita pengo kati ya walionacho na wasio nacho limeongezeka na kiwango cha umasikini, hasa vijijini kinakua kwa kasi hali inayohatarisha umoja wa wananchi.

Kwa mujibu wa Zitto, hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na sera mbovu za CCM na Serikali yake na hakiwezi kukwepa lawama na shutuma kwani ndio chama kinachotawala hivi sasa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), alisema kuwa amepata maono mapya, kwamba ameona viongozi mbalimbali wa dini; masheikh na maaskofu wakichomwa moto kutokana na kutenda dhambi ya woga.
Lema alisema hayo wakati alipokuwa akitoa salamu za Chadema na kusisitiza umuhimu wa vyama vyote vya upinzani kuungana na kwenda kuwaelimisha wananchi madhara ya hofu na woga unaowakabili.

“Nimepata maono, nimeona viongozi wa dini, mashekhe na maaskofu wakichomwa moto wa jehanamu, nikamuuliza Mungu kwanini, mbona hawa wanachomwa moto, akanijibu kwa sababu ya dhambi ya woga,” alisema Lema.

Source:Gazeti la Mtanzania
Sio ndani ya ccm tu ila kwa pamoja bus tulikopanda hatujui salama yetu maana dereva hatujui katumia nyasi zinazopigwa marufuku au maji meupe ndani ya vifuko vya plastiki.
 
Ccm ni ya mtu mmoja tu kwa sasa nyie wengine mmekalia kuti kavu,mda wowote linaanguka
endelea kujidanganya tu.kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi sana,tunafanya uchaguzi wa ndani ambao wagombea hawatatoa rushwa wala fitna ili kuchaguliwa
 
Mhe alikaririshwa kuwa mauaji ya kimbari Rwanda yalisababishwa na kalamu wakati ukweli ni tofauti za kijamii zilizokuwepo!

Anajenga chuki miongoni mwa jamii anategemea amani au majanga?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom