No, no, no! True religion must have high view of life! You cannot simply kill somebody simply because he doesn't subscribe to your religion. I like Christianity because it says: honor every human life for, although they are not on right direction according to Bible, but they were also created in the image of God.
Back to the topic now, I badly wait to see southern Sudan independence from nothern colonialism
Naomba nielekeze kitabu ulichonacho wewe wapi nitakipata ili nione iwapo kina hiyo biashara ya utumwa unayoitaka wewe.
Nijuwavyo ni kuwa habari nyingi za biashara ya utumwa afrika mashariki ni za chuki za wamishionari wa kikristo kuwasingizia waarabu kwa nia ya kuudhuru uislamu.
Nakubali kwamba unataka kuleta umoja na mshikamano, ambao ni muhimu kwetu sisi. Lakini angalia ktk hizi topic zinazohusu Waislamu zinavyoshambuliwa na hawa Christians Fundamentalists, kama Max Simba, huyu mpagani aneyejiita Abdulhalim nk.
Mbona nyinyi wabaguzi halafu wajinga!.Ami,
Kuna vijarida vyenu vilivyojaa udini kama Annur, na radio zenu za kidini Radio Heri nadhani wasomaji wake akili zao zimetayarishwa kupenda mada kama zako. Sio hapa please.
Fahamu kuwa Sudan ni nchi iko vitani tangu mwaka 1983. Sababu ya vita ni kuwa watu wa Sudan Kusini ambao si waarabu na ambao hawahitaji kuwa waarabu au Waislamu wanalazimishwa na serikali ya kiislamu ya Sudan kubeba Uarabu na Uislamu. Watu karibu million 4 wamekufa kwa vita hiyo na walio wengi kati ya hao ni wa Kusini ndio waliokufa.
Fahamu pia kuwa kuna watu wapatao million 4 wa Sudan ya Kusini wamekimbia makazi yao kwa hofu ya majeshi ya Serikali, na pia raia 500,000 wa Sudani Kusini ni wakimbizi nje ya Sudan.
Sudan ina mchanganyiko mkubwa wa makabila na tamaduni. Wasudan hao ni waumini wa dini mbalimbali pia. Ni wazi Waislamu ndio wengi asilimia 65, wakifuatiwa na wakristu asilimia 15 na wanaofuata dini za jadi ni takriban 20%. Kitamaduni 52% wanafuata utamaduni wa kiafrika, japo wengine ni Waislamu (kama Darfur), wengine ni Wakristo wa Kusini na Wafuatao dini za jadi. Wanaofuata utamaduni wa Kiarabu moja kwa moja ni kama asilimia 39, na waliobaki wanachanganya.
Makabila yaliyopo Sudan kama nilivyosema ni mchanganyiko mkubwa sana. Kaskazini kuna makabila ya waafrika (weusi) ambao ni waislamu: Wanubi na Wabeja; na magharibi wako Wafur (Watu wa Darfur) ambao nao ni Waislamu pia. Hawa wa Darfur pamoja na kwamba ni Waislamu wanabaguliwa na Waislamu wanaojipa Uarabu pia. Kusini walio wengi ni Wakristu na wanaofuata dini za jadi. Wako Wadinka ambao ni 10% ya Wasudan wote, na kwa Kusini ni 40% ya WaSudan wa Kusini, wapo pia wanuer, Wachollo, Wamurle, Wamandari na Wabaka; pamoja na makabila mengi madogo madogo.
Ni kweli Sudan Kusini kuna mafuta ambayo yanaiingizia Serikali $2 millioni kwa siku, lakini $1million kwa siku zinatumika kwa jeshi tu.
Kwa maoni yangu, Serikali yoyote ambayo haiwezi kukubali tofauti za watu na kujaribu kuwaunganisha kwa kuwafanya waarabu na waislamu kama huko Sudan haitafanikiwa kumaliza umwagaji wa damu. Na kama hawawezi kupokea hizo tofauti, basi mawazo ya kujigawa lazima yawepo, na ni kwa kunusuru maisha ya watu, ambayo yana thamani sana bila kujali rangi wala dini zao.
Nakubali kwamba unataka kuleta umoja na mshikamano, ambao ni muhimu kwetu sisi. Lakini angalia ktk hizi topic zinazohusu Waislamu zinavyoshambuliwa na hawa Christians Fundamentalists, kama Max Simba, huyu mpagani aneyejiita Abdulhalim nk.
Sudan imeweza kuhimili kwa vile inaongozwa na wasomi waliobobea wa kiislamu.Inakuuma kuhusu hesabu ya jeshi.Lakini ni kwa maslahi ya umoja wa Sudan.
Wewe huwezi kunipangia wapi pa kuandika na wapi pa kuishi.
Nikipenda ni hapa na kuishi kwetu Darfur.
Mimi sina hofu wala ubaguzi kama wako.
Ndiyo lugha yao ya kuzaliwa na inayotumika kila sehemu.Tatizo ni nini?.
Ubaguzi wenu kila pahala,hata lugha nayo munaiogopa.
Mapema mwakani kura ya maoni inatarajiwa kupigwa nchini Sudan kuamua mustakbali wa eneo la kusini la nchi hiyo.
Wakati dunia nzima ikipigania kuwa wamoja na maeneo yenye kujaribu kujitenga kama huko Comoro nguvu zikitumika kupinga kujitenga,mambo ni tofauti huko Sudan.
Baadhi ya uongo wa mataifa ya magharibi kuhalalisha kujitenga eneo la kusini lenye utajiri mkubwa wa mafuta ni eti waarabu wanawabagua waafrika.
Hapo chini ni raisi wa Sudan general Omar Al bashir akionesha upanga wake kama silaha ya kupambana na wenye kuitakia mabaya Sudan,akiwa amezungukwa na wasaidizi na walinzi wake.
Nawashauri sana mnaozungumzia maswala ya Sudan ambao hamjawahi kufika, kuishi na kujionea mwenyewe usijitahidi kuelimisha wale ambao wameshafanya hivyo. Nimekaa Sudan zaidi ya miaka mitatu. Je utakubali kuwa hadi leo hii tunavyoongea utumwa bado upo nchi ile?? Hivi unayo habari kuwa wanao watumwa hata kwenye balozi zao leo hii? Tafadhali tafuta kitabu kimetungwa na Msudani wa kusini ambaye alikuwa mtumwa aliyebahatika kutoroka na akaweza kujiendeleza kiasi cha kutunga kitabu "Escape from Slavery" kimetungwa na Fancis Bok. Kuna Mama aliyetekwa nyara na waarabu wa kaskazini mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 12 tu akauzwa na kuteswa sana na mwarabu wa Kaskazini mwishowe akauzwa na kupelekwa kufanya ubalozi wao London ndiko aliweza kutoroka kwa bahati sana na kuwa huru baada ya miaka saba. Nadhani anaitwa Nazer Mende. Iko mifano mingi sana ya hivi karibuni tu. Wapo wa-Sudani wa kusini wengi sana ambao ndugu zao walipotea kwa kutekwa nyara na waarabu wa kaskazini na hawajui walipo. Wapo wanaume wengi ambao wamerudi nyumbani wasikute wake zao na watoto wao, na kukuta tu habari kuwa askari wa kaskazini walivamia na kuondoka nao. Wapo wanawake wengi sana wamepoteza waume zao na watoto kwa mtindo huo huo. Ninaomba sana asiyefahamu mambo ya Sudan asiyazungumzie hapa kijuu juu. tafuta kwanza kufahamu kitu unachoshabikia maana ukikutana na watu waliopoteza ndugu zao uchungu utakaokupata unaweza ukuletee magonjwa yasiyo na tiba maishani. Tafadhali shukuruni Mungu tuko Tanzania nchi yenye ustaarabu wa kuishi pamoja bila kubaguana. Sote tusisahahu kusema "Mungu ibariki Tanzania".