Msimamo wako ni znz yenye mamlaka kamili, serikali 3 au mkataba.
Hivi karibuni umekata kona na kusema'' wznz wameyataka wenyewe'' nikakuuliza, sheikh Mdondoaji kulikoni mbona waniacha pwani bamvua kubwa hili? Ukanijibu umegundua kitu kwa hawa akina Jusa.
Basi niliposikia neno inshallah nikawa kimya nikisubri habari, ndio hadi leo twaonana tena.
Haya, nijaalie kwanza, na ahli, swaumu na kila jema. Tukae kitako unipe habbari, kama waelekea kule tulikokuwa tunakwenda au umekata kona zaidi. Mie sijatoa tuhma yoyote naeleze kilichojiri tu. Lau kuna sintofahamu, huu ndio wakati unieleweshe nikutake radhi niliposhindwa kukuelewa bdio uungwana.
Karibu.
Nguruvi,
Mwanzoni ni kweli nilikuwa pamoja na wale waliotaka Zanzibar huru. Hii ni kwasababu ninawafahamu wazanzibari na mie nimefanya kazi na kuishi Zanzibar muda mrefu. Ila kuna mambo nimeyaona hayajakawa sawa hasa huku kwenye ajenda ya kudai mamlaka kamili. Hoja hii imegubikwa na ubinafsi na kutokujali maslahi ya baadhi ya wazanzibari wenzao hivyo basi kuendeleza lile lile linaloendelea kwa wanayolalamikia.
Pili hakuna mwenye dhamira ya dhati kuwasaidia wazanzibari kimsingi kuna ukungu mzito umetanda katika hii hoja ya Zanzibar yenye mamlaka kamili. Ukitaka kujua angalau wenye kudai mamlaka kamili either wamekosa madaraka? either wamekuwa ni wahanga wa mapinduzi? either wamekuwa wakiharibikiwa biashara zao baada ya mianya ya ukwepaji kodi kuondoka? Either ni watu waliokosa mvuto wa kisiasa baada ya kufa siasa za kindaki ndaki. Hivyo basi wamejiunga katika uwanja wa marriage of convinience kudai madaraka yao kwa msingi wakiwa wachache watadai vizuri zaidi na hivyo pengine wanaweza kufanikiwa wanachokidai. Baada ya kugundua hilo nimejitoa kwani a. Hakuna madai ya dhati yenye lengo la kumsaidia mzanzibari wa kawaida. b. Ule ubinafsi unaolalamikiwa utaendelea hata kama Zanzibar ikiwa huru.
Kimsingi Nguruvi nimeamua kumuunga mkono Mwanakijiji tuwe na Serikali moja au Dola moja. Hizi habari zenginezo tutazitengeneza taratibu .
Swaumu alhamdulilah inakatika taratibu tunamaliza ya 15. Karibu sana halwa ya lozi na kahawa na pia tende zenye sharbati kidogo huku maeneo ya kariakoo. Nasikia mnataka kuandika kitabu wewe na nduguzo vp mmeshakikamilisha?
Nilikuwapo!!!