Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
Mbunge wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya, mkoani Mbeya, Mhe. Masache Njeru Kasaka amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuiamini Serikali Kwa kuwa imeendelea kutekeleza ahadi mbalimbali zilizoahidiwa mwaka 2020
Mbunge wa Jimbo la Lupa Wilayani Chunya amesema, Wilaya ya Chunya imetengewa fedha zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na kuahidi zahanati ya Kijiji cha Nkwangu kata ya Upendo kuwa mmoja wa wanufaika wa vifaa hivyo ili kusogeza huduma za kiafya karibu na maeneo yao.
"Mimi na viongozi wenzangu hatujawaangusha na hatutawaangusha maana tukiwaangusha maana yake tumemwangusha Mhe. Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, jambo ambalo sisi watumishi wenu mliotutuma kuwasemeeni maeneo mbalimbali hatuwezi kufanya hivyo maana hata ninyi ni mashahidi kwamba ahadi tulizo ahidi tunaendelea kuzitekeleza" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa Wilayani Chunya.
Mbunge wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya Mhe. Masache Kasaka, amewataka wananchi wa Jimbo la Lupa kuendelea kuiamini Serikali anayosema imeendelea kutekeleza ahadi mbalimbali zilizoahidiwa mwaka 2020 kupitia ilani ya CCM ikiwemo ujenzi wa zahanati, uboreshaji sekta ya elimu na miundombinu ya barabara.