Njaa mbaya wanaume, acha tu wanawake wapende pesa

Njaa mbaya wanaume, acha tu wanawake wapende pesa

Zee Korofi

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2021
Posts
1,604
Reaction score
1,440
Nilijaribu juzi kukaa asubuhi mpaka jioni kwa kunywa chai tu, aisee asikuambie mtu, njaa mbaya! Umasikini mbaya mnooo! Leo nawakingia vifua wanawake, msiwalaumu jamani, tutafute pesa.

Kuna muda unapigwa mzinga mzito, unaishia kulaani kabisa na kumtukana huyo bae wako. Ila jua tu ana wazazi, wadogo zake wanasoma, anauguza wagonjwa, chakula kimekwisha n.k!

Acheni tu! Kwa maruwe ruwe yale niliyoona, acheni tu wanaume masikini SANA wasipendwe, wakifanikiwa huwa ndio wa kwanza kuwatenda waliowavumilia, hawana shukrani tena na huanza dharau na matusi.

Acheni wanawake wapende pesa!!! Tutafute pesa.
 
kwani vizinga ni mshahara kwanini asifanye kazi unatetea ujinga.
Yani mdada mzima ukae kutegemea boyfriend ndo ulishe familia yako ndo maana matundu kila sehemu kwa kupenda vitonga tufanye kazi.
 
kwani vizinga ni mshahara kwanini asifanye kazi unatetea ujinga.
Yani mdada mzima ukae kutegemea boyfriend ndo ulishe familia yako ndo maana matundu kila sehemu kwa kupenda vitonga tufanye kazi.
Matundu kila sehemu?[emoji23]
 
Hapo ndo ulizingua, mwanaume ukiamua kushinda njaa unashinda kweli hakuna kula kitu.
Chai ndo ilikufanya uteseke zaidi.

I remember nilimalizaga mwezi nakula mala moja tu kwa siku usiku peke ake, nashinda njaa kutwa nzima fresh tu yani, njaa inapiga kimtindo ukakaza tuu
 
We mtoa mada mayai kweli. Nakumbuka miaka 5 nyuma kipindi nasoma Udom pale kuna muda boom ilkua inakata mapema sana na sijaweka bill ujasi wala cafeteria, aloo nilikua nashindia FURSANA na MKATE yaani ilikua ni balaa mpaka hata mwezi mzima na unazunguka kuhudhuria vipindi vyote kuna vingine vya college nyingine huko labda Education mimi nlkua Cnms kuna umbali ila unatembea tu mradi uhudhurie. Alafu wewe kidume toto mayai ndembedembe unalia kushinda njaa masaa tu. Tuulize wakulima tunaenda shambani na chupa la maji tu ya kunywa unashinda unalima unakuja kula jioni au usiku alafu ww unashinda ndani na remote unalialia.
 
Come on man. Be creative. Washauri wajiongeze kufanya ujasiriamali wasiwe dependent
Na kazi za kina dada nyingi mno zinalipa kuliko za kiume, ususi, kuuza vijora na madera, kupika keki maandazi, vitumbua, mghahawa, uana mitindo na mapambo n.k

Imeandikwa "YER 17:5 BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA"
 
Hapo ndo ulizingua, mwanaume ukiamua kushinda njaa unashinda kweli hakuna kula kitu.
Chai ndo ilikufanya uteseke zaidi.

I remember nilimalizaga mwezi nakula mala moja tu kwa siku usiku peke ake, nashinda njaa kutwa nzima fresh tu yani, njaa inapiga kimtindo ukakaza tuu
Daaah pole sana, ni lini hiyo? Ukiwa masomoni(chuo) au?
 
Daah yan mwanaume njaa tu tena sio siku moja bali ni masaa unalia lia km mwanamke!!sisi wengine kipind tunachacha tulishawai kulalia biskut ya 200 na tukavunga,yan mkuu njaaa siku moja tu alaf utakuta hapo hauna familia upo mwenyw tu unaon km ni big issue sana!aseh ww unachekesha sana
 
Mtoa mada ni kama unatamani ungekuwa mwanamke
 
Nilijaribu juzi kukaa asubuhi mpaka jioni kwa kunywa chai tu, aisee asikuambie mtu, njaa mbaya! Umasikini mbaya mnooo! Leo nawakingia vifua wanawake, msiwalaumu jamani, tutafute pesa.

Kuna muda unapigwa mzinga mzito, unaishia kulaani kabisa na kumtukana huyo bae wako. Ila jua tu ana wazazi, wadogo zake wanasoma, anauguza wagonjwa, chakula kimekwisha n.k!

Acheni tu! Kwa maruwe ruwe yale niliyoona, acheni tu wanaume masikini SANA wasipendwe, wakifanikiwa huwa ndio wa kwanza kuwatenda waliowavumilia, hawana shukrani tena na huanza dharau na matusi.

Acheni wanawake wapende pesa!!! Tutafute pesa.
Acheni kuwachukulia wanawake ni kupenda pesa mnawaaminisha vijana upumbavu tuu fikiri kabla ya kuropokaa Mkuu
 
Kawaida sana kupiga deshi hata siku moja ,ni nzuri kiafya,ukiwa unakula good time eerday ndio vyanzo vya kisukari ,pressure etc
 
Back
Top Bottom