brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,393
habari nilizozipata punde karibu na uongozi wa Simba zinasema mazungumzo baina simba na niyonzima yako katika hatua ya mwisho kumwaga wino wakati wowote.
Malkia wa nyuki amechukizwa na hatua ya yanga kumsainisha mrisho ngassa na kuongoza msafara ya kulipa kisasa, hii inatokana na yanga kuiona simba kama shamba la bibi kwa kwenda kujivunia wachezaji kama wanavyotaka, sasa ni muda wa kuchukua hatua .
stay tune more to follow....
Malkia wa nyuki amechukizwa na hatua ya yanga kumsainisha mrisho ngassa na kuongoza msafara ya kulipa kisasa, hii inatokana na yanga kuiona simba kama shamba la bibi kwa kwenda kujivunia wachezaji kama wanavyotaka, sasa ni muda wa kuchukua hatua .
stay tune more to follow....
MEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 5:00 ASUBUHI
HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.
Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.
source: BIN ZUBEIRY
Uongozi wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom klabu ya Young Africans leo umekata mzizi wa fitina kwa kiungo mchezeshaji kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kumalizika kwa mkataba wake awali.
Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
Mwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb
source: NIYONZIMA AONGEZA MIWILI YANGAView attachment 94937View attachment 94937View attachment 94937View attachment 94937